Njia gani nzuri ya kumsaidia mjasiriamali mchanga kupata mtaji?

Njia gani nzuri ya kumsaidia mjasiriamali mchanga kupata mtaji?

2009-04-01257

Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
13
Reaction score
3
Ndugu katika jamii forum, mimi ni kijana wa kitanzania, nategemea kuhitimu mafunzo ya uhandisi katika fani ya uchenjuaji madini( mineral processing Engineering) mwezi wa sita mwaka huu. kutokana na namna wachimbaji wadogo wadogo wa madini hasa dhahabu kutokuwa na uwezo wa kukamata madini mengi kutoka kwenye udongo wenye madini hayo, nimeona ni vizuri kuanzisha mradi wa kusaga, kuchenjua na kusafisha dhahabu utakaotoa huduma kwa hawa wazalishaji wa dhahabu. na kuzalisha dhahabu yenye ubora unaotakiwa.
Changamoto ninayo dhani itakuwakikwazo kwangu ni upatikanaji wa pesa ikiwa ni mtaji wa kuanzisha mradi huo. kwahiyo wanajamii naomba msaada wenu wa mawazo nini nifanye ilikupata angalau shilingi za kitanzania milioni 20.
 
Naona umeamua kutupia na reg stration # kabisa jembe!!! Back to the point mim nakushauri anza na biznec ndogo ambayo itakusaidia ku raise hiyo capital ya 20 mil badala ya kukomaa kutafuta hiyo by the time unaifikia utakua na xperience ya kutosha juu ya biznec n kuraise other sources of income..huu ni mtazamo tu maana watanzania hatunaga utamaduni wa kumchangishia mtu hela za kuanza biznec..ila harusi nin n nin tunafanyaga..over...!
 
Nenda hospitali kubwa ya moyo ongea na deal na daktari akuandikie nyaraka zinazoonesha kuwa una matatizo ktk moyo hivyo inabidi ufanyiwe oeresheni haraka iwezekanavyo, na gharama za operation ni Milioni 20. Then wajulishe ndugu, jamaa, marafiki na watu wa karibu kuomba msaada wa kifedha. then ukipata fanyia biashara, kisha baada ya mwaka ukifanikiwa, warudishie fedha zao na uwajulishe ukweli na ukatoe sadaka ktk nyumba za ibada ili Mungu pia akusamehe.
 
Hiyo' Ogopasana' ni kali mno, vilevile nikifanya hivyo watu watapoteza imani kwangu milele yote.
 
Usisubiri kupata pesa yote kwa mkupuo,kama una chanzo cha pesa cha kawaida jaribu kuweka si chini ya asilimia 10 kila upatapo pesa,haba na haba hujaza kibaba,usijali itakuchukua muda muhimu usipoteze focus,au kama hauna fanya kama alivyokushauri Lyamber halafu uanze kutenga pesa kwa ajili ya mradi wako.
 
Ulivyo nishauri bwana Nyabaheta ni vizuri , nimekuwa nikitunza pesa kidogokidogo tangu nilipopata wazo hili nikiwa nafanya mafunzo kwa vitendo kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu mwaka 2010. mpaka sasa nimetunza kiasi cha fedha za tanzania 1,000,000. pengine kadiri alivyo sema bwana Lyamber niangalie biashara ya kuanzia kwa mantiki ya kupata uzoefu pamoja na kuendelea na upembuzi yakinifu wa lile wazo kuu.
Asante
 
Ulivyo nishauri bwana Nyabaheta ni vizuri , nimekuwa nikitunza pesa kidogokidogo tangu nilipopata wazo hili nikiwa nafanya mafunzo kwa vitendo kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu mwaka 2010. mpaka sasa nimetunza kiasi cha fedha za tanzania 1,000,000. pengine kadiri alivyo sema bwana Lyamber niangalie biashara ya kuanzia kwa mantiki ya kupata uzoefu pamoja na kuendelea na upembuzi yakinifu wa lile wazo kuu.
Asante

Mdau
Zingatia sana ushauri wa Nyabaheta na Lyamber kwani ni wadau wengi wanafikia malengo yao kwa njia hizo.
Lakini sisi kwa leo tungependa kuzungumzia hii dhana ya CROWD FUNDING. Japo inaonekana kama dhana mpya kwa hapa Tanzania, lakini inafanya kazi.

Je Crowd Funding ni nini? (Tafadhali rejea kwenye kiambatanisho cha picha hapa chini)
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    46.3 KB · Views: 136
Zifuatazo ni baadhi njia za kupata mtaji:


1.Matumizi ya guvu zako kupata mtaji unaweza ukafanya shughuli ambazo hazihitaji pesa kuziendesha kwa mfano kusukuma tolori,kuwa msaidizi wa mafundi,kufanya kazi mauzo ktk site za ujenzi
,kuponda kokoto n.k
2.Kufanya biashara zinazo tumia mtaji mdogo biashara hizo zitakufanya upate mtaji mkubwa mfano kuuza mahindi ya kuchoma,kuuza matunda n,k
3.mikopo kutoka kwa ndugu,jamaa au bank mara nyingi mikopo ya bank uitaji dhamana ya mali fulani lakini hii ya ndugu au jamaa utegemea uaminifu,mahusiano au jinsi unavyo ishinao hao watu.
4.kuomba ndugu au majirani wakuchangie mtaji hii pia ni njia ambayo unaweza kutumia kupata mtaji ingawa ni ngumu kufanikiwa na inamajungu na dharahu pindi inapo onakana unatangaza shida.

kwa kifupi ndo hivyo masikini tufanyavyo kupata mtaji cha msingi huwe mvumilivu na ufanye kazi kwa bidii
 
MKUU OGOPASANA nikweli kabisa sometime we have to break some of the rules(NOT LAW)kwa nia njema yenye tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
 
'start small an grow big, u don't need a million to start a business, u need a focus and a sound plan.'

when u take off money will flow in.
 
Back
Top Bottom