Njia gani nzuri ili Tajiri ayachukulie kwa uzito mambo unayomshauri pengine huwa anayasahau kwa sababu ya ana mambo mengi

Njia gani nzuri ili Tajiri ayachukulie kwa uzito mambo unayomshauri pengine huwa anayasahau kwa sababu ya ana mambo mengi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Labda nielezee Kwa mfano ili nieleweke. Kwa mfano unafanya kazi katika kiwanda au kampuni na wewe ni kibarua tu means huonani sana na management ya juu na kila linaondelea juu hujui wala huhusiki tu kwenye mipango yoyote. Hujui uhusiano wao Kwa wao hujui wanayoyasema.

Sasa nyie vibarua kuna hoja fulani mnazo mnazotamani Tajiri azibadilishe hasa mambo ya maslahi kama unavyojua migogoro mingi sehemu za kazi huwa ni kuminyana minyana katika Haki pengine kuna mtu wa karibu wa Tajiri ndo anawaumiza au kuwakata pasina utaratibu wa Haki.

Tufanye sasa Wewe una pata bahati walahu ya kukutanaga na Tajiri mara nyingi ila kama unavyojua Tajiri hazoeleki hata kama mnaonana hupaswi kujiweka karibu kujiendeleza au kulazimisha muwe marafiki sana tuseme mnakutana tu kwenye mambo mengine tu ya kijamii maybe vijiweni au kwenye starehe bar, n. K

Sasa katika kutia stori huwa pia unampa suggestion za kuboresha mifumo fulani kiwandani kwenu na hasa ambayo vibarua mnailalamikia ama kuna mtu wa Juu Kwa maksudi anawakandamiza.. Tajiri Kwa kuwa anaona ni wazo zuri Tena positive anatoa commitment kwamba kuanzia sasa atachukua hayo mapendekezo na kuyafanyia kazi mara moja yaani Kwa wakati huo unaanza kupata matumain kweli Tajiri atayafanyia kazi na atafuatilia jinsi wa chini yake wanavyowalipa na kuwazingatia vibarua..


Cha ajabu miezi inapita na miaka inapita mambo yako vilevile yaani ishu tu ya kimaamuzi ambayo Tajiri ipo ndani ya uwezo wake ila haitimizi. Unaanza kuhisi labda Kwa kuwa huwa anasahau mambo ni mengi ya kampuni au basi labda atakuwa na yeye ni part ya kunufaika kutokana na madhambi ya hao waandamizi wake.unajua unaweza ukahisi na yeye ana husika kwenye ukataji wa maslahi yenu.

Unashindwa uamini lipi unapata Tena nafasi ya kukutana naye unamkunbushia na kweli anaonyesha kabisa yuko aware na hilo suala ila maamuzi tu mepesi hayazingatii Kwa situation kama hiyo ni nini cha kufanya? Je, ni busara kujikalia tu kimya ukaacha mambo yaendelee hivo hivo hata kama yanaumiza au kuna mbinu gani nyingine? je umface Tajiri huku unatoa machozi ili ashtuke na ajue how serious you are with the changes issue.
 
Back
Top Bottom