MgungaMiba
JF-Expert Member
- Aug 28, 2011
- 999
- 816
1. Kwa kuelezea tu aliyoyafanya ndani ya miaka 5 ya utawala wake bila kuelezea faida zake za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa Wapiga kura, haitapatikana impact ya kutosha kuwashawishi Wapiga kura wamkubali. Aidha kunatoa mwanya wa kutosha kwa wanaompinga kuyaponda anayoyafanya na kuonesha hayana maana kwa Wapiga kura bali yanawaongezea ugumu wa maisha tu.
2. Kwa mfano wanawaambia watu walio wengi wa hali ya chini kuwa wao wana shida ya maji lakini zimenunuliwa ndege ambazo hawatazipanda wao bali matajiri tu ndo watazipanda, huduma za afya sio nzuri lakini yeye anajenga reli na madaraja nk.
3. NAMNA NZURI YA KUFANYA;
Kwanza kabisa ni kuorodhesha mambo yote mazuri na makubwa aliyoyafanya kwa mpangilio wa manufaa yake kwa watu (in order of importance to the people)
4. K.m. Kiwango kikubwa cha kusambaza umeme vijijini na faida zake, mashine za kusaga nafaka sasa zinatumia umeme ambapo gharama ya kusaga imeshuka kulingana na ilivyokuwa kwa mashine za dizeli. Minara ya simu vijijini inapata umeme wa uhakika hivyo mawasiliano ya simu yameboreka na kwa unafuu zaidi, kuchaji simu vijijini sio tatizo tena. Matangazo ya Runinga yanapatikana kwa wingi na kirahisi vijijini nk
5. Kila Barbara za lami zilikopita, hasa vijijini, hususan zilizojengwa awamu hii, Wananchi wake waambiwe kuwa gharama kubwa za fedha za kodi zao pamoja na mikopo zimetumika ili wapate unafuu wa kupeleka mazao yao masokoni na unafuu wa nauli wanaposafiri kutokana na kuongezeka kwa vyombo vya usafiri n.k.
6. Kila palipojengwa Zahanati, Kituo cha afya, au huduma za Mobile Clinic, Wananchi wa maeneo hao waambie kuwa serikali imetambua tatizo lao, hivyo hata kama kutakuwa na upungufu wa dawa lakini hawatakosa ushauri wa kitaalam utakao okoa maisha yao, hasa katika huduma za Mama na Mtoto. Sio sawa na huduma hiyo ilipokuwa haipo kabisa, kwakuwa Wapinzani wataponda kuwa huduma haziridhishi.
7. Kwa huduma zote zenye manufaa kama Elimu, Maji, Usalama, Kilimo, nk. kila kilichofanyika katika eneo husika, Makampena waeleze kwa ufasaha kilichofanyika na manufaa yake kwa wananchi, nina imani kila mahali nchini kuna jambo la manufaa limefanyika katika miaka 5 hii. Kadhalika hakuna eneo ambalo limetimia kila kitu, utakuta kwingine wana Maji, Zahanati nk lakini hawana barabara nzuri, kwingine wana barabara nzuri, maji yapo lakini hawana Zahanati n.k. basi hao wakishaelezwa yaliyokwishafanyika waahidiwe kuwa wakishamchagua tena Magufuli, kama alivyotekeleza hayo, basi atatekeleza hayo ambayo bado. Wapinzani hawatazungumzia yaliyokwishafanywa abadan, bali wata focus zaidi kwa yale ambayo bado.
7. Kwa Miradi Mikubwa Ya Kitaifa;
Kwa ununuzi wa Ndege, waambiwe kuwa pesa zitakazolipwa na watakaozipanda, faida itakayopatikana itatumika kuwapelekea huduma za maji vijijini, madawa hospitali nk.
Ujenzi wa SGR utawapatia usafiri wa hakika na nafuu kwa wote wanaoishi inamopita reli hiyo, hivyo kiwango cha biashara na uwekezaji utaongezeka katika maeneo hayo, hivyo kiwango cha maisha kitapanda, aidha mapato ya serikali yataongezeka hivyo kuongeza huduma zake hata kwa wale ambao wako mbali na reli hiyo.
Ujenzi wa Stiegler's Gorge (Nyerere) utawezesha umeme ambao sasa unaenezwa karibu katika vijiji vyote upatikane kwa uhakika na kwa bei nafuu sana kiasi cha watu vijijini pia kuweza kutumia majiko ya umeme, pasi n.k bila hofu ya gharama kubwa, pia serikali itapata mapato makubwa ambayo itayatumia kuboresha Elimu, Afya, unafuu wa kodi kwa wafanyabiashara n.k.
ielezwe hivyo kwa miradi yote mingine ya kitaifa na faida zake za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
8. Ielezwe kuwa udhibiti Mkubwa wa mapato ya serikali na Rasilimali za Taifa uliofanywa na Rais Magufuli umewezesha kutekeleza hayo yaliyofanywa na kumeifanya nchi kuweza kukopesheka.
9. Kazi ya kuyataja mapungufu ya Magufuli waachiwe Wapinzani (Mimi nikiwa mmojawapo) tuna uwezo mkubwa wa kuyaelezea kwa ufasaha na kwa kuyakuza sana, shida yetu tumtoe madarakani yeye na Chama chake ili tutawale sisi.
10. Ni vidokezo vichache tu, hapa siwezi kuandika mada nzima, kwa vile naona wasemaji wengi, akiwemo Magufuli mwenyewe, wamejikita kusema tu tumefanya hili na lile bila kuchambua faida zake, bila kujali eneo wanakoyazungumzia. Ukienda Tandahimba ukaisifia SGR, Lissu akifika huko atazungumzia sakata la Korosho, hatazungumzia umeme uliosambazwa vijijini huko wala miradi ya maji iliyotekelezwa n.k. Lissu ana uwezo mkubwa wa kujieleza kwa ufasaha na ushawishi kuliko Magufuli, lakini Magufuli ana uwezo mkubwa wa kutekeleza dhamira yake. Mipasho mitupu haisaidii sana.
10. Wagombea Udiwani kwa vile wako Kata zote nchini, Rais hatafika Kata zote, hawa wakifundwa vizuri pamoja na Waenezi wa Kata, wanaweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi zaidi, hakutakuwa na haja ya Wasimamizi wa Uchaguzi kupora ushindi wa mtu.
Mpinzani wa Kweli.