Njia ya zipi sahihi kutuma mzigo Marekani

Njia ya zipi sahihi kutuma mzigo Marekani

shafii77

Member
Joined
Mar 18, 2019
Posts
60
Reaction score
85
Hello ndugu, ninahitaji kutuma mzigo marekani ni kilo 5 TU za karafuu je ni kampuni gani ya ndege au yoyote ya usafirishaji naweza kuitumia kutuma mzigo wangu kwa haraka na unafuu? Wenye uzoefu naombeni msaada wenu na pia naomba kujua gharama exactly za kutuma huo mzigo.
 
Ok kati ya FedEx na DHL wapi kuna unafuu wa nauli?
 
Ulishawahi kutuma hiyo kitu usije lipa ghalama alafu zikafika kule zikawa seized coz Wana Sheria Kali zisije kuwa zimebeba vimelea wa magonjwa ya mimea so jihakikishie ilo kwanza
 
Hello ndugu, ninahitaji kutuma mzigo marekani ni kilo 5 TU za karafuu je ni kampuni gani ya ndege au yoyote ya usafirishaji naweza kuitumia kutuma mzigo wangu kwa haraka na unafuu? Wenye uzoefu naombeni msaada wenu na pia naomba kujua gharama exactly za kutuma huo mzigo
Tumia njia mojawapo kati ya zifuatazo
1. DHL
2. FedEx
3. EMS.
Njia zote ni salama na zote zina Door to door deliver kwa Marekani kwa mimi ninaependa Budget ningetumia EMS sababu bei ya kusafirisha mzigo ndogo ukilinganisha na DHL.

Jambo la Pili kuzingatia ni vibali kama export permit, phytosanitary certificate, certificates of origin n.k
Vibali ni muhimu sana sababu hauwezi kusafirisha hizo karafuu bila hivyo vibali.
Jambo la vibali nimezungumzia hivyo sababu nime assume kwamba karafuu zako haziko processed, ila kama karafuu zipo processed utatakiwa kuwa na vibali toka mamlaka ya dawa na chakula.
 
Back
Top Bottom