DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Mara kwa mara kumekuwa na malalamiko makubwa saana kuhusu Mapungufu katika sector ya Afya hasa katika nchi zetu za Afrika {Sana sana katika nchi ziitwazo dunia ya Tatu (3rd world countries) Ambazo nyingi zipo katika kusini mwa jangwa la sahara}
Mapungufu hayo katika sector ya afya kwa sasa yanasababisha vifo vinavyokadiriwa kuwa 40% ukitoa magonjwa sugu kama HIV/AIDS ,Malaria na mengineyo ambayo huchangia kwa 60%. "Ukiitoa COVID19 ambayo kwa sasa ndiyo tishio la dunia.
Kwa hiyo kuongelea,kubadili au kurekebisha sector ya afya ili kupunguza vifo huwezi kabisa kufumbia macho hasa katika kutatua ama kupunguza chanzo cha vifo katika jamii yetu hasa Tanzania.
ILI KUREKEBISHA LAZIMA VITU VIFUATAVYO KUFUATWA
1.KUHUSU UONGOZI NA UTAWALA BORA
Kwanza kabisa hii ni sehemu nyeti kwani huwezi kuzungumzia sector ya afya kama huwezi kuzungumzia wasimamizi wa sector hiyo wakiwemo waliopewa dhamana na serikali iliyopo madarakani ikiwemo Waziri mwenye Dhamana ya Afya na Waziri wa Tamisemi na Wengine wanaohusika kwa Karibu na Afya.
Wahusika wote wanatakiwa kuwa committed ikiwemo kutoa ushauri mzuri kwa serikali ili iweze kujikita katika kutatua changamoto kwa Asilimia 95% na Sio kufikiri katika kuongeza vitu vingine ila zaidi kurekebisha vilivyopo..
Katika sehemu hii vipo vichache vya kubadili ili kurekebisha sector hii muhimu.
(a)Sera/sheria /kanuni za afya zinazotumika haziko updated
Sera ya sasa Ya afya ni sera ya mwaka 2007 na haijafanyiwa marekebisho hivyo kutokidhi hali ya sasa ya kiuchumi hasa kwa dunia ya sasa inayoenda kwa technoljia.
Mapungufu ya sera hayo (kwa maoni yangu na nahisi yanahitaji marekebisho )
Ntayataja kwa uchache zaidi.
(I)Sera imejikita zaidi katika tiba sana kuliko kinga
Katika afya tunategemea zaidi kuona mifumo yetu ikijikita zaidi katika kinga na tiba hivyo kuona nchi kubwa kama Tanzania imejikita zaidi "kisera" katika tiba na sio kinga ni kasoro ambayo husababisha majanga mengi kuingia nchini na pengine mengine tunaweza kushindwa kuyamudu kutokananna kishindwa kujikinga nayo kwa mfano magonjwa kama Zika,Dengue,chikungunya na mengineyo ambayo yalisadikika kuingia nchini kwetu labda huenda kungekuwa na sera nzuri iliyojikita katika kinga huenda tungeweza kuact mapema katika kuchukua tahadhari ili yasiweze kutokea ikiwa ni pamoja na kutafuta chanjo na njia zingine na pengine hata Ugonjwa kama COVID19 Tungeweza kuact mapema sana katika kujikinga ama kupata chanjo mapema kwani me nauhakika kabisa katika Tiba Hatuko vizuri kiasi hicho kwani vifaa vingine hatuna au viko pungufu.
(ii)Pendekezo la Msamaha kwa makundi maalumu
Sera ya afya (2007)sera namba 5.4.8.3 ,Sera hii ilikuwa ni sera nzuri sana kwa wakati huo kwani baada ya uchumi kuwa mgumu serikali ilitambulisha huduma ya uchangiaji wa gharama za afya mwaka 1993.hivyo kuweka msamaha kwa makundi hayo kama watoto chini ya miaka mitano kulipunguza sana Vifo vya watoto chini ya miaka mitano (Pongezi kwa hilo saana)
Ila kwa sasa vituo vingi vya serikali vinajitegemea katika kutatua shughuri nyingi ikiwemo manunuzi ya madawa na kujiendesha vyenyewe tofauti na zamani hivyo ongezeko la Wagonjwa wa msamaha linasababisha vituo vingi kushindwa kujiendesha vyenyewe,kwani dawa nyingi na huduma nyingi hutolewa kwa watu wale wenye Msamaha na kituo kupata hasara ama kipato kidogo na hvyo wengi kushindwa kujiendesha,
Pendekezo langu;- Serikali iweke mikakati ikiwemo wale wote walio makundi maalumu ya kisera ione jukuma ikiwemo kuwakatia bima ya afya ili kutopoteza mapato vituoni.
Na pia sheria nyingi za Afya ikiwemo MEDICAL, DENTAL AND ALLIED SCIENCE ACT YA MWAKA 2020 Sio rafiki sana kwa Practitioner wengi.
Pia katika sehemu hii ya uongozi na utawala ningepemda kuomba kuwepo uwazi na uwajibikaji kwa watendaji wote kutoka ngazi ya chini mpaka juu bila kujali hofu wala challenges zozote ikimbukwe hii ni sector nyeti sana.
2.KUONGEZA HAMASA KWA WASOMI WA NYAKATI HIZI KUWEZA KUPENDA KUSOMEA KADA ZA AFYA(KUWEKEZA KATIKA KIZAZI HICHI KATIKA KUIPENDA KADA HII)
Kingine ningeiomba serikali katika kuwekeza katika vijana wanaoibukia katika kuzipenda fani hizi za madaktari manesi na kada zingine za afya ili kuongeza hamasa na kuwaondolea mawazo kwamba fani hizi ni ngumu sana na kujenga Wasomi na wafanyakazi wengi wa sekta hii..Tofauti na kizazi kilichopo sasa hibi ambacho wengine walienda kusomea kwa sababu ya kupata pesa hivyo wakifika kazini na wakakuta tofauti huamua kufnya vitu visivyopendeza
3.KUONGEZA HAMASA KATIKA WAWEKEZAJI
Kuongeza hamasa kwa wawekezaji kufanya uwekezaji katika kujenga viwanda vingi kwa ajili ya Madawa na vifaa mbalimbali vya Hospitali ili kupunguza burden ya serikali katika kuagiza nje.Na pia ili kupata vifaa vingi vyenye technolojia ya juu.
4.UFANYAJI WA TAFITI NYINGI JUU YA MAGONJWA.
Magonjwa mengi huwa hayako static maana yake ni kuwa magonjwa mengi hubadilika kwa dalili na historia,kwa hiyo ili kuboresha sector hii pendekezo langu serikali Kupitia NIMR ijikite zaidi katika kupata wasomi wengi ili kufanya Utafiti,"Research" ili kupata hasa picha za magonjwa mbalimbali na kufundisha wafanyakazi katika sector hizo..ikiwemo kufanya mabadiliko ya Matibabu kwa mfano:natoa sifa sana katika tafiti za malaria zinazopelekea kubadilishwa kwa dawa nyingi na hatimae kupunguza usugu wa dawa.
5.MWISHO UTOAJI WA HUDUMA.
Ningependa utoaji wa huduma katika hospitali ama vituo vyote vya kutolea huduma za afya ziwe zilizo bora ili kufanya Huduma hiyo kusifika tofauti na ilivyo sasa ambapo "negligence" zimekuwa nyingi sana ambazo hazina msingi kwa alimia kama 40% ya vifo vya mama na mtoto husababishwa na negligence za watumishi kwa wagonjwa,hivyo pia utoaji wa huduma uimarishwe ikiwa ni pamoja na kuongeza motisha kwa watumishi.
Ningekuwa na mengi sana ya kuongea ila napenda kuishia hapo
Kwa kumaliza ningeomba serikali ijikite zaidi katika kuimarisha sector hii kwani,Tukiharibu huku tutasababisha vifo,walemavu na magonjwa mengi ambayo yangeweza kuzuilika kwa kufuata taratibu ndogo tu
Asante
Dr Mambosasa Asante

Upvote
5