Njia Panda.

Njia Panda.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Kwa kipindi cha nyuma,michezo ya jukwaani ilikuwa ni sehemu ya Sanaa ilopata umaarufu sana nchini kutokana na jinsi michezo hiyo ilivyokuwa na nguvu kubwa ya kuiteka jamii ya watanzania katika kuwaburudisha,kuwaelisha na kuwafurahisha.
Wasanii mbalimbali na watu wenye vipawa vya kuandika michezo hiyo na tamthilia walijikita katika sanaa hii kuonyesha uwezo na umahiri wao katika kubuni na kutunga michezo ambayo itapendwa na watanzania wengi na watu wengine toka pande tofauti tofauti za ulimwengu huu.
Mbali na kutunga,pia wataalamu mbalimbali walijikita katika katika kufundisha wasanii wa michezo hiyo ya jukwaani na kuona ni namna gani Wanaweza kulitumia jukwaa Hadi wakaweza kuigiza michezo hiyo.
Katika mwaka 1987,ndugu E.K. Katikiro aliandika kitabu kuhusu maigizo kitabu ambacho kiliitwa "Misingi ya Maigizo" akielezea historia ya Sanaa ya maigizo ya filamu,aina za michezo yenyewe huku kikubwa akifundisha aina ya majukwaa ya kuigizia michezo hiyo majukwaa ambayo Hata Leo kila anaejifunza sanaa hii katika makundi yeyote ya Sanaa nchini basi atapata nafasi ya kufahamu iwapo tu atakutana na waongozaji wazuri wa mazoezi.

................NJIA PANDA............
Henry Muhanika ni mmoja kati ya wapenzi wa sanaa za michezo ya maigizo ambae aliamua kuchukua jukumu na kutumia kipaji chake pale alipoandika mchezo uitwao "Njia Panda" katika ka mwaka 1981.
Mchezo ambao ulikuwa ukielezea maisha ya mchungaji anaeamini katika Mungu na kuamini kuwa hata familia yake huishi maisha ya imani kama yeye.
Mchungaji Emanuel anatajwa katika mchezo huu kama mtu mwenye imani imara ndani ya moyo wake ambae anaamini kuwa hata familia yake ina imani kama yake.
Mchungaji Emanuel licha ya kuwa na imani ya mungu,hakubaliani Hata kidogo na imani za waganga lakini hajui kuwa mke wake licha ya kuwa mke wa mchungaji lakini anaamini katika ushirikina na Hata kufanya ramli ili kufahafamu mambo mbalimbali kuhusu familia yake.
Mke wa mchungaji Emanuel anaitwa Zabeti anaishi maisha akiwa na siri kubwa ya mtoto wao wa kwanza ambae alimpata baada ya kunywa dawa za kiganga.
Mbali na kuwa na imani za kishirikina,Zabeti pia ana mahusiano ya kimapenzi na mchungaji mwingine ambae ni rafiki wa mchungaju Emanuel.
Kawini ambae ni mtoto mkubwa wa mchungaji Emanuel anagundua siri anatishia kuitoa lakini baadae anaamua kuunyamazia na kutokumwambia baba yake.
Siri inabaki kuwa sisi huku mengi yakifanyika na hatimae mganga wa kienyeji anakuja kutoa siri hiyo.
Je nini kilitokea,mchungaju Emanuel alimfanyaje mchungajji mwenzake ?
Je aliachana na mke wake ?
Siri nyingine mpya inafichuka kuwa Kawini kapewa ujauzito na mwalimu Kassimu ambae ni Muislamu,je mchungaji ataruhusu binti yake kuolewa na muislamu.
Majibu yote ni ndani ya kurasa sitini na nne za "Njia Panda".

WAHUSIKA WA MCHEZO:
Mchungaji Emanuel.
Mchungaji Yohana-rafiki wa mchungaji Emanuel
Zabeti-mke wa mchungaji Emanuel.
Kawini-binti yake mchungaji Emanuel.
Antoni-mtito wa kiume wa mchungaji Emanuel.
Audax-mtumishi wa mchungaji Emanuel
Roza-mdogo wa mchungaji Emanuel.
Kassimu-mwalimu.
Sungura-mwalimu
Mganga wa kienyeji.
Hawa ndio vinara katika mchezo huu.
Idd Ninga
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom