Njia za kunenepa.

Mwanakulipata

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2018
Posts
714
Reaction score
1,193
Habari zenyu... Kama kichwa kinavyojieleza hapo... Wanasemaga unene ni shida ila kuna watu tupo kama ubao uliokauka...tunaitaji mwili.... Kama kuna mtu anajua njia za kunenepa...au ushauri anaeza akashare...

uzi tayari
 
Habari zenyu... Kama kichwa kinavyojieleza hapo... Wanasemaga unene ni shida ila kuna watu tupo kama ubao uliokauka...tunaitaji mwili.... Kama kuna mtu anajua njia za kunenepa...au ushauri anaeza akashare...

uzi tayari
Njia pekee ya kunenepa ni kula chakula cha kutosha haswa vyakula vyenye mafuta mafuta.
 
Mm vilo vyaongezeka ila mwili uleule..
 
Mtu kuwa mwemba au unene inategemea na vitu vingi sana mfano.
1.Genetic/vinasaba. Kama umeumbwa mwembamba hata ufanye nini huwezi kunenepa hayo ndiyo maumbile yako.
2.Shughuli unazofanya.Kama wewe una asili ya unene na shughuli zako unazofanya zinahitaji nguvu nyingi kuliko uwezo wa mwili kuhimili huwezi kunenepa mkuu.
3.Chakula. Kama chakula unachokula ni kidogo au hakiko sawa kulingana na mahitaji ya mwili wako huwezi kunawili/kunenepa mkuu.
4. Stress. Kiwango cha stress alichonacho mtu kinaweza kumfanya mtu akanenepa au akakonda inategemea na mambo mengine.
............................................................
Youngblood
 
Acha roho mbaya kijana, utanenepa tu
 
Njia pekee ya kunenepa ni kula chakula cha kutosha haswa vyakula vyenye mafuta mafuta.
Sio mafuta mafuta. Hii ni slow way. Kwanza vitakukinai hutaweza kula amount inayotakiwa.

Piga vyakula na vinywaji vyenye processed sugars unenepe. Soda, majuice ya viwandani, chocolates, cake na cream yake and stuff of the kind
 
Kula mayai + ndizi za kuiva + maziwa kwenye sahani moja kila siku asubuhi na usiku, mchana hakikisha hukosa nyama choma kwenye mlo wako. Kwenye simu au laptop hakikisha una clips za vichekesho au story za kuchekesha.

Uje kunishukuru after 2 months
 
Ukiwa unakula unachotaka ukashiba/unalala pazuri/unavaa/huumwi hovyo hovyo/huna jambo linaloutatiza moyo muda mwingi/ una mpenzi anaeeleweka na anakuelewa
Una kazi/biashara ambayo inakufanya mda mwingi mwili uwe umerelax tu bila mikiki mikiki
Huna stress za ajabu ajabu ,hudaiwi kodi,hudaiwi ada/huvunji wala hujavunja sheria ya nchi
Umeridhika na hali yako kwa 90% moyo umeubwaga

Ukiyatimiza hayo usiponenepa basi kafanye surgery
 
Mkuu karibu kwenye chama chetu cha nyama ,michemsho ,supu na bia ..naamini utatimiza lengo lako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…