Njia ya uzazi Iko centimeter 4 tangu saa Tano usiku haijaongezeka

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Habari wakuu mke wangu baada ya kupatwa na dalili za uchungu tumemfikisha hospital saa nne usiku, baada ya kufika akapimwa njia ikiwa centimeter 3 uchungu ukiwa unamuijia na kupotea baada masaa manne kupimwa njia ikawa centimeter 4.

Sasa Hadi saa hii Bado uchungu unakuja na kupotea dokta nae anasema nikusubiria Hadi njia iwe centimeter 8 walau ndo anaweza pewa drip ya uchungu...wakuu nauliza ni suluhu kama mtu njia haiongezeki na uchungu unakuja na kupotea!
 
Ushauri wa daktari unaheshimika, ila inapaswa kuwa imefanyika kipimo cha kujua hali ya mtoto tumboni na mapigo ya moyo yanaendaje (kama bado hakijafanyika), pia hali ya mama maana uchungu una maximum time ambayo ikizidi mama anaweza kuchoka na baadae njia ikifunguka akashindwa kusukuma mtoto.

Haya yote yanategemea na jinsi wataalamu wanavyo monitor hali yake...si rahisi kutoa majibu ya direct kwa sisi ambao hatumuoni na hatuna takwimu za vipimo.

Ila tu KUA MAKINI ikionekana masaa yanazidi standard ni vyema kufikiria juu ya upasuaji ili kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.
 
Kipimo Cha kujua Hali ya mtoto tumboni kikoje iko
 
Maximum time ya uchungu ni mda gani
 
Mfanyieni uzazi wa upasuaji haraka sana kabla hamjampoteza mtoto au wote
 
Kwa nini usitulie na kuwaachia wataalamu wafanye kazi yao?Tangu jana umetoa macho kuiangalia njia inavyofunguka?Tulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…