Mbao za Mawe
JF-Expert Member
- May 11, 2015
- 23,372
- 54,943
Habarini wanafunzi wenzangu!
Nilianza masomo ya awali mwaka 2012 baada ya jirani yangu mmoja kuniambia kuwa kuna shule moja nzuri sana hapa mjini, hivyo nasaha zake zikanivuta na kuanza shule ya sekondari (Jani la Furaha). 2015 nilipewa namba ya mtahiniwa na nikawa huru kusoma shuleni hapo hadi leo masomo yangu yanaendelea ila naona kuna uonevu shuleni hapa inabidi niache shule sasa.
Wakati naingia shuleni hapo nilisoma kwa uhuru sana na kufanya vitu vyangu bila kuingiliwa na mtu yeyote yule, kuna kipindi baadhi ya waalimu walikuwa wanataka kuingilia masuala yangu na nilikuwa nawaonya sana kuwa waache sitaki kuingiliwa kwa kile ninachokiamini, kuna shule nyingi za kusoma ila waalimu wakiona nipo kwenye 'haka kashule kao ka kata' basi wanachukulia kwamba hiki kishule chao huwezi kukiacha kwa vile wanajua kina ulevi wa ngono ndani yake, hivyo watatukamata kwa kishawishi hicho. Mimi niwaambie uongozi wa shule kuwa sina ulevi wowote shuleni hapa zaidi ya kutaka kuwa huru na nisiingiliwe katika masomo.
Juzi nilikuwa nina shida, ikabidi niende ofisini kwa mwalimu mkuu na wenzake kadhaa, nikaonana nao na kuwaambia tatizo langu ila cha ajabu walikaa kimya kama hawajanisikia, jambo ambalo kwangu mimi naliona kama dharau ya kiwango cha juu sana kuwahi kutokea katika historia ya maisha yangu.
Sasa basi ninaamua kitu ambacho kitanipa uhuru na shuleni wajue kuwa ninaweza kufanya chochote ili tu kulinda heshima yangu dhidi ya waalimu.
NATANGAZA VITA DHIDI YA WAALIMU ILI NIFUKUZWE SHULE HARAKA IWEZEKANAVYO. Nataka nifukuzwe shule moja kwa moja siyo kusimamishwa masomo.
Njia ya haraka ni kupiga/kutukana Mwalimu.
Asanteni.