Pre GE2025 Njia pekee ya wapinzani kuingia Ikulu ni kupata idadi kubwa ya wabunge kisha kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwanza CCM haitaruhusu upinzani upate idadi kubwa ya wabunge kuliko wao. Pili hata ingetokea na wakapiga kura ya kutokuwa na imani bado rais angelivunja bunge hilo. Katiba yetu ni mbovu mno ibadikishwe, tupate tume huru ya uchaguzi. Kwasasa njia pekee ni wananchi kuingia mtaani na kuikataa CCM kwa mawe na mapanga.
 
Uko sahihi ila huo mchakato ni wa miaka mingi sana na itategemea na udhaifu wa CCM. CHADEMA walishajichanganya mwaka 2015.
 
kabla hamjapiga kura ya kutokuwa na imani na rais anawahi yeye analivunja bunge mankuwa mmechelewa mnaingia kwenye uchaguzi na mnashindwa vibaya
 
Kwa nini vyombo vya Dola kwa sasa havisimamii Haki?
Katiba inasimamiwa na mwenyekiti wa ccm, yeye ndio muajiri mkuu wa watumishi wote wa serekali, usipofuta maagizo yake yawe ya kisheria ama la kazi huna.
 
..CCM wanalijua hilo.

..Na kinga yake ni kuengua wagombea ubunge wa upinzani kabla mchezo haujaanza.

..kinga nyingine ni kutokutangaza wapinzani ktk majimbo kadhaa wanayoshinda.
Hapo ndipo mass mobilization itumike. Wananchi walazimishe walio enguliwa warudishwe na kama watashinda watangazwe.

Wakikataa kuwatangaza ndio watangaze migomo, maandamano n.k. na waseme bayana kuwa hawatatoa ushirikiano kwa wale waliotangazwa.

Hii inaweza kufanikiwa kwa sababu vyama vingi makini vitakuwa vimeumia na hivyo kuungana kuweka presha kwa wenye mamlaka.

Amandla...
 
CCM haiwezi kutoka kwa maneno hata siku moja, Watanzania waamke waipiganie haki yao ya kufaidi keki ya Taifa lao.
 
Hao wabunge watapatikana vipi kwenye hii tume ya uchaguzi ya kishenz?
 
Pointi ya pili kweli inawezekana.nimepata habari kuwa maafisa wa ngazi za juu jeshini wamevutiwa sana na uongozi wa yule jamaa wa Kwa akina Aziz Kii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…