Njia ya haja kubwa inawasha sana

Njia ya haja kubwa inawasha sana

Status
Not open for further replies.

Msolid1990

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
144
Reaction score
50
Jamani ndugu zangu njia yangu ya haja kubwa inawasha sana kwa nnje ni kama miaka minne hivi ukiwa unawasha sana. Najikuna huko hadi najichubuka, nimetumia sana dawa ya minyoo nilivyoshauriwa na daktari lakini bado cjapata nafuu. Mnisaidieni!!
 
mmmh !!

magonjwa mengine bana....

utata mtupu....
 
Yaani umekosa kabisa neno mbadala la kutumia!
Hebu muone daktari mtaalamu upate tiba sahihi maana hapa JF watakushauri tu bila kuiona hali ya eneo husika.
 
Inawezekana hautumii dawa sahihi za minyoo? Ama minyoo inakurudia?
Nakushauri rudi kwa dr. Kuna haja ya kufanya vipimo, na ikihitajika culture kujua dawa gani itakusaidia.
 
Pole sana kiongozi subiri wataalamu waje utapata msaada!
 
MKUUU POLE SANA.. KWA MTAZAMO WANGU SIO MINYOO BALI NI FUNGUS ... fikiria kama ulishawapi pata fungus kwenye Korodani labda.. au kama ulisoma shule mliokuwa mnashare vyombo vyakuogea kama mataulo na ndoo za maji pia... JARIBU DAWA ZA KUONDOA FUNGUS
 
hao ni wadudu kitaalamu wanaitwa "al-kudhuv"
 
Jamani ndugu zangu mku*n*du wangu unawasha sana kwa nnje ni kama miaka minne hivi ukiwa unawasha sana. Najikuna huko hadi najichubuka, nimetumia sana dawa ya minyoo nilivyoshauriwa na daktari lakini bado cjapata nafuu. Mnisaidieni!!

Daaah! Unaishi maeneo gani?
 
Simple, kula mboga za majani kwa wingi wakati ukipunguza kabisa maharage, nyama. Au kwa kifupi tumia chakula chenye fibre kama hizo green, brown bread. Halafu kama unatumia toilet paper acha kabisa labda iwe kwenye sehemu hamna maji; muda wote baada ya haja kubwa tumia maji. Halafu fanya usafi hata kama hujaenda haja kubwa kwa kutumia toilet soap au liquid soap mfano handwash yenye mild dettol.

Baada ya kama miezi mitatu hali ikiwa ile ile ndugu nenda hospitali kafanyiwe 'endoscope' au muone mtaalamu wa magonjwa ya ngozi.
 
Kama ni tatizo la muda mrefu na dawa nyingi umetumia bila ya mafanikio, inaweza ikawa aina fulani ya Kansa ya ngozi ( Mungu apishilie mbali). Jaribu kufanya uchunguzi zaidi na uanze na madaktari wa magonjwa ya ngozi. Mungu atakusaidia.
 
Duuuuh haya magonjwa mbona yanautani sana? Mmmmh sina ushauri za ya kukwambia maumivu yakizidi....!
 
mwone daktari wa ngozi Prof Massawe anapatikana Samora Avenue Kelvin house first floor opp na Sapna. Itakubidi uwahi kuweka appointment maana anaona wagonjwa 10 tu kwa siku.
 
samahani nimecheka,na baadhi ya comment zinachekesha.mpaka umeelezea humu,ina maana hali inakusumbua.jaribu kubadilisha hospitali,maybe itasaidia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom