Njia za kufuata ili kutatua matatizo yoyote yale

Njia za kufuata ili kutatua matatizo yoyote yale

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Matatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu,,kwa maana kwamba kama kusingekuwa na matatizo basi huyu mwanadamu asingekuwa na umuhimu wowote hapa duniani

Kwahiyo shida na matatizo ndio yanatufanya tutafakari kwa kina,tuwaze na kuwazua na mwisho wa siku tunapata ufumbuzi

Kuna njia nne kuu za kufuata ili utatue changamoto zozote ambazo utakutana nazo

Mosi, hakikisha unajua shida au tatizo liliopo mbele yako,wataalamu wa mambo wanasema ,ukijua tatizo basi tayari utakuwa umefikia nusu ya suluhisho lake

Mfano,, kama mwanaume anasumbuliwa na nguvu za kiume,basi anatakiwa ajue kwanza je,tatizo ni la kisaikolojia au ni kimaumbile? Akitambua hasa shida ni nini atakuwa amefikia nusu ya sulihisho

Pili, tafuta majibu yote ambayo yanaweza kuwa suluhisho la tatizo husika,andika kila wazo liwe kubwa au dogo ambalo unahisi linaweza kuwa suluhisho

Tatu, waza na kuwazua au tafakari kwa kina kwa kuangalia,kila jibu upande wa hasara na faida,kisha tafuta jibu ambalo faida zake ni kubwa kuliko hasara

Nne, lifanyie kazi hilo suluhisho,ukishaamua kulifanyia kazi hilo suluhisho basi fanya na usianze tena kuwa na mashaka nalo,hata kama halitakuwa kwa asilimia mia moja lakini utakuwa umefikia hatua kubwa ya kupata ufumbuzi

Ni hayo tu!
 
Pia wasisahau kuwa umaskini ni mlundikano wa matatizo ambayo hajatatuliwa ,njia ya kukwepa matatizo ni kuuvuta umaskini.
 
When problems comes, not a single spy ,but in battalions. Alisikika william shakespeare akisema akiwa bar.
 
Back
Top Bottom