chai ya moto
Member
- Jul 27, 2021
- 25
- 72
Serikali zote Duniani ni lazima ziwe na vyanzo vya mapato vya uhakika vya kuendeshea Serikali mapato hayo ni muhimu kwa sababu ndiyo yanayojenga barabara,yanayonunua silaha,yanayonunua madawa na kulipa mishahara na posho watumishi wa umma na wanasisa.Hivi karibuni kumeibuka mjadala kuhusu makato yanayofanywa na Serikali kupitia miamala ya simu za mkononi,mapato hayo yanaumiza kwa sababu Watanzania wengi ni mafukara wa kutupwa.
Baada ya kelele mbalimbali tarehe 23 julai 2021 Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai aliibuka na kuwataka wale wote wanaopinga tozo hizo watoe njia mbadala ili serikali ipate fedha za maendeleo.
Hizi zifuatazo zinaweza kuwa njia mbadala za Serikali kupata fedha za maendeleo
Kuongeza wigo wa mapato
Katika nchi yetu watu wanaolipa kodi ni wachache sana ni watumishi wa umma na watumishi wa sekta binafsi pamoja na wafanyabiashara waliosajiliwa na mamlaka ya mapato Tanzania ndiyo wanaolipa kodi.Kuna watu wengi sana wanaopata mapato makubwa lakini hawalipi kodi.Kwenye kundi hili kuna madalali,mafundi ujenzi,mafundi seremala,wafugaji,wakulima,watangaza matangazo ya biashara kupitia mitandao ya kijamii na wafanyabiashara wanaotumia mitandao ya kijamii kufanya biashara.
Niliamua kuwahoji watu wafuatao ili nijue namna wanavyofanya biashara zao nilianza na Seif Salum mkazi wa Mabibo Dar es salaam, na mpaka rangi kucha yeye aliniambia anapata shilingi elfu 30 kila siku lakini halipi kodi ya aina yoyote,Jakob Mushi mfanyabiashara wa soko la Loliondo Kibaha ana mtaji wa zaidi ya milioni sita akiwa anauza nafaka lakini halipi kodi zaidi ya ushuru wa soko shilingi 500 kwa siku.Joseph Kasongu dalali mashuhuri wa nyumba,viwanja na mashamba mkazi wa Maili moja Kibaha ana miliki basi dogo,amejenga na anasomesha kutokana na kazi yake ya udalali lakini halipi kodi ya aina yoyote.Mifano ya aina hii ni mingi sana na ipo kila kona ya Tanzania. Kinachotakiwa Serikali isajili Watanzania wote wanaostahili kulipa kupitia mtandao wa vitambulisho vya taifa na kuwapa namba za mlipa kodi waanze kulipa kodi.Kinachotakiwa nI kuwapangia kodi inayolipika kutegemea na vipato vyao na kwa utaratibu rafiki utakaowezesha watu walipe kodi bila kukimbizana.
Utalii
Tanzania ina vivutio vya kila aina kuliko nchi nyingi Duniani lakini kwa mwaka inapokea watalii wachache sana,mwaka 2016 ilipokea Watalii milioni 1.2,mwaka 2017 ilipokea Watalii milioni 1.3 na mwaka 2019 ilipokea Watalii milioni 1.5 wakati Tunisia mwaka 2019 ilipokea Watalii milioni 9.4 na kama isingekuwa ugonjwa wa UVIKO 19 mwaka 2020 wangeweza kuvunja rekodi ya kupokea Watalii milioni 10. Sera nzuri,huduma bora,mikakati mizuri pamoja na kutangaza vivutio vyao ndiyo siri ya kupokea Watalii wengi hakuna uchawi wala miujiza.Kwenye kutangaza Utalii tunashindwa hata na Rwanda inayotumia fedha nyingi kutangaza utalii kupitia michezo hasa kupitia vilabu mashuhuri vya soka Duniani vya Arsenal ya Uingereza na na PSG ya Ufaransa,leo hii mchezaji mashuhuri Dunani wa soka Lionel Messi anavaa jezi iliyoandikwa "tembelea Rwanda" sisi tumebaki tumebung'aa.Rwanda mwaka 2019 walipokea Watalii milioni 1.6 .Nchi ndogo isiyo na vivutio vingi inapokea idadi ya Watalii inayofanana na Tanzania!
Idadi kubwa ya Watalii ndiyo wingi wa fedha wanazoleta ni wakati wa Serikali na wadau wa utalii kujipanga na kutatua kero zinazowapata Watalii wakitembelea Tanzania pamoja na kutangaza kwa nguvu utalii wetu ili tupate fedha nyingi na kuachana na kuwabinya Watanzania kwenye tozo mbalimbali.
Rasilimali zilizopo chini ya ardhi
Kwenye ardhi ya Tanzania kuna gesi za aina mbalimbali na madini ya kila aina lakini rasilimali hizo bado hazijalinufaisha taifa kwa kiwango kikubwa.Kuna madini mengi bado hayajachimbwa.Mwaka 2013 niliwahi kutembelea machimbo ya madini ya rubi ya Ngembambili na Masuguru Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma ambayo yanachimbwa na wachimbaji wadogo wadogo ambao hawana vifaa ,ujuzi na tekinolojia inayotakiwa kwenye uchimbaji,wanachokifanya ni kuchimba juu juu na kuhamia sehemu nyingine.Pale wanapohama wanakuwa wameacha madini ambayo yanakuwa chini sana na hawawezi kuyafikia kutokana na kuwa na zana duni,kutokuwa na ujuzi na kukosa tekinolojia ya uchimbaji .Machimbo ya aina hii ni mingi sana inachotakiwa Serikali ishirikiane na wadau kufanya utafiti kwenye machimbo kama haya na kuwezesha madini yachimbwe ili fedha zipatikane za kujenga barabara,kulipa posho na mishahara Watumishi na Wanasiasa,kujenga madaraja na matumizi mengine muhimu ya Serikali.
Pia kuna sehemu nyigi za nchi ambako kuna rasilimali chini ya ardhi lakini bado hazijagundulika mfano kampuni ya Helium one mwaka 2016 iligundua gesi ya Helium mkoani Rukwa yenye ujazo wa futi za ujazo bilioni 98.9 za gesi hiyo muhimu na hadimu Duniani imeifanya Tanzania kuwa na hifadhi kubwa zaidi ya gesi hiyo Duniani.Kwa ugunduzi huo wa gesi ya Helium kuna uwezekano mkubwa wa Tanzania kuwa na gesi nyingine na madini mbalimbali ambayo hayagundulika au hayajaanza kuchimbwa kwahiyo Serikali ishirikiane na wadau kufanya utafiti na kukiwepo madini au gesi washirikiane na wawekezji kwa kumiliki hisa na uwekezaji wa aina hiyo siyo mgeni Tanzania kwani kwenye mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka uliopo Mbinga Ruvuma kampuni ya Intra energy inamiliki asilimia 70 na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Tancoal iliyo chini ya Shirika la maendeleo la Taifa inamiliki asilimia 30.
Rasilimali zilizopo chini ya ardhi kama zikichimbwa kwa kutumia sera nzuri,mikakati bora na kutanguliza uzalendo zinaweza kuipaisha nchi hii kiuchumi na Watanzania wakanufaika kwa rasilimali hizo kama ilivyo kwa nchi ya Botswana ambao uchumi wao wanategemea almasi ambayo inachangia asilimia 50 ya mapato ya Serikali.Botswana imefanikia sana kwenye madini kwa sababu ya ubia wa 50 kwa 50 na makiampuni yanayochimba almasi nchini humo.
Pamoja na vyanzo nilivyo orodhesha pia Watumishi wa umma walioajiriwa kwa kazi hiyo wasumbue vichwa vyao kutafuta vyanzo vya mapato na kuboresha vilivyopo badala ya kuhangaika na tozo za miamala ya simu.

Upvote
12