Njia ya TAZARA imeanza kuhujumiwa rasmi?

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
2,427
Reaction score
4,944
wakuu sana.

hizi taarifa za treni zinazotumia njia ya TAZARA kuacha njia zimekuwa nyingi mno. nadhani kila mwezi kuna taarifa moja au mbili za treni kuacha njia ama upande wa Tanzania au ule wa Zambia.

taarifa za hivi punde zinasema kuna treni imeacha njia Mlimba.

juzijuzi tu hapa zilitoka taarifa upande wa Zambia kuwa kuna treni imeacha njia eneo fulani hivi jina silikumbuki.

je, matukio haya ni ya kawaida tu au kuna hujuma inafanywa na wamiliki wa malori maana wana maslahi na mizigo inayotoka Zambia na Kongo kuja na kutoka Dar es Salaam?

je, serikali hii ni legelege? maana kipindi cha magufuli huu upuuzi haukuwepo.
 
Alikuwa inadaiwa analinda reli yupo kortini anapambana na shauri lake

Unategemea nani alinde sasa??
 
Kama hiyo reli ni chakavu na Wafanyakazi wapo hoi bin taabani mishahara wanapata tarehe 40 unategemea kitatokea nini? Na hali imefanya mpaka Tazara kuanza kuuza na kukodisha fixed assets zake, hata Wastaafu wake hawalipwi mafao.
 
Kama hiyo reli ni chakavu na Wafanyakazi wapo hoi bin taabani mishahara wanapata tarehe 40 unategemea kitatokea nini? Na hali imefanya mpaka Tazara kuanza kuuza na kukodisha fixed assets zake, hata Wastaafu wake hawalipwi mafao.
Hapo sikubaliani nawewe kwa kiasi fulani.

Unahujumu reli idondoke alafu ilidondoka unafaidika na nini?. Mosi unasababisha hata kazi isifanyike ili mapato hayo mnayoliowa trh 40 yawepo, pili unasababisha maumivu kwa wenzako ambao kwa upande mwingine wanatakiwa kupata riziki kutokea train ikiwa njiani.

So ni ujinga unaopitiliza kufanya hujuma kama ni staff wa Tazara.
 
Una uhakika kuwa imehujumiwa,na kama ni kweli leta ushahidi hapa kuthibitisha madai yako. Nadhani wewe hufahamu status ya reli ya Tazara ilivyo takribani miaka ishirini sasa.
 

Ukiambiwa leta ushahidi usiotia shaka, ili wahujumu wachukuliwe hatua unao?
 
".....juzijuzi tu hapa zilitoka taarifa upande wa Zambia kuwa kuna treni imeacha njia eneo fulani hivi jina silikumbuki..."

".....je, serikali hii ni legelege? maana kipindi cha magufuli huu upuuzi haukuwepo..."



Unapomuongelea Magufuli huku ukilitaja na eneo la Zambia ambalo halikuwa linatawaliwa nae kutokea ajali kama hiyo hauoni kama lawama zako zinalenga kutokupata suluhisho la tatizo? Unamuandama mama bila kujua historia ya reli yenyewe.
 
Mods futeni majungu na mpigeni ban mleta uzi. Anakaa anakurupuka ghafla anaandika vitu visivyo kuwa na uthibitisho na kutuhumu watu fulani ambao ana chuki nao binafsi. Hata hajui lolote kuhusu mfumo wa reli na changamoto zake. Acha kiherehere
 
Labda Hichilema ataokoa jahazi
 
Ukiambiwa leta ushahidi usiotia shaka, ili wahujumu wachukuliwe hatua unao?
Huo ushahidi usio tia shaka upo tayari/utakubali kuletwa au ushahidi utaamua kukataaa?

Na je hao wenye ushahidi wako tayari ushahidi wao ujulikane?
 
Utetezi wako haushawishi kabisaa.

Unajua maana ya hujuma lakini unaweka cover
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…