Baba Mtu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2008
- 870
- 170
Habari wanaJF,
Nimeleta kwenu bandiko lako ili tuweze kujadili njia mbalimbali za asili za kupanga uzazi.
Tujadili...
2. Uzazi wa Mpango: Jinsi ya kutumia Majivu kuzuia mimba
3. Matumizi ya mbegu za Mnyonyo kupanga uzazi
4. Mwanaume kumwaga nje ya uke ( Pull Out Method )
Nimeleta kwenu bandiko lako ili tuweze kujadili njia mbalimbali za asili za kupanga uzazi.
Tujadili...
KUTUMIA KALENDA KWA KUZUIA MIMBA
Njia hii haina uhakika sana wa kuzuia mimba, lakini ni nzuri kwa sababu haigharimu chochote.Njia hii huwafaa zaidi wanawake amabo taratibu za siku zao za kwenda mwezini ni kawaida mara moja kila baada ya siku 28, na ili iweze kuzaa matunda, njii hii huhitaji mtumiaji awe tayari kukaa bila kukutana kimwili kwa muda wa wiki moja kila mwezi!
Kwa kawaida kuna siku 8 tu kila mwezi ambazo mwanamke anaweza kupata mimba ambapo siku hizi zipo katikati ya siku zake za kwenda mwezini, na huanza siku 10 baada ya siku ya kwanza ya kupata damu ya hedhi. Hivyo basi ikiwa mwanamke yoyote hataki kupata mimba ni lazima aache kukutana na mwanaume kwenye siku hizi 8! Naamini hili linawezekana kwani siku nyingine zilizobakia wapendanao wanaweza kujiachia kama kawaida kwani hakuna uwezekano wa mwanamke kushika mimba!
Ili kuepukana na kutatanikiwa, ni lazima mwanamke aonyeshe kwenye kalenda zile siku ambzo hatakiwi kukutana na mwanaume. Hapa inaweza kuwa ngumu kuchora kalenda ya ukutani kwa kuwa inatumiwa na wengi lakini ni rahisi kutekeleza hili kwa kutafuta pocket kalenda [kijikalenda ambacho waweza kiweka kwenye pochi yako]
Kwa mfano: Unaingia kwenye siku zako tarehe 5 Desemba, weka alama kwenye tarehe hiyo kisha hesabu siku 10 na baada ya hapo pigia msitari siku 8 zinazofuata!
Angalia mfano huu:-
Kumbuka siku hizo nane utakazozipigia msitari ni hatari kwani ukikutana na kidume tu na kushiriki ngono bila kutumia kondom utashika mimba, hivyo ni vema usikutane na mwanaume hata kidogo, yani epuka hata akikubembeleza na lugha laini kuwa nitapizia nje sweetie, sijui nini na nini kama hataki tumia kondom kataa kwani kupizia nje ni bahati nasibu hasa pale mwanamke anapoamua kumpa mwanaume maujuzi ya kabatini ambayo ni adimu, yaani mwanaume hupewa kwa sababu maalum tu hali inayomfanya apagawe kwa huba na hivyo huweza msababisha ashindwe kupiziza nje!
Nimalize kwa kusema kuwa, mwanamke anapaswa kuendelea na utaratibu huu kila mwezi lakini akumbuke kuwa, njii haina uhakika sana mbaka itumiwe sambamba na njia nyingine kwama vile kondom.cc.@Nabihu
2. Uzazi wa Mpango: Jinsi ya kutumia Majivu kuzuia mimba
Habari wakuu wote jamvini....
Nimepata kusikia kuwa binti akinywa juice ya majivu ndani ya saa 2 toka mbegu za kiume ziingie ktk papuchi ake basi anakuwa salama kbs kuepuka mimba bila kujali siku ya salama au hatari.
Mchanganyo uko hivi,
1. Weka majivu nusu glass
2. Jaza sehemu ya glass iliyobaki kwa maji safi
3. Koraga na ili upate mchanganyiko mzuri
4. Acha maji yajitenge na majivu
5. Kunywa maji ya juu
Zingatia: waweza andaa juice hiyo kabla ya kuanza tendo kwa usalama. Juice haina madhara. Japo yaweza sababisha tumbo kuuma kwa muda mfupi.
Juice ina ukakasi/uchachu.
Wewe wajua kinga ipi ya asili?
Tupeane mawazo wadau wangu. Wote mnakaribishwa
==============
Majivu yatumika kupanga uzazi na utoaji mimba Mbeya
LICHA ya Serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoa elimu ya kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kote nchini, baadhi ya wanawake katika wilaya ya Mbeya Vijijini na Jiji la Mbeya wamekuwa wakitumia majivu kama njia ya kupanga uzazi na kutoa mimba zisizotarajiwa.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala hii katika mji wa Mbalizi Mbeya Vijijini na kata ya Manga na Foresti Jijini Mbeya umebaini kuwa wanaoongoza kwa kutumia njia hiyo ni pamoja na wake za watu na wahudumu wa Bar.
Wanawake waliohojiwa wakiwemo wawili kati yao ambao wakawa na mahusiano na mwandishi wa makala haya ili kukamilisha uchunguzi, walisema kuwa majivu hayo wanakunywa kikombe kimoja kila baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa na wanaume ambao wana mahusiano nao ya kimapenzi na wengine waume zao.
''Majivu unatakiwa unywe ndani ya masaa 12 baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa ili mimba isitunge'' anasema Mama Angel mkazi wa eneo la Mama John ambaye ni mke wa mtu.
Mama Angel anakiri kuwa amewahi kutoa mimba kwa njia za kisasa ambayo haikuwa mimba ya mumewe na alipoambiwa kuwa kuna njia zingine za kujikinga ikiwemo kunywa majivu baada ya tendo la ndoa ameendelea kutumia njia hiyo kwa miaka mitatu sasa.
''Kule hospitali nilitundikiwa maji ya uchungu ambayo yanaongeza njia na ndani ya masaa matatu mimba ikatoka'' anasema Mama Angel bila kutaja hospitali aliyotolea mimba.
Uchunguzi huo uliofanywa mwezi Octoba na Novemba 2012, umebaini kuwa kwa sasa wanawake wengi hawapendi kutumia njia za uzazi wa mpango wa kisasa mfano Sindano, vipandikizi na vidonge kwa madai kuwa huduma hizo zina madhara.
Wanawake 43 waliohojiwa wakiwemo wake za watu 13 walisema kuwa madhara waliyoyapata baada ya kutumia njia za uzazi wa mpango wa kisasa ni pamoja na kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa.
Baadhi walisema kuwa wanaogopa kufanyiwa upasuaji (kusafishwa) kunakotokana na uvimbe unaosadikika kutokea baada ya kutumia kwa muda mrefu huduma hizo za kisasa hasa vidonge maarufu kama majira.
''Tarehe za Hedhi hubadilika na kutoeleweka baada ya kutumia dawa hizo za uzazi wa mpango wa kisasa zikiwemo sindano na vidonge'' anasema Naomi Haule ambaye ni mhudumu wa Bar.
Wengine ambao waliomba hifadhi ya majina yao, wanasema mbali na kutumia majivu kama njia ya uzazi wa mpango kuzuia mimba na utoaji mimba, baadhi yao wanatumia kisamvu, Vidonge vya uzazi wa mpango maarufu kama (Majira) na majani ya mti unaojulikana kwa jina la Songwa kutoa mimba zisizotarajiwa.
''Wake za watu wanaopata mimba ambazo si za waume wao, wafanyabiashara na wahudumu wa Bar siyo siri tunaongoza katika kutumia njia hizi na utoaji mimba kwa njia za kienyeji'' anasema Rehema Mwakitalu akiwa na wenzake eneo la Mwanjelwa ambaye pia ni muhudumu wa Bar.
Walipoulizwa kuwa kwanini wasitumie njia za kisasa katika utoaji mimba walisema kuwa kikwazo ni gharama za utoaji mimba kwa njia za kisasa ambapo mwanamke mwenye mimba ya mwezi mmoja hutozwa Shilingi 40,000 ili asaidiwe kutoa mimba hiyo.
Walizitaja hospitali ambazo zinahusika kutoa mimba hizo kwa siri kuwa ni pamoja na hospitali ya wazazi Meta na zahanati zingine za madaktari binafsi zilizopo eneo la Nzovwe, Mama John na Uyole.
Aidha mbali na hospitali hizo, wanawake hao walisema kuwa pia kuna waganga na wakunga wa jadi wanaowasaidia kutoa mimba hizo ambazo wanadai kuwa hazikutarajiwa na kwamba wakunga hao wapo eneo la Mapelele wilaya ya Mbeya na Iwambi Jijini Mbeya.
Kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi wanasema; '' Ni bora kupata ukimwi kuliko mimba kwasababu ukipata ukimwi unajulikana baada ya mud asana na unapata dawa za kurefusha maisha lakini mimba ukipata huwezi kuendelea na starehe na ukijifungua unalazimika kulea mtoto kwa muda mrefu huku na wanaume wengi hawaeleweki kwenye matunzo'' wanasema wanawake hao.
Wanawake wahudumu wa Bar walipoulizwa kuwa kwanini wanatumia zaidi majivu kama njia ya uzazi wa Mpango na utoaji Mimba walisema kuwa baadhi ya wanaume huwa hawapendi kutumia mipira (Condom) wakati wa kujamiiana hivyo baada ya tendo la ndoa wanalazimika kutumia njia hiyo kama moja ya njia rahisi ya kuzuia mimba kutotunga.
Walipoulizwa kama wanajua madhara ya kutumia huduma ya majivu na kisamvu kwa muda mrefu kama huduma ya uzazi wa mpango na utoaji mimba walisema kuwa hofu yao ni kwamba wanaweza kupata kansa au kutozaa tena.
''Ili kuepukana na kupata madhara ya kansa yanayoweza kutokana na majivu, huwa mtu akinywa basi siku hiyo anatakiwa kunywa maji kwa wingi ili kupunguza kemikali zitokanazo na majivu'' anasema Asha Juma.
Anasema yeye ni Mama wa watoto watatu na tangu amepata mtoto wake wa kwanza mwaka 1998 amekuwa akitumia majivu kila baada ya tendo la ndoa.
Na kwamba alipojaribisha kutumia vidonge alisumbuliwa na nyonga na kukosa hamu ya tendo la ndoa hatimaye akaenda kusafishwa na alipojaribisha sindano pia alipata madhara ya kukosa hamu ya tendo la ndoa ambapo mpaka sasa anatumia Majivu kama njia salama kwake ya uzazi wa mpango.
Baadhi ya madaktari waliohojiwa kwa sharti la kutoandika majina yao gazetini wamekiri kuhusika na biashara ya utoaji mimba kwa njia za kisasa na kuzitaja njia wanazotumia.
''Wenzetu kuna sheria za utotaji mimba lakini ajabu hapa Tanzania tunakataza wakati watu wengi wanatoa mimba tena hasa wake za watu na njia ambazo wengi tunazitumia kwa usalama zaidi ni kuwatundikia Drip za maji ya uchungu na vidonge vya uchungu vinavyoongeza njia kwa mwanamke''wanasema madaktari hao kwa nyakati tofauti.
Siku wanazotumia zaidi ni siku za Jumapili ambapo wanasema kuwa baada ya kumaliza utoaji huo wa mimba wanawake hao wanatoka wakiwa salama na kuwapatia dawa za kutuliza maumivu na kuwashawishi kula vyakula na vinywaji vya kuongeza damu.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa, katika sayansi ya akili watu wanaojamiiana huwa wanatumia kinga mara ya kwanza na ya pili baada ya kuanza mahusiano na huwa hawatumii tena kinga baada ya kukutana mara ya tatu na nne na kuendelea.
Sanjari na hayo imebainika kuwa wauguzi wengi huwa hawatumii njia za kisasa za uzazi wa mpango licha ya kuendelea kuwashawishi wananchi wengine kutumia njia hizo kwa madai kuwa vidonge hivyo huwa wakimeza haviyeyuki.
''Sisi wengi hatutumii kwasababu kuna madhara makubwa ukitumia kwa muda mrefu ambapo ukitaka kuzaa unalazimika kwenda kusafishwa kizazi na vidonge hivyo haviyeyuki na inatia hofu kuwa ukikwanguliwa unaweza usizae tena'' walisema baadhi ya wauguzi wa hospitali za Ifisi Mbalizi na hospitali ya wazazi Meta kwa sharti la kutotaja majina yao.
Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu, anasema kuwa mila na desturi ni tatizo katika utumiaji sahihi wa uzazi wa mpango na kwamba katika wilaya ya Mbeya Vijijini mwaka 2011 vilitokea vizazi hai 38 kati ya 100,000 na vifo 113.
Kwa upande wa Jiji la Mbeya mwaka 2011 anasema vizazi vilikuwa 109 kati ya 100,000 na vifo vilikuwa 363 ambapo katika uzazi huo hospitali ya wazazi meta ndiyo inahusika zaidi na inahudumia wanawake pia wanaotoka nje ya Jiji la Mbeya.
Chanzo: https://www.jamiiforums.com/blog/majivu-yatumika-kupanga-uzazi-na-utoaji-mimba-mbeya
=========
April 18, 2015:
Habari zenu wana MMU,
Habari za siku nyingi leo nataka nitoe ushauri kwa dada zangu au wadogo zangu, pia hata kwa kaka zangu kuhusu jinsi yakuweza kuzuia mimba kwakutumia njia ya asili tofauti na kama tujuavyo wengi wetu kwa sasa wamekua wakitumia njia kama vidonge vya kizuia mimba, sindano na vijiti ambapo njia hizo za za uzazi wa mpango zmekua na madhara makubwa kwa wanawake ikiwa na uke kua na maji na uvimbe tumboni.
Njia yenyewe ya asili ni majivu
Jinsi ya kutumia majivu ni unakoroga kijiko kimoja au viwili kwenye kikombe au grass sio lazima ijae maji unasubiri baada ya dakika tano ndio unakunywa na waweza kunywa majivu hayo lisaa limoja kabla ya tendo au baada ya tendo lakini yasizidi masaa sita baada ya tendo.
Ni njia nzuri sana na haina madhara pia ni njia ya asili na ni njia ambayo hata mimi nimekua nikiitumia na rafiki zangu pia.
3. Matumizi ya mbegu za Mnyonyo kupanga uzazi
SWALIHabari wapendwa
Naomba maelekezo na ushuhuda ikiwezekana namna ya kutumia mbegu za mnyonyo kuzuia mimba.
Please msaada
JIBU
Njia ya Kwanza: Kupanga Uzazi Unaweza kutumia mbegu ya mnyonyo 1 kwa ajili ya kuzuia mimba kwa muda wa mwezi mmoja . Unafanya hivi unapo maliza siku zako za hedhi ukishaoga kuwa msafi twanga mbegu 1 ya mnyonyo kisha unywe na maji utaweza kuzuia mimba isiweze kukuingia kwa muda wa mwezi mmoja utakuwa unafanya hivyo kila mwezi unapokuwa upo msafi. Tafadhali usile mbegu ya mnyonyo zaidi ya moja ni sumu unaweza kudhurika au kupoteza hata maisha yako.
Njia ya Pili: Yana kiasi fulani cha sumu ya protini ijulikanayo kitaalam kama ricin ambayo ikitumiwa kwa kiasi kidogo huharibu utungo, huweza pia kutumiwa kama mafuta ya kupaka ama losheni katika sehemu za siri ili kuua mbegu za uzazi za kiume wakati wa tendo la kujamiiana.
Tahadhari
- Mnyonyo ni mti wenye sumu inayoweza kuua binadamu au wanyama endapo itatumika kuzidi kipimo.
- Mazao yoyote yatokanayo na mnyonyo huhatarisha au/na kuharibu mimba na hata kuweza kusababisha kifo cha mjamzito, hivyo, matumizi yake lazima yawe ya uangalifu mkubwa.
4. Mwanaume kumwaga nje ya uke ( Pull Out Method )
Ieleweke kuwa hii njia ya"pull out method" huzuia mimba kama unajitambua vilivyo (yaani unajua wakati gani unakaribia a point of no return) na pili kama hakuna shahawa kwenye precum. Lakini kama umesha-cum mara ya kwanza halafu ukachomoa ili uendelee raundi nyingine basi uwezekano wa shahawa zilizobaki kwenye urethra kutoka na precum na kusababisha conception ni mkubwa.
Cha kufanya baada ya ku-cum nenda msalani kakojoe ili kuua shahawa (sperm) waliobakia kwenye urethra kwasababu mkojo una tindikali inatakayoua hao wanajeshi. Baada ya hapo endelea kama kawa la sivyo unatakuwa unacheza tu.
![]()
Mmea wa Gendarusa ambao unasemekana kuzuia wanaume kuzaa
Wanasayansi wanadai kuwa dawa mpya iliyozinduliwa ya mpango wa uzazi kwa wanaume imefanikiwa kwa asilimia 99.
Dawa hio imetengezwa kutoka kwa mmea ujulikanao kama Gendarusa ambao wanaume wa kisiwa cha Papua wamekua wakitumia kujizuia kuwashikisha wake zao mimba.
Mmea huo unasemekana kuwa na madini ambayo yanatatiza uwezo wa mbegu za kiume kuzalisha kwa kuzimaliza nguvu na pia kuzifanya kutoweza kuingia katika mayai ya mwanamke.
Profesa Bambang Prajogo, mtafiti mkuu wa mradi huo anasema ana furaha sana kuripoti kwamba dawa hio itaanza kuuzwa mwaka 2016 baada ya miaka mingi ya utafiti na majaribio.
Ingawa dawa hio ya mpango wa uzazi kwa wanaume ina athari zake, kama vile wanaume kuongeza uzazi wanapoitumia wanasayansi wanaamini kuwa athari hizo ni ndogo sana ikilinganishwa na dawa zinazotumiwa na wanawake kwani hauthiri sana homoni zao.
Dawa hio inaweza kumezwa saa moja tu kabla ya tendo la ndoa. Lakini wazee wa jamii hio huchanganya dawa hio na chai na kuinywa dakika thelathini kabla ya tendo la ndoa
Hata hivyo wanaume wanaambiwa wasiwe na wasiwasi kwani wanapata uwezo wa kuzalisha tena siku thelathini baada ya kusitisha utumizi wa dawa yenyewe.
Chanzo: BBC
