TECNO Tanzania
Senior Member
- Jul 6, 2016
- 192
- 217
Je, unafahamu kuwa kupitia simu yako unaweza kupata msaada wa kufahamu ghalama mbalimbali za malekebisho ya simu bila hata kufika katika kituo chetu cha matengenezo CARLCARE SERVICE CENTER. Unachotakiwa ni kudownload APP ya Carlcare then katika menu ya APP pale utaona vitu mbalimbali kama ifuatavyo: -
Menu ya carlcare app baada ya kufungua
Kwenye kipengele cha “LOCATION” hapo ndio utaweza kuona kila kituo cha Carlcare kila mkoa, mahali kilipo na bila kusahau namba za simu. Unachotakiwa kufanya ni "ingia kwenye sehemu ya LOCATION kisha sachi mkoa uliopo , baada ya hapo vitakuja vituo mbalimbali kwa mkoa huo na mahali kituo kilipo.
Maelezo ya kituo cha carlcare
Kwenye kipengele cha “PRICE” hapo ndio utakutana na vipengele mbalimbali cha kwanza kabisa ni kuchagua model ya simu yako, baada ya hapo yanakuja maelezo yakionesha kila sehemu inaotakiwa kufanyiwa maelekebisho na ghalama ya kulekebishia. Hivyo inakuwa rahisi kwako kujua ghalama za matengenezo bila hata kufika kwenye kituo cha kutolea huduma.
Mfano wa ghalama za malekebisho
Kufahamu Zaidi juu ya carlcare na utoaji huduma tembelea: Infinix, TECNO, itel official customer support-Carlcare Tanzania