Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 5,489
- 14,091
Magugu maji yana njia nyingi za kuondoa ikiwa ni kutumia madawa, kupandikiza samaki na viumbe wanaokula magugu maji na kuondoa kwa kukata kwa njia ya mkono na mashine Maalum za kukatia magugu maji (water weeds harvester).
Kwa hatua iliyofikia kwenye ziwa Victoria ni kutumia mashine za water weeds harvester ambazo zinaelea kwenye maji na amphibious water weed harvester ambazo zina uwezo wa kupita majini na nchi kavu kisha kuyakusanya magugu maji nchi kavu ambapo yatapakiliwa kwenye vyombo vingine na kwenda kuhifadhiwa sehemu tofauti.
Uganda (Port Bell na Jinja port) wenzetu walifanikiwa kudhibiti Magugu Maji kwa kutumia water weed harvester ila changamoto kubwa waliyopata ni kununua water weeds harvester zenye uwezo mdogo na muda mwingi zilikuwa na breakdown na gharama ya marekebisho kuwa kubwa.
Kwa dharura inaweza ikatumika njia ya kukodi water weeds harvester kutoka kwa nchi jirani au kuweka backhoe au excavator kwenye meli ndogo kisha kuchota magugu maji na kupata njia ya kuweza kupita vivuko na vyombo vya majini bila usumbufu.