Njiwa wa kufugwa wamekuja Jenga kwangu, Sasa wamezaliana kibao. Nini maana yake?

Njiwa wa kufugwa wamekuja Jenga kwangu, Sasa wamezaliana kibao. Nini maana yake?

Niliwahi kufuga njuwa nikiwa p/s.
Tabia moja ya njiwa ni kuwa hawapendi usumbu.
Ukimchinja mmoja hadharani wengine hutoroka.
Njiwa wengine huamia bila kujua walikotoka.
Njuwa hutumiwa na waganga, Niliuza sana njiwa weusi na weupe pee.
Njiwa huleta furaha ya moyo.
Nyumbani au jirani kukiwa na msiba njiwa nao huweka matanga, hubaki vibandani mwao.
Njiwa humtambua bisi wao wanaweza kukurukia hata begani.
Mungu akijalia ntakuja kufuga tena njiw wanaleta puece of mind.
 
Njiwa ni viumbe wa AMANI....

Njiwa hukaa na kuishi penye UTULIVU ,UPENDO na MLO.....

Ukiona wametulia hapo kwako ujue pamejaa BARAKA......

Endelea kuwalisha utazidi "KUFUNGULIWA"......

#MfugaNjiwa
#Yetzer-ha-tov
Da mi waliniita mla njwa.
Nilifuga kama 100.
 
Wakuu naombeni majibu.Inafaa kuwakaanga na kula
Dah! Kweli upele humpata asiye na kucha! Yaani Allah amekuletea kitoweo chenye vitamini ya kutosha mwilini, halafu wewe unakuja kuuliza majibu badala ya maswali!
 
njiwa hawapendi masengenyi na ugomvi ukiwasengenya wanahama wote
Kweli kabisa, kuna dada aliwafuga wakawa wengi, akasafiri kama miezi 3 akawaachia mlinzi na nduguze wawalishe, wakawa wanawasimanga njiwa wale wanakula Sana, wanakunya ovyo, wanapiga kelele. Aisee walihama, walirudi mmoja mmoja baada ya Yule sister kurudi!

Nilikuwa siamini hii kitu!
 
Back
Top Bottom