Njia ya mafanikio kimaisha ni ipi?

Njia ya mafanikio kimaisha ni ipi?

f2rk

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2013
Posts
501
Reaction score
425
Habarini ndugu zangu! Mimi ni mwajiliwa kampuni x,kipato changu kwa mwezi ni 1.5m,nina mke na mtoto!
Katika maisha kuna plan tofauti
A-Nyumba,gari,vitegauchumi;
B-Vitega uchumi,nyumba,gari(au gari,nyumba)

Niliamua kufuata plan B,nikawekeza kwenye kilimo na ufugaji ili kuzalisha milioni 30 za kuwekeza kwenye miradi mikubwa zaidi ambayo haihusiani na kilimo,baada ya kuanza kupata faida ndo ningejenga na kununua usafiri;Bahati mbaya hali ya hewa imekuwa mbaya nimepata hasara kubwa isipokuwa kwenye ufugaji na hivyo mradi mkubwa hautowezekana kuanza mwaka huu mpaka nijipange upya.

Kuna vipesa kidogo ntavipata april hii,nafikiria bado whether ninunue kiwanja na kuanza kujenga au nivitupie tena kwenye kilimo? Ufugaji mdogo unaendelea na lengo ni kutoa kuku mia wa nyama kila wiki,na wamayai wanakaribia kuanza kutaga! Msaada wenu kwa wenye uzoefu zaidi na ujasiriamali na maisha
 
Yap! Binafsi naungana na wewe kwa kufuata plan B. Kiuchumi, unapojenga nyumba ya kuishi umeweka investment isiyo na return, na wal afedha hiyo haizunguki, jambo hili kwa kawaida na mazoea tuliyonayo si rahisi kueleweka kwa wengi. watu watakwambia nyumba kwanza, upate uhakika wa kuishi. hii ni kutokana na uelewa wetu finyu katika mambo ya investment na pia attitude tuliyonayo katika mambo ya uwekezaji na biashara kwa ujumla. tumekuwa waoga wa ku-take risk na ndo maana tunakimbilia nyumba za kuishi.

Na hata wakati fulani, mtu akianzisha biashara fulani akipata faida anaipeleka katika ujenzi badal aya kukuza biashara aliyonayo. mathalani ana kuku wa mayai 200, akipata faida hawazi kuwa kuongeza kuku hata kufikia elfu 2 na pengine zaidi, anabaki na idadi hiyo na anakimbilia kujenga. yote ni woga wa risk, anawaza kesho inaweza kutokea lolote, hana uhakika na uimara wa biashara yake.

Wakati fulani, miaka kama 7 hivi imepita nilitembelea Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), nikaambiwa, kwa mgodi wa Bulyanhulu - kahama, tumewaruhusu kununua nyama ya kuku toka afrika kusini kwa sababu mahitaji yao kwa wiki, hakuna mfugaji mtanzania mwenye uwezo aliyejitokeza kuyafikia. hii ni kwa sababu tuna biashara za kujikimu, na pia ndo maana watanzania wengi ni waoga kuchukua mikopo kwa kuweka dhamana nyumba ya kuishi. mtu ana tamani apate nyumba ya pili kwanza ndipo achukue mkopo akiamini hata akishindwa, basi amebaki na pahala pengine. mtu huyu kichwani mwake kashaweka wazo la kushindwa, unategemea nini?

Jiulize kwanini wahindi wengi ni hodari wa kupanga kuliko kujenga.

Ushauri wangu, kama una uhakika na soko la biashara yako ya kuku wa nyama na mayai, hiyo faida uliyopata kuza biashara yako, waza sasa kutoa kuku wa nyama elfu moja na kuendelea kwa wiki badala ya mia. kuku wako wa mayai wakianza na ukaona soko la mayai lipo, waza kuwa mzalishaji mkubwa wa mayai pengine katika kata nzima unayoishi. unaweza kujenga kama ujenzi huo niwa kuendeleza biashara yako ya ufugaji, pengine umekodi mabanda na una sehemu finyu itakayozuia upanuzi wa biashara yako. Gari unaweza kununua ile u nayodhani itaendeleza biashara. suzuki Carry na nyinginezo zinazoweza ku-serve matumizi binafsi na biashara yako inaweza kuwa sahihi.
 
Big up, thumbs up una mawazo kama yangu, kujenga ni kufukia pesa
 
Wafundishe na marafiki zako maana ni wachache wanaoweza kuiputa njia ya kwanza ambayo kimsingi huwa inaleta marafiki wengi wa kupaka rangi ambao katika hali ngumu hupotea kama upepo wa kisulisuli
 
Thanks Honda xl kwa ufafanuzi makini,mabanda ya kuku nimejenga mwenyewe vyumba vitatu vya futi 12 kwa 12,next week naongeza vyumba viwili ili kufanikisha lengo la kuchukuwa vifaranga wa nyama 200 kila baada ya wiki mbili na wa mayai kila baada ya miezi mitatu mpaka wafike layers 600. However mradi huu ni kwa ajili ya kuendesha familia tu!
 
Back
Top Bottom