Njia mbadala ya kufidia tozo

Njia mbadala ya kufidia tozo

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Serikali sikivu ya Rais Samia Suluhu baada ya kufanyia kazi maoni ya wananchi kuusu tozo sasa imekuja na njia zitakazofidia tozo njia moja wapo ni kupunguza matumizi ya serikali yasiokua na ulazima ambayo ni:

-Semina zimepunguzwa ili kubana matumizi
-Misafara, (magari) machache kubakizwa
-Miradi itakaguliwa na viongozi wachache
-Chai zitapunguzwa vikaoni ili kubana matumizi

Serikali imeamua kupunguza mzigo kwa Watanzania lengo ni kuwainua wananchi
 
Pia serikali ni kubwa mno, baadhi ya wateule wapunguzwe.

Moja ya kada inayopaswa kupunguzwa ni WAKUU WA WILAYA.

Majukumu ya wakuu wa wilaya yanaweza kutekelezwa na wakurugenzi wa wilaya.
 
Kwani mawaziri wakitembelea Paso kuna shida gani
V8 moja Tsh. 600,000,000

Wenye V8 mpaka sasa...
  1. Mawaziri
  2. Manaibu Waziri
  3. Makatibu Wakuu
  4. Naibu Makatibu Wakuu
  5. Wakurugenzi wa idara za Serikali
  6. Wenyeviti wa bodi
  7. Wajumbe wa Bodi
  8. Wakuu wa Mikoa
  9. Wakurugenzi wa Mikoa
  10. Wakuu wa Wilaya
  11. Wakurugenzi wa Wilaya
  12. Wabunge?
  13. Wawakilishi...
Naomba msaada tafadhalini, endelezeni orodha...
 
Na mbaya zaidi wako wengi, ingekuwa unachagua uzaliwe wapi, kamwe mtu huwezi chagua uzaliwe Tanzania
 
Kwani wameondoa kwenye makato ya kutoa hela kwenye ATm na kwa wakala?? Mbona unasifia tu buree
Hizi ni baadhi ya sehemu zilizofanyiwa kazi
Tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote), kuhamisha fedha ndani ya benki moja, kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine pia tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha
 
Pia serikali ni kubwa mno, baadhi ya wateule wapunguzwe.

Moja ya kada inayopaswa kupunguzwa ni WAKUU WA WILAYA.

Majukumu ya wakuu wa wilaya yanaweza kutekelezwa na wakurugenzi wa wilaya.
acha kiherehere, wakuu wa wilaya Wana kazi kubwa kuliko wakuregenzi
 
Sasa mishahara yao inafanya kazi gani kama hadi chai na sambusa maofisi kwao zinanunuliwa kwa kodi za wananchi hi nchi kuna kitu hakipo sawa
 
acha kiherehere, wakuu wa wilaya Wana kazi kubwa kuliko wakuregenzi

..hoja yangu ni kwamba majukumu ya wakuu wa wilaya yanaweza kutekelezwa na wakurugenzi.

..serikali itaokoa fedha nyingi za walipakodi ikiwa itafuta nafasi za wakuu wa wilaya nchi nzima.
 
Naunga mkono.

Ila kama kumpigia mbuzi gitaa tu.
 
Hizi ni baadhi ya sehemu zilizofanyiwa kazi
Tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote), kuhamisha fedha ndani ya benki moja, kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine pia tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha
fafanua kwenye utoaji hapa mkuu, nimetoa jana makato ni yale yale
 
Sasa mishahara yao inafanya kazi gani kama hadi chai na sambusa maofisi kwao zinanunuliwa kwa kodi za wananchi hi nchi kuna kitu hakipo sawa
Watanzania tupunguze malalamiko ndio maana wameona havina umuhimu wamepunguza kwaajili yetu wenyewe tena bado tuanze kulalamika Rais Samia Suluhu anajitahidi sana kuleta maendeleo na lemgo lake ni kuondokana na mikopo ili nchi iweze kujitegemea
 
Naunga mkono.

Ila kama kumpigia mbuzi gitaa tu.
Hii ni serikali ya utekelezaji lazima itatekeleza na kama umeona nguvu ya umma imesaidia tozo hizi kupunguzwa kwaiyo hii ni serikali inayowasikiliza wananchi wake
 
..hoja yangu ni kwamba majukumu ya wakuu wa wilaya yanaweza kutekelezwa na wakurugenzi.

..serikali itaokoa fedha nyingi za walipakodi ikiwa itafuta nafasi za wakuu wa wilaya nchi nzima.
Huna hoja yoyote, kwa nn majukumu ya wakurugenzi yasitekelezwe na wakuu wa wilaya?
 
..hoja yangu ni kwamba majukumu ya wakuu wa wilaya yanaweza kutekelezwa na wakurugenzi.

..serikali itaokoa fedha nyingi za walipakodi ikiwa itafuta nafasi za wakuu wa wilaya nchi nzima.
Wakuu wa wilaya wapo toka nchi imepata uhuru ndugu yangu na itakuaje wilaya kama hakuna mkuu wa wilaya Rais Samia Suluhu anafanya kazi kubwa tumpe hongera zake ameikuta nchi kwenye janga la corona pia vita vya ukraine vikayumbisha uchumi lakini Tanzania tumeendelea kusimama
 
Back
Top Bottom