SoC03 Njia bora ya kuepukana na mikataba mibovu (Tanzania)

SoC03 Njia bora ya kuepukana na mikataba mibovu (Tanzania)

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Aug 11, 2022
Posts
7
Reaction score
2
Mkataba ni maridhiano baina ya watu wawili au zaidi,serikali kwa serikali,kampuni kwa kampuni au serikali na kampuni.Mikataba nayo husaidia kuinua uchumi wa nchi au kampuni inapokuwa na manufaa kwa nchi husika au kampuni.Pia huweza kusababisha hasara inapokua haina manufaa.

mikataba mibovu ni aina ya mikataba haina manufaa bali huwa ni hasara kwa nchi au kampuni.kuna baadhi mikataba mibovu ambayo serikali ya tanzania imeingia ambayo haina faida katika kukuza uchumi bali imeleta hasara kubwa kwa serikali.

mfano wa mikataba mibovu ambayo serikali imeingia na imepata hasara.
banki kuu ya tanzania (B.O.T) na tegeta escrow. huu mkataba umeisababishia hasara serikali kiasi cha pesa tsh billioni 300 .Wahusika wengine wapo serikali hadi leo na hawajachukuliwa hatua za kisheria.

Kilichofanyika wahusika ni kubadilishiwa vitengo vya kufanya kazi.hii nayo imeisababishia serikali hasara.

serikali inabidi itumie njia zifuatazo ili kuepuka mikataba mibovu.

kuwashirikisha wanasheria na mawakili mbalimbali katika kuchambua vipengele vya mkataba mbalimbali katika mkataba kabla ya kusainiwa na rais. Hii itasaidia panapokuwa na kasoro basi wataweza kugundua na kupafanyia marekebisho na kukiondoa kipengele kinachotiliwa mashaka.

Pia hawa wanasheria na mawakili watasaidia pale muwekezaji aliyeingia mkataba akienda kinyume na mkataba kuweza kuuvunja kulingana na vifungu vya sheria vilivyomo kwenye mkataba na vilikiukwa. Pia hii itasaidia serikali kuepuka kutokupigwa faini au kudaiwa fidia inapofunja mkataba bila kufuata vifungu vya sheria vilivyomo kwenye mkataba.

Kushirikishwa wananchi katika kutoa maamuzi. serikali inabidi iwe inaweka mikataba yote wazi kabla ya kusainiwa ili kuwapa wananchi fursa ya kutoa mawazo yao. Ushirikishwaji wa wananchi katika kutoa maamuzi utasaidia wananchi kujenga imani na viongozi wanaowatawala. Pia hii itasaidia viongozi kujijengea hali ya kujiamini wanapokuwa wanawahutubia wananchi anaowaongoza. Pia itakua rahisi kiongozi kujua matatizo yanayowakumba wananchi anaowaongoza.

ushirikishwaji wa vyama vya siasa katika kutoa maamuzi. Hii ni miongoni mwa njia ambayo itasaidia kuondoa migongano kati ya chama tawala na vile vya upinzani. Serikali inabudi kuwashirikisha viongozi wa upinzani katika kujadili mikataba kabla ya kusainiwa. Ili kusaidia kujua hasara na faida ya mkataba pia kuondoa vipengele vilivyomo kwenye mkataba na havina faida yeyote katika kukuza uchumu. Serikali kuu itapaswa kuheshimu maoni ya vyama vya upinzani bila kujali itikadi ya chama fulani.

Kutokuruhusu mikataba ijadiliwe na watu wachache na kusainiwa kwa ujumla. Hii hali imeipeleka tanzania pabaya kuna baadhi ya mikataba mibovu iliyosainiwa na watu wachache leo hii inasababisha ndege zetu kukamatwa na rasilimali zingine kuzuiliwa. Kunapokuwa na watu wachache inakua ni rahisi kwa muwekezaji kutoa rushwa kwa watu waliopewa dhamana ya kujadili mkataba. hii itapelekea kusainiwa hata kama mkataba ni mbovu bali wao wataangalia maslahi binafsi badala ya nchi. Mfano mchanga wa madini uliokua unasafirishwa ule ulikua ni mkataba mbovu na umeisababishia serikali hasara. Hii inatokana na mkataba ule kujadiliwa na watu wachache na kibaya zaidl walikua sio wazalendo wao walikua wanaangalia maslahi binafsi. Kwaiyo tunaiomba serikali ishirikishe watu wengi wenye uelewa ili kuepukana na mikataba mibovu na kuinusuru nchi na madeni ya fidia.

Serikali kutumia makampuni katika kuingia mikataba mbalimbali. Nchi zilizoendelea zinatumia makampuni kuingia mikataba na nchi mbalimbali. Mfano Dp world hii ni mfano wa kampuni inahusika na uendeshaji wa bandari mbalimbali dunia. Hii kampuni inamilikiwa na nchi iliyochini ya falme za kiarabu (UAE). UAE wanachukua faida kutoka katika hii kampuni lakini ukiishitaki auishitaki nchi bali utaishitaki kampuni ya Dp world. Tunaishauri serikali ibadilike kimfumo badala ya kutumia udhamini wa nchi itumie kampuni ili kuepusha nchi na migogoro aidha na makampuni fulani au nchi fulani. Hii njia itasaidia sana Tanzania hasa katika upande wa mikataba na itaepusha kuingia katika mikataba mibovu na pia itaepusha rasilimali za nchi kutozuiliwa ,kupotea au kukamatwa.

Naishauri serikali iwe inapitia mikataba ya wawekezaji wote iliyoingia nao ili kubaini wanachofanya ni sahihi na ndokilichoandikwa kwenye mkataba. Maana kunamuda wawekezaji wanaingia mkataba wa kumiliki ardhi kwa ajili ya kilimo kumbe lengo lao wapate fursa ya kukopea kwenye mabanki na hawalimi wanachukua mkopo wanaenda kufanya mambo mengine na hata wengine hawalimi wanakata miti mingine wanauza, wanachoma mkaa baada ya hapo shamba wanalitelekeza. wawekezaji wa aina hii wanabidi wachukuliwe hatua kisheria na ikiwezekana wavunjiwe mikataba yao kwa mujibu wa sheria.

Kuna baadhi ya wawekezaji wanakwepa kodi na kunabaadhi ya watumishi wanawajua wanawanyamanzia maana wanapata maslahi binafsi kutoka kwa wawekezaji hao. Kutokana na kosa la kutokulipa kodi umehujumu uchumi nchi adhabu yake n kifungo na faini. Pia wawekezaji kama hawa wavunjiwe mikataba yao bila kujali ujamaa au urafiki fulani

Pia naishauri serikali kuwajibika na kuangalia kwa umakini na ukaribu kabisa mikataba ya madini, bandari, misitu, kilimo na usafirishaji. Maana hizi sekta ni muhimu na ninguzo za uchumi wa nchi. Pia ipitiwe mikataba ya awali irekebishwe nchi isije ingia kwenye mzigo wa madeni kutokana na kulipa fidia zilizosababishwa na watu wachache.

MWANDISHI. Mr Og
 
Upvote 1
Kuna baadhi ya wawekezaji wanakwepa kodi na kunabaadhi ya watumishi wanawajua wanawanyamanzia maana wanapata maslahi binafsi kutoka kwa wawekezaji hao
 
Naomba.
Msaada jinsi ya kuacha maana kama kufilisika nimefilisika now
Screenshot_20230728-161319.jpg
 
Back
Top Bottom