UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Baada ya kubaini ukubwa wa tatizo la ukataji wa miti ovyo na kuchambua sababu zake pamoja na wajibu wa wahusika, swali linalobaki ni moja: Je, Tanganyika ina uwezo wa kuokoa misitu yake au itaendelea kushuhudia uharibifu hadi rasilimali hii itakapopotea kabisa?
Uchunguzi unaonyesha kuwa pamoja na ukubwa wa tatizo la ukataji wa miti ovyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, suluhisho lake halipo mbali kama linavyoonekana. Wadau wa mazingira, viongozi wa serikali na wataalamu wa kilimo na uhifadhi wanaeleza kuwa endapo mizizi ya tatizo itashughulikiwa hususan umaskini wa kipato, uzalishaji mdogo wa mazao ya kilimo na utegemezi wa nishati chafu basi kasi ya uharibifu wa misitu inaweza kupungua kwa kiasi kikubwa.
Hivi karibuni, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeanza kuchukua hatua mbalimbali zinazolenga si tu kudhibiti ukataji wa miti kwa nguvu ya sheria, bali pia kubadili mifumo ya maisha ya wananchi ili misitu ilindwe kwa njia endelevu.
Uchunguzi huu umebaini kuwa Tanganyika tayari imeanza kuchukua hatua katika ngazi tatu, usimamizi wa haraka, mabadiliko ya mfumo wa maisha, na uwekezaji wa muda mrefu katika uchumi wa kijani.
Nishati Safi ya Kupikia: Kupunguza shinikizo kwa misitu
Moja ya suluhisho muhimu ni kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia. Serikali, kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imeanza kuchukua hatua za kusambaza majiko banifu na majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma, anasema hatua hiyo tayari imeanza kuleta matumaini.
“Kwa mwaka 2025 pekee, tumegawa majiko ya gesi zaidi ya 350 bure na majiko banifu kwa bei ya ruzuku ya shilingi 7,500. Lengo ni kupunguza matumizi ya mkaa,” alisema.
Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia, Kwa Tanganyika, Halmashauri imejiwekea malengo ya kati, kufikia asilimia 60 hadi 70 ifikapo mwaka 2030.
Hata hivyo, wadau wanasema mafanikio ya mpango huu yatategemea upatikanaji wa gesi, uelewa wa wananchi na kuendelea kwa ruzuku.
Afisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Wilaya ya Tanganyika, Bruno Mwaisaka, anasema pamoja na changamoto za rasilimali, juhudi zimeongezwa ili kufikia maeneo ya ndani zaidi.
Aidha, matumizi ya teknolojia ya kisasa ikiwemo droni yanaangaliwa kama nyenzo ya kuongeza ufanisi wa ufuatiliaji katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma, anasema hatua hizo zina lengo la kuziba mianya ya uvamizi wa misitu na kuimarisha uwajibikaji wa ngazi za chini.
Katika vijiji, viongozi wameanza kuhuisha Kamati za Maliasili ili kupunguza migongano ya maslahi na kuongeza uwazi.
Charles Maembe, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bujombe, anaeleza umuhimu wa kufanya mabadiliko ya mara kwa mara katika uongozi wa kamati hizo ili kuongeza ufanisi na kuondoa upendeleo.
Hatua hizi zinaweka msingi wa udhibiti wa haraka, lakini viongozi wanatambua kuwa ulinzi wa kudumu hauwezi kutegemea doria na adhabu pekee.
Kilimo endelevu kupunguza uvamizi wa misitu
Uchunguzi ulionyesha kuwa bila kuboresha sekta ya kilimo, uvamizi wa misitu utaendelea,wataalamu wamewekeza zaidi katika elimu ya kilimo bora, mbinu za kuongeza rutuba ya udongo na kilimo cha mazao yenye tija kubwa kwenye maeneo madogo.
Mwita, anasema kuongeza idadi ya maafisa ugani ni hatua muhimu.
“Tukiwafikia wakulima wengi zaidi kwa elimu ya kilimo endelevu, shinikizo la kufungua mashamba mapya ndani ya misitu litapungua,” alisema.
Moja ya mikakati inanotajwa kuwa na matokeo ya muda mrefu ni kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, ili wakulima waache tabia ya kufungua mashamba mapya ndani ya misitu.
Katika kukabiliana na hilo, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kimeanza kutekeleza mradi mkubwa wa kuongeza tija ya kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika. Halmashauri imetenga bajeti ya zaidi ya shilingi milioni 400 katika mradi huo unaowalenga wakulima wadogo ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakilima kwa kutumia mbinu za kizamani, hali iliyosababisha mavuno madogo, kipato kidogo na hatimaye kulazimika kukata misitu ili kupanua mashamba.
Akizungumza kuhusu mradi huo, Mhadhiri Mwandamizi wa SUA, Dkt. Proches Msibula, alisema takwimu zinaonesha kuwa licha ya Tanganyika kuwa na ardhi yenye rutuba, uzalishaji wa mazao hususan mahindi umekuwa chini ya kiwango.
“Kupitia mafunzo ya vitendo na matumizi ya teknolojia rahisi, mkulima anaweza kuvuna hadi gunia 14 za mahindi katika nusu heka ya shamba, hii inaongeza kipato bila kuhitaji kufungua mashamba mapya,” alisema.
“Baada ya mavuno, wakulima hawa wanatarajiwa kuwa waelimishaji kwa wakulima wengine vijijini mwao, ili elimu isambae kwa haraka,” alisema mbinu hiyo inalenga kuhakikisha kuwa mabadiliko ya kilimo yanakuwa ya kudumu, na shinikizo kwa misitu linapungua taratibu.
Hamisa Ramadhan anasema mabadiliko ya mtazamo tayari yanaonekana, wakianza kuona kilimo kama biashara badala ya mazoea akisema hatua hiyo ina umuhimu mkubwa kwani mkulima anayezalisha kwa tija hana sababu ya kuvamia misitu.
Kwa wataalamu wa mazingira, mabadiliko ya fikra hizi ni silaha muhimu katika mapambano dhidi ya ukataji wa miti ovyo.
Mikakati ya halmashauri ni zaidi ya doria na faini
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma, amesema Halmashauri imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana na ukataji wa miti ovyo, ikiwemo doria, elimu kwa jamii na ushirikiano na wadau wa mazingira kama Carbon Tanzania, Jane Goodal,The Nature Conservancy, FZS na Taasisi za serikali.
Amesema Halmashauri imekuwa ikitenga asilimia 10 hadi 15 ya bajeti yake kwa ajili ya shughuli za utunzaji wa mazingira, lakini pia imegundua kuwa udhibiti wa kweli hauwezi kupatikana kwa kutumia faini pekee.
“Ndiyo maana tunaunga mkono miradi ya kuongeza tija ya kilimo, kwa sababu mkulima anayevuna vizuri hawezi kuvamia msitu,” alisema.
Ameongeza kuwa endapo mradi wa SUA utafanikiwa, Halmashauri ina mpango wa kuupanua kwenye zao la mpunga na mazao mengine ya biashara kama pamba.
Ushiriki wa jamii ndilo suluhisho la msingi
Karibu viongozi wote waliozungumza katika uchunguzi huu wanakubaliana juu ya jambo moja, bila ushiriki wa jamii, hakuna suluhisho la kudumu. Afisa Mazingira, Bisura, anasisitiza umuhimu wa wananchi kuchukua umiliki wa rasilimali zao.
“Misitu ipo ndani ya vijiji, kama wananchi hawataona manufaa ya moja kwa moja, watakuwa tayari kuharibu badala ya kulinda,” alisema.
Viongozi wa vijiji wanasema juhudi zote hizo haziwezi kuleta matokeo bila ushiriki wa wananchi wenyewe, wanasema jamii inapaswa kuelewa kuwa uharibifu wa misitu unarudi kwao kupitia upungufu wa maji, kilimo duni na umaskini.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Katuma, Yassin Kapaya, anasema kuwa uvamizi wa misitu unaweza kuhatarisha fursa hiyo.
“Tukiendelea kuruhusu watu kuvamia misitu, wawekezaji wa kaboni wataondoka na vijiji vitakosa mapato ya maendeleo,” alisema.
Ndiyo maana miradi kama Carbon inaonekana kuwa suluhisho mbadala, kwa kuwa inahusisha jamii moja kwa moja na kuwapatia mapato kutokana na uhifadhi wa misitu. Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kuwa mafanikio ya mradi huu yanategemea nidhamu ya matumizi ya ardhi na ulinzi thabiti wa maeneo yaliyotengwa kwa uhifadhi.
Biashara ya Kaboni kuunganisha uhifadhi na maendeleo
Mapato hayo yatokanayo na biashara ya kaboni yanatumika katika miradi ya maendeleo ya jamii, jambo linaloongeza motisha ya kulinda rasilimali.
Mwenyekiti Kijiji cha Katuma Kapaya anasema biashara ya kaboni imeanza kubadilisha mtazamo wa wananchi kuhusu misitu, kutoka chanzo cha kuni na mashamba, hadi kuwa rasilimali yenye thamani ya kifedha wakisema huu ni mkakati wa muda mrefu unaounganisha uhifadhi na uchumi wa kijamii.
Matumizi ya teknolojia na doria ili kuimarisha ufuatiliaji
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeanza kuangalia matumizi ya teknolojia ya kisasa, ikiwemo droni ili kufuatilia maeneo yasiyofikika kirahisi.
Mkurugenzi Mtendaji Juma anaeleza kuwa teknolojia inaweza kusaidia kuziba mianya ya uhalifu.
“Baadhi ya wananchi hutumia mwanya wa timu za doria kushindwa kufika maeneo ya mbali na kuanzisha mashamba haramu, ikiwemo ya bangi, teknolojia inatusaidia kubaini mapema,” alisema.
Aidha, ushirikiano kati ya Halmashauri, TFS, TANAPA na vyombo vya usalama unaelezwa kuwa ni nguzo muhimu katika udhibiti wa uvunaji haramu wa mazao ya misitu.
Hitimisho
Uchunguzi unaonyesha kuwa Tanganyika ina mikakati ya kina inayogusa mizizi ya tatizo ili kuimarisha usimamizi, kubadili matumizi ya nishati, kuongeza tija ya kilimo na kuunganisha uhifadhi na mapato kupitia biashara ya kaboni.
Changamoto iliyobaki ni kuimarisha utekelezaji, kuongeza uwazi katika ngazi za chini na kuhakikisha jamii inaendelea kuwa sehemu ya maamuzi. Kwa kuzingatia hatua zinazoendelea, Tanganyika ina msingi wa kujenga mfumo wa uhifadhi unaolinda misitu huku ukiimarisha maisha ya wananchi.
Mwelekeo huu unaonyesha kuwa suluhisho halipo kwenye adhabu pekee, bali katika mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yanayowezesha jamii kulinda rasilimali zao kwa hiari na kwa manufaa ya moja kwa moja.
ANDIKO LA: Swaum Katambo – Tanganyika
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS.
Uchunguzi unaonyesha kuwa pamoja na ukubwa wa tatizo la ukataji wa miti ovyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, suluhisho lake halipo mbali kama linavyoonekana. Wadau wa mazingira, viongozi wa serikali na wataalamu wa kilimo na uhifadhi wanaeleza kuwa endapo mizizi ya tatizo itashughulikiwa hususan umaskini wa kipato, uzalishaji mdogo wa mazao ya kilimo na utegemezi wa nishati chafu basi kasi ya uharibifu wa misitu inaweza kupungua kwa kiasi kikubwa.
Uchunguzi huu umebaini kuwa Tanganyika tayari imeanza kuchukua hatua katika ngazi tatu, usimamizi wa haraka, mabadiliko ya mfumo wa maisha, na uwekezaji wa muda mrefu katika uchumi wa kijani.
Moja ya suluhisho muhimu ni kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia. Serikali, kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imeanza kuchukua hatua za kusambaza majiko banifu na majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma, anasema hatua hiyo tayari imeanza kuleta matumaini.
“Kwa mwaka 2025 pekee, tumegawa majiko ya gesi zaidi ya 350 bure na majiko banifu kwa bei ya ruzuku ya shilingi 7,500. Lengo ni kupunguza matumizi ya mkaa,” alisema.
Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia, Kwa Tanganyika, Halmashauri imejiwekea malengo ya kati, kufikia asilimia 60 hadi 70 ifikapo mwaka 2030.
Hata hivyo, wadau wanasema mafanikio ya mpango huu yatategemea upatikanaji wa gesi, uelewa wa wananchi na kuendelea kwa ruzuku.
Kuimarisha ulinzi na nidhamu ya usimamizi
Katika ngazi ya kiutawala, Halmashauri imeendelea kuimarisha doria kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) pamoja na Askari wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika doria mbalimbali, kwa lengo la kudhibiti uvamizi kwenye maeneo ya misitu ya hifadhi.Afisa Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Wilaya ya Tanganyika, Bruno Mwaisaka, anasema pamoja na changamoto za rasilimali, juhudi zimeongezwa ili kufikia maeneo ya ndani zaidi.
Aidha, matumizi ya teknolojia ya kisasa ikiwemo droni yanaangaliwa kama nyenzo ya kuongeza ufanisi wa ufuatiliaji katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma, anasema hatua hizo zina lengo la kuziba mianya ya uvamizi wa misitu na kuimarisha uwajibikaji wa ngazi za chini.
Katika vijiji, viongozi wameanza kuhuisha Kamati za Maliasili ili kupunguza migongano ya maslahi na kuongeza uwazi.
Charles Maembe, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bujombe, anaeleza umuhimu wa kufanya mabadiliko ya mara kwa mara katika uongozi wa kamati hizo ili kuongeza ufanisi na kuondoa upendeleo.
Hatua hizi zinaweka msingi wa udhibiti wa haraka, lakini viongozi wanatambua kuwa ulinzi wa kudumu hauwezi kutegemea doria na adhabu pekee.
Kilimo endelevu kupunguza uvamizi wa misitu
Uchunguzi ulionyesha kuwa bila kuboresha sekta ya kilimo, uvamizi wa misitu utaendelea,wataalamu wamewekeza zaidi katika elimu ya kilimo bora, mbinu za kuongeza rutuba ya udongo na kilimo cha mazao yenye tija kubwa kwenye maeneo madogo.
Mwita, anasema kuongeza idadi ya maafisa ugani ni hatua muhimu.
“Tukiwafikia wakulima wengi zaidi kwa elimu ya kilimo endelevu, shinikizo la kufungua mashamba mapya ndani ya misitu litapungua,” alisema.
Moja ya mikakati inanotajwa kuwa na matokeo ya muda mrefu ni kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, ili wakulima waache tabia ya kufungua mashamba mapya ndani ya misitu.
Katika kukabiliana na hilo, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kimeanza kutekeleza mradi mkubwa wa kuongeza tija ya kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika. Halmashauri imetenga bajeti ya zaidi ya shilingi milioni 400 katika mradi huo unaowalenga wakulima wadogo ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakilima kwa kutumia mbinu za kizamani, hali iliyosababisha mavuno madogo, kipato kidogo na hatimaye kulazimika kukata misitu ili kupanua mashamba.
Akizungumza kuhusu mradi huo, Mhadhiri Mwandamizi wa SUA, Dkt. Proches Msibula, alisema takwimu zinaonesha kuwa licha ya Tanganyika kuwa na ardhi yenye rutuba, uzalishaji wa mazao hususan mahindi umekuwa chini ya kiwango.
“Kupitia mafunzo ya vitendo na matumizi ya teknolojia rahisi, mkulima anaweza kuvuna hadi gunia 14 za mahindi katika nusu heka ya shamba, hii inaongeza kipato bila kuhitaji kufungua mashamba mapya,” alisema.
Mashamba darasa kuwa Elimu inayozalisha mabadiliko
Nhunda anasema mradi huo umejikita zaidi katika kujenga uwezo wa wakulima kwa vitendo akisema SUA imeanzisha mashamba darasa kwa wakulima viongozi 240 kutoka vijiji nane vya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, wakulima hao wanapatiwa mafunzo ya maandalizi bora ya shamba, matumizi ya mbegu bora, mbolea, udhibiti wa magonjwa na uvunaji wenye tija.“Baada ya mavuno, wakulima hawa wanatarajiwa kuwa waelimishaji kwa wakulima wengine vijijini mwao, ili elimu isambae kwa haraka,” alisema mbinu hiyo inalenga kuhakikisha kuwa mabadiliko ya kilimo yanakuwa ya kudumu, na shinikizo kwa misitu linapungua taratibu.
Mabadiliko ya mtazamo kwa wananchi
Wakulima wanaoshiriki katika mradi huo wanasema elimu waliyoipata imeanza kubadilisha mtazamo wao kuhusu kilimo, wanasema awali walilima kwa mazoea, lakini sasa wanaanza kuona kilimo kama biashara inayoweza kuwapatia chakula cha uhakika, kipato na uwezo wa kugharamia mahitaji ya familia.Hamisa Ramadhan anasema mabadiliko ya mtazamo tayari yanaonekana, wakianza kuona kilimo kama biashara badala ya mazoea akisema hatua hiyo ina umuhimu mkubwa kwani mkulima anayezalisha kwa tija hana sababu ya kuvamia misitu.