change is inclusive
New Member
- May 27, 2024
- 3
- 2
Uwajibikaji wa uzazi wa Mpango umeweka mzigo usio sawa kwa wanawake, licha ya ukweli wa kibaolojia kwamba wanaume wana uwezo wa kumfanya mwanamke apate ujauzito. Wanawake huzalisha idadi ndogo ya mayai kwa mwezi, (kwa kawaida moja) wakati wanaume hutoa mamilioni ya manii(Shahawa) kwa kufanya tendo moja tu la kujamiana.
Ingawa yai moja tu linaweza kurutubishwa na manii (sperm)mwanamume mmoja ana uwezo wa kuwapa mimba wanamke zaidi ya mia moja kwa shahawa zake.
Wakati wa ujauzito mwanamke hawezi kushika mimba tena(kwasababu tayari ana mimba nyingine) lakini, mwanamume anaweza kuendelea kuwapa mimba wanawake wengine (ni kama kusema ndani ya miezi tisa ya ujauzito mwanamke anashika mimba moja lakini mwanaume anauwezo wa kutoa mimba kwa wanawake wengine tisa na zaidi).
Mazingira ya sasa ya Njia za uzazi wa Mpango hayakubalinina tofauti hii.
Njia nyingi za uzazi wa mpango zinaelekezwa kwa wanawake, ikiwa ni pamoja na vidonge, vifaa vya kujipachika, na vifaa vya kuzuia mimba. Kwa upande mwingine, wanaume wanamachaguo machache (ukitoa kondomu na jelly ambao ndio imevumbuliwa hivi karibuni ambayo haijawafikia watumiaji hata 100) hii inaleta mzigo wa uwajibikaji usio sawa.
Jedwali : Matumizi wa uzazi wa mpango wa Dunia.
Chanzo; United Nations, World Contraceptives use.com
Takwimu zinaonyesha kuwa kote duniani, asilimia ndogo sana ya wanaume hutumia njia za uzazi wa
mpango (Tofauti na kondomu) huku ikionyesha upungufu wa machaguo yanayolenga wanaume. Kama matokeo, wanawake mara nyingi ndio wanaobeba na wanapewa mzigo mkubwa wa uzazi wa mpango.
Kihistoria, udhibiti wa uzazi wa mpango umekuwa ukishirikishwa na tamaduni na desturi za kijamii. Kutoka kwa tiba za mimea za zamani hadi njia za kisasa za uzazi wa mpango, jitihada za kudhibiti zimekuwa sehemu ya maendeleo ya kibinadamu.
Hata hivyo, Mzigo mkubwa na mzito umeelekezwa zaidi kwa wanawake, na umakini mdogo umetolewa kwa uzazi wa mpango kwa wanaume.
Kuibuka kwa teknolojia ya kisasa ya udhibiti wa uzazi wa mpango umeleta mageuzi katika sekta ya Afya. Lakini mzigo wa uwajibikaji wa jambo hili umebaki kwa kiasi kikubwa kwa wanawake. Licha ya maendeleo makubwa katika njia za uzazi wa mpango kwa wanawake, hakuna na maendeleo yanayotia moyo katika kuendeleza uzazi wa mpango kwa wanaume.
Madhara ya Uzazi wa Mpango kwa wanawake.
Ni muhimu kutambua madhara ya njia za uzazi wa mpango, haswa Yale wanayoyapata wanawake. Madhara ya kawaida ya njia za uzazi wa mpango za homoni, kama vile vidonge vya kudhibiti mimba au IUD za homoni, yanaweza kujumuisha kichefuchefu, maumivu ya kichwa, maumivu ya matiti (kifua), na mabadiliko ya hali ya mawazo/ msongo wa mawazo (stress)
Picha Jedwali la madhara ya Matumizi ya uzazi wa mpango.
Chanzo; Research Gate.com
Baadhi ya wanawake wanaweza pia kupata madhara makali zaidi, kama vile damu kuganda au kuongezeka kwa hatari ya saratani fulani kama saratani ya (matiti na shingo ya kizazi). Aidha, matumizi ya muda mrefu ya njia za uzazi wa mpango za homoni yanaweza kuathiri uzazi na mizunguko ya hedhikupelekea kutopata mimba au kutokuzaa kabisa(ugumba).
Sababu za ukosekanaji wa uzazi wa mpango wa wanaume.
Katika utafiti mdogo niliofanya 2023-2024. Inaonesha sababu kuu za kwanini njia za uzazi wa mpango kwa wanaume hazipatikani kwa urahisi ni pamoja na ;-
Mfumo wa dhana (conceptual framework).
Wanaume, kuna haja kubwa ya kuipa nguvu hii hoja, kwanini!Amini usiamini unapochukua hatua juu ya afya ya uzazi hasa uzazi wa mpango kuna mambo mengi sana unaepuka hizi ni baadhi ya faida za uwajibikaji kwa wanaume.
Wito wa Kuchukua Hatua:
Ili kushughulikia hii tofauti ya kijinsia katika uwajibikaji wa uzazi wa mpango, jitihada za pamoja zinahitajika kutoka kwa wadau mbalimbali.
• Serikali kupitia wizara ya Afya, wizara ya mipango na wizara zote zinazoguswa zinapaswa kuweka sera zinazozingatia jinsia na kutenga rasilimali kusaidia maendeleo na upatikanaji wa njia za uzazi wa mpango kwa wanaume.
“Kutokana na mipango ndani ya miaka 25 ijayo yaani 2050 Tanzania itakua na mara mbili ya idadi ya watu kuliko ilivo sasa yaani watu milioni 141.(Chanzo; worldbank.org) ni muhimu serikari kuzingatia ongezeko la watu na upatikanaji wa Rasilimali hivyo ni muhimu serikari kupitia hizo wizara husika ikishughurikia jambo la uwajibikaji wa uzazi wa mpango kabla hatuja chelewa”
• Wataalamu wa afya wana nafasi kubwa na jukumu muhimu katika kukuza ufahamu na kutoa huduma kamili za afya ya uzazi zinazojali wanaume na wanawake. “Wizara ya afya itoe ruzuku na pesa kufanikisha utafiti na uvumbuzi wa njia mpya za uzazi wa mpango zinazolenga wanaume zaidi.”
• Watafiti wanapaswa kupewa kipaumbele katika maendeleo ya njia za uzazi wa mpango zinazolenga wanaume ambazo ni salama, zenye ufanisi, na zinazoweza kurejeshwa. Mashirika ya utafiti yanayoshirikisha taasisi za serikali, taasisi za kitaaluma, na makampuni ya dawa yanaweza kuharakisha maendeleo katika jambo hili kwa kuweka kipaumbele kwa maslahi mapana ya Tanzania.
• Aidha, watunga sera lazima wahakikishe kuwa mfumo wa kisheria unawezesha idhini na usambazaji wa njia za uzazi wa mpango kwa wanaume.
• Zaidi ya hayo, Mashirika ya kijamii yanayo husika na nyanja mbalimbali ikiwemo wanawake, wanaume, vijana na watoto, waongeze ushiriki na elimu ya jamii katika kuvunja mazoea ya kijamii na kukuza usawa wa kijinsia katika afya ya uzazi. Kwa kukuza mazungumzo ya wazi na kuchukua hatua za kukabiliana na jukumu za kijinsia za jadi, jamii zinaweza kuunda mazingira yanayowezesha uwajibikaji wa pamoja wa uzazi wa mpango.
Nitafurahi kuiona Tanzania inafikia usawa wa kijinsia katika uwajibikaji. Tunahitaji mkakati mipana ambayo unashughulikia vikwazo vya kijamii, kitamaduni, na kimfumo. Kwa kuunga mkono chaguzi za uzazi wa mpango zinazolenga wanaume na kukuza ushirikiano wa pamoja, tunaweza kuwawezesha watu kufanya maamuzi ya busara kuhusu afya yao ya uzazi na kuchochea usawa katika mazoea ya uzazi wa mpango.

- Mfumo Dume; watu 7/10 wanaamini swala la uzazi wa mpango ni jambo la kike hivo haliwahusu wanaume kwakua mwanamke ndie anehusika na uumbaji moja kwa moja hivo anamaamuzi makuu katika uumbaji.
- Ukosefu wa fedha kwaajili ya utafiti na uwezeshaji wa maendeleo ya njia mpya.
- Ugumu wa kibaiolojia wa maumbile hasa mpangilio wa homoni kati ya mwanamke na mwanaume (ma Daktari na watu wa taaluma )
- Mifumo ya uthibitishaji (mamlaka za udhibiti wa ubora kwa Tanzania tunaongelea TBS). Haijandaliwa kudhibiti na kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo.
- Maslahi ya kibiashara kwa makampuni husika. Uzazi wa mpango wa wanaume hauna maslahi kibiashara hivo wengi hupoteza motisha kuhangaika nazo.
- Dhana za kitamaduni. Baadhi ya tamaduni zinaona uzazi wa mpango wa kiume kama si muhimu au kukubalika kidogo, kusababisha kutoa kipaumbele kwa utafiti unaohusiana.
Mfumo wa dhana (conceptual framework).
Wanaume, kuna haja kubwa ya kuipa nguvu hii hoja, kwanini!Amini usiamini unapochukua hatua juu ya afya ya uzazi hasa uzazi wa mpango kuna mambo mengi sana unaepuka hizi ni baadhi ya faida za uwajibikaji kwa wanaume.
- Hautosingiziwa mtoto, unapokua na usemi juu yako hakuna mwanamke atakae kupa mtoto wa kusingiziwa. Unajua ni lini hukutumia na uhakika ile ulimpa mimba.
- Hauta lea mtoto asie wako, labda uamue. Mtoto wa kupewa eti huyu ni wako inakua mwisho wake, hakuna cha nilipata kwa bahati mbaya hakuna cha ilitokea tu.
- Hakuna mimba za bahati mbaya. Kutokana na mfumo wa wanawake wa kibaiolojia mzunguko wa yai ni kitu kinachohitaji umakini sana kosa moja ni MIMBA. Lakini mfumo wa mwanaume ni tofauti kabisa utakua na uamuzi wa nani umpe mimba.
- Idadi ya watoto. Una uwezo mkubwa wa kuamua idadi ya watoto unaowahitaji kutokana na uwezo wako wa kuwakuza, kuwahudumia na kuwalea.

Upvote
1