Njia ya TAZARA imeanza kuhujumiwa rasmi?

Njia ya TAZARA imeanza kuhujumiwa rasmi?

Waafrika sijui tumelogwa na nani,badala ya kuimarisha kile tulichonacho kwa sasa kabla ya kununua au kujenga kitu kipya eti tunajenga nyumba mpya huku ile tunayoishi ikiwa hoi bin taabani. Ndio haya ya Tazara sasa vs SGR.
Lisu akiwa rais ataweka sawa mambo
 
Huo ushahidi usio tia shaka upo tayari/utakubali kuletwa au ushahidi utaamua kukataaa?

Na je hao wenye ushahidi wako tayari ushahidi wao ujulikane?

Kama ni siri na zibaki sirini kesi iendeshwe kwenye mahakama isiyo ya wazi na kama inakidhi vigezo. Ukileta kwa walimwengu tii sheria bila kushurutishwa.
 
wakuu sana.

hizi taarifa za treni zinazotumia njia ya TAZARA kuacha njia zimekuwa nyingi mno. nadhani kila mwezi kuna taarifa moja au mbili za treni kuacha njia ama upande wa Tanzania au ule wa Zambia.

taarifa za hivi punde zinasema kuna treni imeacha njia Mlimba.

juzijuzi tu hapa zilitoka taarifa upande wa Zambia kuwa kuna treni imeacha njia eneo fulani hivi jina silikumbuki.

je, matukio haya ni ya kawaida tu au kuna hujuma inafanywa na wamiliki wa malori maana wana maslahi na mizigo inayotoka Zambia na Kongo kuja na kutoka Dar es Salaam?

je, serikali hii ni legelege? maana kipindi cha magufuli huu upuuzi haukuwepo.View attachment 1953481
Nani anahujumu? Magufuli ndio alikuwa anaongoza shirika? Hiyo reli sehemu kubwa management ni ya Zambia,waulize wahusika.
 
Una uhakika kuwa imehujumiwa,na kama ni kweli leta ushahidi hapa kuthibitisha madai yako. Nadhani wewe hufahamu status ya reli ya Tazara ilivyo takribani miaka ishirini sasa.
Hivi akili zinakuwa wapi mkuu?.

Aliyeandika kuhusu hujuma ni wewe, mimi nimereply kulingana na ulichiandika how comes?.

Hebu rejea first comment from you.
 
Unaona hali ya Tazara ilivyo mbaya mpaka imefikia hatua ya kukodisha assets zake kwa Lake Oil kinyume na sheria?View attachment 1953508View attachment 1953510View attachment 1953511
Mbaya zaidi sheria ya ujenzi kando ya reli ni mita 30 lakini hawa Waarabu maswahiba zake Riziwani Kikwete wamejenga mita 3 tu kutoka kwenye reli.

Kama kuna kitu nitauchukia utawala huu wa Chifu Hangaya ni uhuni huu unaofanyika hapa kwenye mali ya umma na kuhujumu Public interest kama viwanja vya michezo na ibada kugeuzwa bandali kavu.

Ni kweli Magufuli alikuwa katili lakini asingekubali upumbavu huu unaofanyika Tazara sasa hivi.

Cha ajabu mkurugenzi mkuu wa Takukuru issue hii ipo mezani kwake lakini hakuna hatuwa zozote zinazochukuliwa.

Mama akiendelea kukumbatia kundi la Msoga anapotea na atachukiwa sana na ataipa ccm wakati mgumu sana uchaguzi ujao wananchi wakipewa haki ya kuchaguwa.
 
Duu inauma saana ,,Hii reli nimeifahamu Toka mwaka 1982 ilikuwa nzuri na ya kupendeza..ilifanyiwa ukarabati Vizuri saaana...Sasa Hivi limekuwa gofu tuu.kuna laana kwenye nchi hii.Amini hicho.
 
Kama hiyo reli ni chakavu na Wafanyakazi wapo hoi bin taabani mishahara wanapata tarehe 40 unategemea kitatokea nini? Na hali imefanya mpaka Tazara kuanza kuuza na kukodisha fixed assets zake, hata Wastaafu wake hawalipwi mafao.
Bora ife tu
 
wakuu sana.

hizi taarifa za treni zinazotumia njia ya TAZARA kuacha njia zimekuwa nyingi mno. nadhani kila mwezi kuna taarifa moja au mbili za treni kuacha njia ama upande wa Tanzania au ule wa Zambia.

taarifa za hivi punde zinasema kuna treni imeacha njia Mlimba.

juzijuzi tu hapa zilitoka taarifa upande wa Zambia kuwa kuna treni imeacha njia eneo fulani hivi jina silikumbuki.

je, matukio haya ni ya kawaida tu au kuna hujuma inafanywa na wamiliki wa malori maana wana maslahi na mizigo inayotoka Zambia na Kongo kuja na kutoka Dar es Salaam?

je, serikali hii ni legelege? maana kipindi cha magufuli huu upuuzi haukuwepo.View attachment 1953481
Mwacheni huyo marehemu wenu apumzike yeye sio Mungu na kwa kuwa ameshakufa hawezi kurudi tena.
 
Inaweza kuwa kweli au sio kweli lakini watu wakitaka wakuyumbishe watakuambia Leta ushahidi,ukileta ushahidi faili linapotezwa ikiwezekana hata shahidi anapotezwa "hiyo ndio Africa"
 
Back
Top Bottom