Njia ya Jangwani imefungwa kuanzia saa 11:45 leo asubuhi kutokana na mafuriko

Njia ya Jangwani imefungwa kuanzia saa 11:45 leo asubuhi kutokana na mafuriko

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2017
Posts
505
Reaction score
872
Njia ya Jangwani imefungwa kuanzia saa 11:45 leo asubuhi kutokana na mafuriko kwa mvua inayoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam. Hivyo, tunawashauri wasafiri wetu kutumia usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Morocco kwa wale wanaotokea Posta kwenda Kimara.

Wakifika Morocco wanaweza kuendelea na usafiri wa DART mpaka Kimara na sehemu nyingine za Jiji. Kwa wasafiri wanaoelekea Posta kutoka Kimara, tunawashauri kuchukua mabasi ya DART mpaka Morocco ambapo wanaweza kuchukua usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Posta, Kariakooo.

DART
 
Njia ya Jangwani imefungwa kuanzia saa 11:45 leo asubuhi kutokana na mafuriko kwa mvua inayoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam. Hivyo, wasafiri wanaotumia mwendo kasi (DART) wanashauriwa kutumia usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Morocco kwa wale wanaotokea Posta kwenda Kimara Wakifika Morocco wanaweza kuendelea na usafiri wa DART mpaka Kimara na sehemu nyingine za Jiji. Kwa wasafiri wanaoelekea Posta kutoka Kimara, wanashauriwa kuchukua mabasi ya DART mpaka Morocco ambapo wanaweza kuchukua usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Posta, Kariakooo.

Source:

Poleni sana wakazi wa Dar. Kwamfano hii mvua ikawa ndo imefunguliwa mazima ikapiga back to back kuanzia hizi za vuli zikaja kuungana nazamwaka cjui Dar itakuaje
 
Eneo la jangwani panafahamika kujaa maji miaka lukuki,suluhisho ni kujenga barabara Kama daraja kuanzia fire mpaka Bondeni hotel Lenye kuruhusu maji kupita chini wala sio tuta.

Cha kushangaza awamu ya mwisho ya JK huyu bwana "mitano tena" akiwa waziri wa mabarabara wakati wa ujenzi wa mwendo kasi alirudia makosa yale yale.

Mbaya zaidi akaongeza karakana ya mwendokasi pale pembeni ya mto utadhani ni bwawa la samaki.Halafu utasikia akiwa na microphone anawakoromea wengine "Umesoma wapi Pumbavu kabisa"
 
Badala ya kujenga barabara ya gharama baharini isiyo msaidia mkazi na mpiga kura. Wangetengeneza Jangwani kwanza. Lkn ccm inatakataka kwenye masikio na tongotongo machoni
Ten Percent ndio zimetuponza, yaani masikini akipata nafasi anachofikiria ni kupiga tu!!
 
Hivi watanzania tunajua maana ya uchumi wa Kati? Uchumi wa Kati halafu inamchukua mtu mwenye gari masaa matano kutoka Muhimbili kuja Magomeni mapipa?
Uchumi wa Kati mvua kidogo tu watu wanapoteza Maisha?
Ikitokea leo mkeo ana uchungu wa kujifungua halafu Yuko nyumbani ndio utajua hujui maana ya uchungu wa Kati.
 
Eneo la jangwani panafahamika kujaa maji miaka lukuki,suluhisho ni kujenga barabara Kama daraja kuanzia fire mpaka Bondeni hotel Lenye kuruhusu maji kupita chini wala sio tuta.

Cha kushangaza awamu ya mwisho ya JK huyu bwana "mitano tena" akiwa waziri wa mabarabara wakati wa ujenzi wa mwendo kasi alirudia makosa yale yale.

Mbaya zaidi akaongeza karakana ya mwendokasi pale pembeni ya mto utadhani ni bwawa la samaki.Halafu utasikia akiwa na microphone anawakoromea wengine "Umesoma wapi Pumbavu kabisa"
Tunapenda kutoa maoni bila tafiti. kwa wanaojua jinsi daraja lililojengwa na kajima kuwa lilikuwa refu na kwa chini mitumbwi ilikuwa inapita huwezi toa commen hii. Ni matokeo ya tabia mbaya yetu ya utupaji wa taka katika mito
 
Mkuu Nazungumzia solution ya sasa hivi wewe unaleta historia.Lilikuwa refu na linakidhi mazingira ya wakati huo,sasa hivi linakidhi?
 
Njia ya Jangwani imefungwa kuanzia saa 11:45 leo asubuhi kutokana na mafuriko kwa mvua inayoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam. Hivyo, wasafiri wanaotumia mwendo kasi (DART) wanashauriwa kutumia usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Morocco kwa wale wanaotokea Posta kwenda Kimara Wakifika Morocco wanaweza kuendelea na usafiri wa DART mpaka Kimara na sehemu nyingine za Jiji. Kwa wasafiri wanaoelekea Posta kutoka Kimara, wanashauriwa kuchukua mabasi ya DART mpaka Morocco ambapo wanaweza kuchukua usafiri mbadala ikiwemo daladala mpaka Posta, Kariakooo.

Source:

Tumetekeleza kwa KISHINDO...!!!
 
Mnaolalamika uchumi wa kati mnadhani Tanzania ni dar pekee? Hata mikoani napo Tanzania na hatuna kesi mbovu mbovu za mafuriko. Kubalini bomoa bomoa mpate nafuu ya kero za mafuriko. Ungeni mkono juhudi za kuwatoa wakazi wa mabondeni
 
Back
Top Bottom