TANZIA Njombe: Anthony Mwandulami Afariki Dunia. Alijijengea kaburi la mamilioni ya shilingi

Alikua mganga wa jadi bwashee ni maarufu Sana mkoani Njombe ila ni Aina ya wale waganga wanaojiganga maana alikua njema Sana kiuchumi na ana miradi kibao!
Miongoni mwa mambo yaliyoshangaza ni
  1. TRA walikwenda kumkagua wakitaka kodi, akawakaribisha kwenye viti na kuwapa nyaraka zake wazipitie, muda mfupi wote wakapitiwa usingizi mzito wakaja kuzinduka jioni, hawakutaka kumsikia tena wakaondoka.
  2. Alifuga nyuki chini ya Nissan yake kama walinzi.
  3. Inasadikika alipata kutumia nguvu ya jadi kumfanya mbaya kibaka pale Mnazimmoja Dar baada ya kumwibia mizigo yake
 
Hayo madirisha aliweka ya kazi gani kwenye kaburi, designer wake atufunguwe akili

View attachment 1840366
Mkuu,inasemekana kaburini kuna joto Kali sn.Kwa hiyo hayo madirisha ni Kwa ajili ya kupitisha hewa iingie ndani..Ila mm siyo designer wake

Kaburi nyumba ya milele,haina kupigiwa hodi wala haina kudaiwa kodi.Anatulia zake Safi kabisa huku hewa Safi na mwanga vikipita dirishani
 
acha masikhara shekhe
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
So story yake imeishia hapo.Anatukumbusha kwamba sisi ni Binadamu tuu. "Memento Homo".Tusije tukasahau,kwamba sisi ni binadamu tuu.Fedha na Dhahabu ni mali ya Bwana Full stop.

So hata lingekuwa kaburi la trilioni halina masaada wowote kwake kwa hapo alipofikia

Polen wafiwa wote na wote walioguswa
 
Mkuu kumbe yule mzee unampata daaa wewe utakua Mtwango unapapata vema,
Yule mzee alikua maarufu Sana enzi zile Hadi akajijengea kaburi lake lipo pale njiani Kama unaenda Mtwango Secondary mkono wa kushoto Barabara ya Makambako_ Songea !
 
heeheee huyu mzee alikua na heshima zake hapa nchini wasukuma wa Ubaruku mbarali Mbeya hawatamsahau alikua anawatetea Sana kwenye migogoro yao maana ndio walikua wateja zake wakubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…