Bila shaka hapa ulimwenguni hamna kitu kinaogofya Zaidi ya kupoteza uhai kwa viumbe hai ( WANYAMA NA BINADAMU). Hali hii hutokana na mfumo wa fahamu unaofanya kazi automatic kulinda na kudhibiti uhai usiponyoke mwilini. Kinachopelekea hudhuni kubwa kumwangukia binadamu kutokana na matokeo ya kifo yatokeapo kwake ukilinganisha na viumbe hai vingine ( Kuku, mijusi na nk ){wanyama wenye kiasi kikubwa cha ubongo wanaweza onyesha hudhuni kuondokapo kwa wenzao mf. Sokwe, Tembo nk} ni kutokana kuwa na ubongo yenye uwezo mkubwa hadi kupelekea kujitambua uwepo nafsi yake hapa duniani na uwepo wa nafsi nyingine zenye uelewa kama yenyewe.
Basi kutokana na kifo kutunyanyasa kwa mda mrefu vizazi na vizazi hadi kupelekea watu wetu wa kalamu kutunga story na kanuni za kufwata ili kutufariji ( maisha mazuri baada ya kifo) {kwa ukweli hamna anayejua} hivyo basi wana member humu ndani jibu la shida hii ni binadamu wote dunia nzima kuacha KUZALIANA hii ndo njia pekee ya kukinyima kifo wahanga wake wapya.
Huu ulimwengu tunaoishi ni ulimwengu wa mwili ( Mwili ni mateso) na kitendo cha kuzaliwa hapa duniani ni kitendo cha nafsi kunyakuliwa kutoka kwa kwenye ulimwengu wa kiroho ( huko kwenye ulimwengu wa kiroho kifo hakipo bali kuna milele na milele) ndo maana kitoto kichanga chalia baada ya kuzaliwa kwani roho inakuwa imeumia kutoka kwenye ulimwengu wa kiroho. Na kinachopelekea kitendo cha kujamiana kuwa hakifanywi hadharani kama wanyama wengine na endapo wakikutwa wanashikwa na fedhea ni kutokana na nafsi kuwa guilt kujua kuwa kufanya hivyo kutapelekea nafsi nyingine ishushwe kama matokeo.
Tuachane na dhana za kukariri ( kuja duniani kuijaza dunia) {kuongezeka kwa watu kwa pelekea maovu kuongezeka hii kutokana na kugombania mahitaji muhimu} basi kwa kuwa sisi WATANZANIA tunaonekana tunashindwa kila kitu tufanye jambo hili ili tuwe taifa la kwanza kushinda mauti (kuacha kabisa kuzaliana) baada ya hii post. Nawahakikishia wasomaji itakapofika mwaka 2128 hamna MTANZANIA yeyote ambaye anaishi kwa saa ivi hapa nchini atafariki hapa duniani. Tuwaachie wapenda vya ulimwengu sisi tufwate vya kiroho na tutaimba milele na milele.