Njia tatu rahisi za KUGUSHI MESEJI na MIKEKA zinazotumiwa na kuuza FIXED MATCHES

Njia tatu rahisi za KUGUSHI MESEJI na MIKEKA zinazotumiwa na kuuza FIXED MATCHES

Forgotten

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,518
Reaction score
10,839
Habari wanaJF.
Kwa wale wa FIXED MATCHES nimewaletea njia tatu rahisi zinazoweza kutumiwa kwenye Android kugushi MESSAGE na MIKEKA.

1. FAKE TEXT MESSAGE
Hapa matapeli wengi hutumia hii app kutuma fake messages za ushindi kwenye namba zao za simu ila udhaifu wa njia hii message zake huwa hazionyeshi jina la mtandao message ilipoingia, simu yangu huwa inaonyesha ila sina uhakika kama simu nyingine huwa zinaonyesha pia au la! Mwenye simu ya Android ambayo message ikiingia haionyeshi jina la mtandao atusaidie tujue.

2. HTML/CSS WEBSITE INSPECTOR
Hii app hutumika kwenye website na hapa tapeli huweza kucheza na akili za watu kwa kuedit matokeo ya MKEKA au SALIO LA AKAUNTI na matapeli wengi hutumia SPORTPESA kwa sababu uwezo wa kuedit upo ila kwa 1xBet niliwahi kujaribu lakini ilikataa naweza kusema wapo more secured ila kwenye M-BET ni kugusa tu yani wao hamna kitu ila PM BET nakumbuka pia wao haikubali ukiedit website.

3. CHEATDROID
Hapa tapeli ataweza kuingilia mfumo wa app na kuedit SALIO au hata MKEKA na kugundua kuwa ni fake ni jambo gumu sana so hapa ukiingia kichwakichwa unapigwa mchana kweupee! Pia itabidi simu ya tapeli iwe ROOTED ili aweze kufanikisha hili.

NB: Cha msingi ni kutokumuamini mtu yeyote yule anayeuza fixed matches kwasababu wengi wao huwa wana watu wanawatumia kujitangaza wanakuja kama wateja waliofanikiwa kupitia wao wanakuunganisha na tapeli unaliwa.

Kwa wale wenye knowledge zaidi kuhusu iPhone watoe mawazo yao mimi natumia Android ndo maana nimeleta hizi tu kwa PC najua njia moja tu ambayo ni kuedit WEBSITE. Nimeleta za Android tu kwasababu najua WATANZANIA na WAAFRIKA wengi tunatumia simu za mfumo wa Android kutokana na hali zetu za kiuchumi.
 
Mfano!
20181020_065851.jpg
 
UNAJITEKENYA MWENYEWE UNAJICHEKESHA MWENYEWE
 
Back
Top Bottom