CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,139
Leo Tena kwenye story of change naleta njia rahisi Kabisa kwa mazingira yetu ya kitanzania Kuboresha mazingira mazuri ya kujifunza na kufundisha kwa walimu na wanafunzi Tanzania. Kwa asilimia kubwa humu kama sio wote tumepitia katika elimu ya Msingi na sekondari hapa Tanzania, na bahati nzuri humu Kuna wazazi, walimu, wanafunzi na viongozi mbali mbali na bila shaka tutakubaliana katika badhi ya hoja nyingi kama sio zote na hatimaye kwenye mjadala hapo chini tutashirikiana maoni yetu! Kwa kawaida hapa nchini kwetu ili elimu ikamilike Kuna wadau wanne muhimu ambao ni wazazi, Serikali, walimu na wanafunzi! Ingawa mara kadhaa walimu wanachukuliwa kama sehemu ya serikali! Ingawa haitakiwi kuwa hivyo Kwasababu walimu ndio wanasimama katikati ya hao wote!
Kumekuwa na malalamiko kwa walimu kutokuwa na mishahara ya kutosha pamoja na mazingira magumu ya kazi! Na serikali inajikuta inatumia Nguvu nyingi kujibu hoja hizi
Leo naweka hapa njia rahisi Kabisa ya Kuboresha mazingira mazuri ya kujifunza na kufundisha kwa walimu na wanafunzi!
1. CHAKULA SHULENI
Suala hili Sio sera ya Taifa Bali ni kutegemea na mikoa kwa mikoa na mbaya zaidi ni Kila mkuu wa mkoa husika huona namna kwa busara zake kama chakula kiwepo shuleni au la! Na mara nyingi ni wazazi huwa wanatakiwa kuchangia watoto wao! Sitaki kuongelea umuhimu wa chakula shuleni namna unavyoinua ufaulu, kuleta motisha kwa walimu na wanafunzi, kupunguza utoro n.k kwa haraka jaribu kufikiri nini kinatokea unapokaa asubuhi Hadi saa 9 bila kula chochote!
Sasa fikiri mwanafunzi ambaye hajala kitu uanze kumkaririsha formula mbali mbali! Lakini vipi Kwa yule mwalimu ambaye anaishi mbali na nyumbani kwake na huduma ya chakula haipo shuleni? Unadhani atakuwa anawaza Nini inapofikia majira ya saa 8 -9 mchana? Lakini ikumbukwe mwalimu Hana posho ya chakula! Na badala yake Kila kitu kimewekwa katika huo mshahara! Sasa namna ya Kuboresha maslahi ya mwalimu ni kumuwekea utaratibu wa chakula! Ni rahisi tu kila halmashauri inaweza kutumia maeneo yake na mapato yake kuhakisha walimu na wanafunzi wanakula shuleni! Tafiti zinaonyesha shule ambazo zinatoa chakula Cha mchana kwa walimu na wanafunzi zimekuwa na matokeo mazuri sana katika mitihani ya Taifa!
2. VITABU VYA FASIHI NA BAADHI YA MADA ZIFUNDISHWE KUTOKANA NA ENEO ALIPO MWANAFUNZI
Hili ni suala lingine zuri! Mwanafunzi huwa anafurahi zaidi na kushiriki jambo analojua na atafanya kwa ufanisi zaidi! Mfano kwenye Somo la jeografia mwanafunzi aliyeko Bukoba anaweza kujifunza zaidi kilimo Cha ndizi na huyu aliyeko Tanga mjini akajifunza uvuvi, huyu wa singida akajifunza kilimo Cha alizeti! Hii itamsaidia mwanafunzi kwanza kufanya kitu ambacho ana uelewa nacho!
Lakini haitakuwa na ugumu sana Kwa mwalimu kumuelezea mwanafunzi jambo Hilo! Kuna sehemu nyingine mwalimu ukimwambia mwanafunzi Kuhusu alizeti ni jambo geni kwake! Hata kujua alizeti inafanana vipi hajui! Lakini unamtolea swali 'jinsi ya kupanda na kuvuna alizeti' hii ni sawa na kumleta samaki nchi kavu!! Lakini mwafunzi huyu huyu ungemuuliza jinsi ya kuandaa samaki!! Angeweza kutoa maelezo mazuri sana!!
Vile vile kwenye VITABU VYA FASIHI , huyu mwanafunzi wa mtwara ,Lindi tanga, n.k anaweza kusoma vitabu vyenye maudhui ya eneo lake mfano ndoa za mitala, ukeketaji, uchawi n.k, mapenzi n.k
Na huyu wa Dar , mwanza, Moshi n.k akajifunza vitabu vyenye mambo ya rushwa, ujambazi, wizi, n.k na aina za vitabu hivyo vipo! So ni namna ya kuchagua aina gani ya kitabu kifundishwe wapi! Wakati mwingine Ugumu wa mambo tunausababisha sisi wenyewe!
3. IDADI WA WALIMU NA WAFUNZI IZINGATIWE
Ni ngumu sana mwalimu kuhudumia wanafunzi wengi peke yake! Hata kama utamuongezea mshahara kiasi Gani lakini hataweza kuhudumia wote kwa ufasaha! Mwalimu anatakiwa kujua Kila aina ya mwanafunzi wake darasani hii inamsaidia kujua aina ya wanafunzi anaohusika nao na namna ya kuwasaidia, Kuboresha mazingira mazuri ni pamoja na kumpa mwalimu muda wa kupumzika na kufanya mambo mengine ya kijamii! Hali ilivyo kwa sasa ni ngumu mwalimu kupata muda wa kupumzika!
Kuna baadhi ya maeneo mwalimu kusahihisha na kumaliza madaftari yote ya darasani kwake ni lazima atumie wiki au wiki mbili!! Hebu fikiria mwalimu afundishe wanafunzi 1000 !! Hata akitoa maswali mawili je atamaliza lini? Lakini tunaweza kumsaidia huyu mwalimu kwa kuongeza Nguvu kazi zaidi!! Lakini pia kwa mwanfuzi ni rahisi kupata huduma kwa haraka!
4. NYUMBA ZA WALIMU NA HOSTELI KWA WANAFUNZI
Tuache utani ni ngumu sana mwanafunzi atoke umbali zaidi ya kilometa 5 Kwa kutembea ama wale ambao wanagombania dala dala na aunganishe dala dala zaidi ya tatu umlinganishe na yule ambaye atatoka bwenini tu kuelekea darasani! Lakini Upande wa pili kwa walimu
Akiwa mbali na shule tayari anaongeza gharama ambazo kwa Namna Moja inampunguzia Ari ya kufanya kwa ufanisi! Hapa sijasema mambo ya nauli na Kodi ya Nyumba! Je vipi kama huyu mwalimu akawa anapatikana kwa haraka na Kwa ukaribu zaidi shuleni!?
Hapa nashauri serikali ijenge nyumba za kutosha Kwa Kila shule na walimu wakae shuleni na iwe nyumba nzuri ambayo mwalimu anaweza kujisikia na yeye ni mtu katika jamii!
MWISHO:
Hizi ni njia rahisi Kabisa kwa nchi yetu kwa kuanzia katika na hakika kama yakifanyika tutaona maendeleo makubwa sana kwenye nchi yetu!
Karibuni kwa mjadala
CK Allan
Mdau wa elimu
NAOMBA KURA YAKO

Upvote
1