Wana JF nimejaribu kuwaza hivi kwanini nchi yetu haitumii sana njia ya PPP- Public Private Partnership katika kuanzisha miradi ya maendeleo nchini?
Njia hii naona inakuwa na unafuu sana maana sio mkopo bali ni ubia kati ya serikali na mwekezaji wa mradi.
Mwekezaji analeta pesa yote ya mradi na anajenga kwa kutumia wakandarasi wake.
Akimaliza mradi ukaanza kufanya kazi hapo wanaanza kugawana mapato labda kwa asilimia 60% mwekezaji na Serikali asilimia 40% kufuatana na makubaliano yao mpaka pesa za mwekezaji zinarudi zote hata iwe miaka 20, 30 n.k
Uzuri wa njia hii mradi unalipa kodi za serikali kama kawaida. TRA inakusanya kodi since day one- yani siku ya kwanza .
Nafikiri njia hii nayo tuikazanie itatusaidia