SoC01 Njia mbadala ya Tozo ya Miamala ya Simu

SoC01 Njia mbadala ya Tozo ya Miamala ya Simu

Stories of Change - 2021 Competition

lucas meshack

Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
14
Reaction score
8
LUCAS MESHACK

Hivi karibuni serikali kupitia Bunge lilipitisha sheria ya tozo katika mihamala ya simu kwa njia ya simu. Sheria hiyo ilitokana na mapendekezo ya Bajeti ya Serikali 2021/22 pamoja na sheria ya fedha ilipelekea kuweka tozo katika miamala ya fedha inayofanywa kwa njia ya simu, jambo ambalo limeongeza mzigo kwa mwananchi wa kawaida pamoja na wafanyabiashara wadogo na wakubwa.

Kupitishwa kwa sheria hiyo, imedhihirisha kwamba serikali imeshindwa kubuni vyanzo vipya vya mapato kutoka katika vyanzo vya uhakika, kuamua kumfuata mwananchi masikini wa hali ya chini tena anayeishi kijijini, kwa msemo wa sasa tunasema hohehae.

Kupitishwa kwa sheria hiyo pia kumeonyesha kuwa serikali haijamuhurumia wala kumjari mwananchi masikini ambaye anatafuta pesa kwa jasho lenye chumvi huku macho yakiwa na vumbi.

Serikali inapaswa kuja na mkakati kabambe wa makusanyo ya tozo kwenye simu lakini siyo hiki ambacho wamekianzisha cha ‘kumkandamiza’ mtanzania masikini ambaye anategemea kutumiwa pesa au kutoa kutoka kwa mtu mwingine.

Nini kifanyike? Kwanza serikali iongeze ushuru kwenye uagizaji wa simu za mkononi zinazotoka nje kwa wafanyabiashara. Kwa kufanya hivyo itakuwa inapata kiasi Fulani cha fedha ambacho kitasaidia katika ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Kwa mfano wakipitisha sheria kwamba kwenye kila simu moja serikali itachukua Sh. 500, hivyo kwenye simu milioni moja tu zitakazoingizwa nchini kwa siku moja serikali itakuwa imepata Sh.milioni 500, kwa mwezi itakuwa imeingiza Sh. bilioni 15. Wakati huohuo wafanyabiashara hao wa simu wakafidia Sh.500 waliyokatwa kwenye mauzo za simu. Ni hakika hakuna Mtanzania atakayemsikia akilalamika.

Pili, serikali itoze Sh. 200 tu kwenye kila cover za simu zinazoingia nchini, ukichukua kwa makava milioni moja yatakayoingizwa kwa simu maana yake serikali itapata Sh. milioni 200, kwa mwezi itakuwa imepata Sh. bilioni moja. Hakika hutamsikia Mtanzania akilalamika.

Tatu, serikali itoze Sh. 100 kwenye kila protector ya simu inayoingizwa nchini kutoka nje, katika protector milioni moja tu zitakazoingizwa kwa siku serikali itakuwa na uhakika wa kupata Sh. milioni 100 na kwa mwezi itakuwa na uhakika wa kupata Sh. bilioni tatu.

Ni wakati muhafaka sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuja na mikakati mipya ya kupata kodi ambavyo vikianzishwa havitaweza kumuumiza mwananchi masikini.

000000
 
Upvote 1
Back
Top Bottom