May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Ni dhahiri ya kuwa kwa sasa Dunia inashuhudia vilio kila kona juu ya kero na balaa linalosababishwa na taka za plastiki.
Na kama ilivyo kwingine Nchi yetu nayo haijanusurika na janga hili, kila Mtu mzima anashuhudia hatua mbaya tuliyofikia ikisababishwa na taka hizi za plastiki.
Ni vyema sasa kwa wale Wote wenye Viwanda vya Vifungashio vya plastiki na Waagizaji wa Vifungashio vya plastiki wakaungana na kusimamia ili walau kila Mtaa kuwepo na kiwanda kidogo ambapo watakusanya taka kwenye eneo husika na kuzichakata ili kupata vipande vidogovodogo.
Nimeshakutana na Wadau kadhaa wanaokusanya taka hizi lakini ni ukweli usio na shaka kuwa hawana uwezo wa kukusanya taka zote...na mara nyingine hata huchagua aina ya plastiki.
Kazi kubwa ya Viwanda hivi ni kukusanya taka za aina zote za plastiki na nailoni ili kuzichakata kabla ya kuzipeleka kwenye kituo kimoja Wilayani ambapo watakuwa wanafanya uzalishaji mkubwa wa malighafi za ujenzi.
Unaweza kuzalisha Tofali, Vigae (paving) n.k. kutoka aina karibia zote za taka zitokanazo na plastiki.
Serikali ikaribishe Wadau wenye mawazo hayo na wawezeshwe kwa kupata mashine na maeneo ya kufanyia shughuli hizi...ingawa inatarajiwa kuwa shughuli inayoweza kuingiza kipato lakini hata kama haitokuwa hivyo bado faida ya kuwa na hivi viwanda ni kubwa zaidi kwa uhai wa Nchi na mazingira yake.
Je wajua hata mashine ndogo tu ya kusagia nyama yaweza kutumika kuchakata plastiki na nailoni?.

mazingira yake.