Njia nzuri ya kuachishwa shule 'NI KUPIGA MWALIMU'

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,372
Reaction score
54,943
Habarini wanafunzi wenzangu!

Nilianza masomo ya awali mwaka 2012 baada ya jirani yangu mmoja kuniambia kuwa kuna shule moja nzuri sana hapa mjini, hivyo nasaha zake zikanivuta na kuanza shule ya sekondari (Jani la Furaha). 2015 nilipewa namba ya mtahiniwa na nikawa huru kusoma shuleni hapo hadi leo masomo yangu yanaendelea ila naona kuna uonevu shuleni hapa inabidi niache shule sasa.

Wakati naingia shuleni hapo nilisoma kwa uhuru sana na kufanya vitu vyangu bila kuingiliwa na mtu yeyote yule, kuna kipindi baadhi ya waalimu walikuwa wanataka kuingilia masuala yangu na nilikuwa nawaonya sana kuwa waache sitaki kuingiliwa kwa kile ninachokiamini, kuna shule nyingi za kusoma ila waalimu wakiona nipo kwenye 'haka kashule kao ka kata' basi wanachukulia kwamba hiki kishule chao huwezi kukiacha kwa vile wanajua kina ulevi wa ngono ndani yake, hivyo watatukamata kwa kishawishi hicho. Mimi niwaambie uongozi wa shule kuwa sina ulevi wowote shuleni hapa zaidi ya kutaka kuwa huru na nisiingiliwe katika masomo.

Juzi nilikuwa nina shida, ikabidi niende ofisini kwa mwalimu mkuu na wenzake kadhaa, nikaonana nao na kuwaambia tatizo langu ila cha ajabu walikaa kimya kama hawajanisikia, jambo ambalo kwangu mimi naliona kama dharau ya kiwango cha juu sana kuwahi kutokea katika historia ya maisha yangu.

Sasa basi ninaamua kitu ambacho kitanipa uhuru na shuleni wajue kuwa ninaweza kufanya chochote ili tu kulinda heshima yangu dhidi ya waalimu.

NATANGAZA VITA DHIDI YA WAALIMU ILI NIFUKUZWE SHULE HARAKA IWEZEKANAVYO. Nataka nifukuzwe shule moja kwa moja siyo kusimamishwa masomo.

Njia ya haraka ni kupiga/kutukana Mwalimu.

Asanteni.
 
Sawa James Delicious
 
Naamini watakusikia, na kujiepusha na hiyo mijigumi👊👊👊 kabla haijawafikia mana kifo kipo karibu sana usije ukawaua bule.
 
Ulishindwa nini kumalizana nao palepale. Ungemkunja hata mmoja pale wangekuheshimu huku hawapo hawawezi kukusikia

Enzi zangu waliniita ghost natembea na nyembe nilishawahi litoa alama shavu la T. O. D(teacher on duty) nlkuwa ukinizingua sirembeshi awe ticha au student

NB : nliishia kufukuzwa hio shule hizi tabia ni mbaya
 
Inabidi kianzishwe chuo cha uandishi?
Bora ungemshauri aende DSJ [emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
 
Angalia usije kutana na teacher wa miraba minne ukaishia kula kichapo kizito na shule usifukuzwe.
Kama mwalimu Msigwa [emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
 
Moderators
Umetoka kaburini kuja kuita moderators 😝😝😝😝 nadhani familia yako au kwa wazazi wako na hata marafiki wa karibu ni watu wenye matabasamu 24HRS

Ngoja nikutafutie namba za Mr beneficial
 
Umetoka kaburini kuja kuita moderators [emoji13][emoji13][emoji13][emoji13] nadhani familia yako au kwa wazazi wako na hata marafiki wa karibu ni watu wenye matabasamu 24HRS

Ngoja nikutafutie namba za Mr beneficial
sijaelewa mkuu. ..
 
ukiwa kilaza huna faida shule kila siku wewe ni wa mwisho

hata ukijamba tu unaweza shtuka umefukuzwa kwa utovu wa nidhamu

ila ukiwa GENIUS hata upige walimu staff nzima HEAD MASTER atakuombea msamaha

hata ufanye kosa la namna gani kamwe hutofukuzwa hiyo shule

japo shule chache zenye misimamo (watakufukuza bila hiyana)

ila hizi shule ambazo wanaamini wewe ndio matokeo yako yataipaisha shule

asee hufukuzwi ng'o ,utapambana na adhabu zote ila sio ufukuzwe
 
Back
Top Bottom