Njombe: Ahukumiwa miaka mitano jela kwa kosa la ushirikina

Njombe: Ahukumiwa miaka mitano jela kwa kosa la ushirikina

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Mahakama ya Wilaya ya Ludewa imemhukumu kifungo cha miaka 5 jela John Chale(60) mkazi wa kata ya Ilela wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa kosa la kumfanyia vitendo vya kishirikina mtoto wa mdogo wake Videana Chale(18) na kupelekea kupata ukichaa.

Akisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya Ludewa Isaac Ayengo imeelezwa kuwa binti huyo alipatwa na kichaa ambapo wazazi wake walimpeleka kwa mganga wa kienyeji ndipo walipoambiwa kuwa amerogwa na mshtakiwa huyo.

Lakini hawakuishia hapo walimpeleka kanisani nako ikagundulika hivyo pia ndipo walipoamua kumuuliza mshtakiwa huyo kwakuwa amekuwa na tabia ya vitendo vya kishirikina na anamiliki nyoka ndani ya nyumba yake ambaye kwa macho ya kawaida amekuwa akionekana kama jiwe.

Aidha mshtakiwa huyo alikiri kutenda kosa hilo ndipo baba mzazi wa mtoto huyo Hekima Chale akaamua kupeleka jambo hilo katika vyombo vya sheria ambako mtuhumiwa huyo alikana lakini baada ya kufanyika upelelezi na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili mahakama ilijilidhisha kuwa yeye ndio ametenda kosa hilo.

Mwendesha mashtaka wa serikali aliiomba Mahakama kumpatia mshitakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na jamii kwa ujumla kwani vitendo vya kishirikina vinasababisha migogoro ya familia na jamii kwa ujumla na kupelekea mauaji na baada ya hoja hizo Mahakama imeamuru mshitakiwa kutumikia kifungo cha Miaka 5 gerezani.

Source: Issa Michuzi
 
Kule mpk mwenyekiti wa wachawi anajulikana, nilikuwa huko 2006, tilipewa taadhali kwenye msiba hakuna kula mpk ukaribishwe/ upewe chakula la sivyo utajuta maana wanachokula siyo chakula cha msibani km tulivyozoea huku mitaa ya pwani.
Aiseee yaani wanautukuza uchawi? Sasa Hawa manabii wanaomangamanga huku mjini na miujiza si wakaweke Kambi huko waufurumushe uchawi🤔🤔🤔
 
Waende huko km watu hawajala miguu yoote wakabakisha mapaja. Kwa sasa mchanganyiko kidogo upo wa watu enzi nzile ukizozana na mtu utaipata cha moto.
Aiseee hatari sana
 
Kuna kifungu kwenye sheria kimezungumzia uchawi na ushirikina, maana huko ni hatari mpaka mwenyekiti wa wachawi anajulikana na ana nguvu
Vipo,huko wapelekewe dini na elimu vinasaidia kupunguza huo ujinga
 
Back
Top Bottom