Njia ya kibabe kukomesha fitna na majungu

Njia ya kibabe kukomesha fitna na majungu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Katika harakati za kutafuta mkate kumekuwa na fitina nyingi na majungu miongoni mwetu.

Sasa katika biashara zangu nikapata bro ambaye kila ikitika jioni anapiga simu kuwasema wenzake mabaya. Nilimvumilia mara ya kwanza tu,mara ya pili nimemuunga conference call (mkutano) na mtu aliyekuwa anamsema bila kujua. Alivyomaliza tu kubwabwaja, nikamwambia mhusika yupo hapa anakusikia yote sasa tumpe nafasi na yeye ajibu. Upande wa pili ukaomba arudie ili ajibu kimoja baada ya kingine. Bro kusikia sauti ya mtu aliyekuwa anamfitinisha akakata simu. Tukajaribu kumpigia hakupokea baadae akazima simu. Tukampigia mkewe ampe simu,amegoma kupokea.

Ushauri wangu ni kwamba wabongo wengi ni watu wa kupakazia. Kama jungu litakuja kwa njia ya simu, hebu tumia conference call kumaliza mzizi wa fitna
 
Ghafla wana JF wote watageuka na kusema wao hua hawawasemi watu.Ila wao hua wanasemwa tu.
Wana if bana ikija mada ya magari kila mtu anagari ikija mada ya elimu kila mtu msomi wa masters

Sasa imekuja mada ya umbea wote wapo upande wa wasiopenda umbeya

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Usipo pigwa majungu maana yake hauna ushindani na haukubariki,majungu ni moja ya promotion kwa anayekusengenya.
 
Back
Top Bottom