Njombe: Binti afariki baada ya kupigwa na Shangazi yake kwa kuchelewa kurudi nyumbani

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia mwanamke aliyefahamika kwa jina la Apronia Mwinuka(35) mkazi wa mtaa wa Kikula kata ya Makambako mkoani Njombe kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo shangazi yake Elina Mwinuka (18) kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa anasema uchunguzi umebaini binti huyo amefariki kutokana na kipigo alichokipata huku ikidaiwa alichelewa kurudi nyumbani kutokana na kupitia kwa mpenzi wake.

“Alichokifanya shangazi alitoa adhabu, aliamua kutoa adhabu ya kipigo kwa huyu binti na anasema yeye alipitia kwa mtu ambaye mpenzi wake,kwa hali kama hiyo shangazi alikasirika kwanini alichelewa,na kile kipigo kilisababisha binti akafariki dunia wakati akipelekwa kupata matibabu”

Mume wa Apronia, Thadei Mhongole amesema tukio hilo limetokea wakati yeye akiwa kwenye shughuli za utafutaji na aliporudi alikuta binti huyo akiwa amezimia baada ya kupigwa na shanganzi yake.

“Ni mtoto wa kakaangu kwa kweli kuondokewa na huyu ndugu yangu ninasikitika sana,wito wangu hasa kwa akina mama wawe na kiasi katika kuwaonya watoto”alisema Mhongole

Baadhi ya majirani wa familia hiyo wamesema kuwa mwanamke huyo amekuwa na tabia ya kuwaadhibu watoto mara kwa mara.

“Ni kawaida yake kuwaadhibu hata watoto wake mara kwa mara hata wakipoteza mkoba sasa adhabu ya juzi ikawa imezidi kipimo ikampekea mtoto kukata roho kabisa,tulipokagua kwenye nyumba yao tulikuta kuna njiti za mihanzi ambazo alikuwa anamtandikia na vipande viwili vimebanduka kabisa”alisema mmoja wa majirani

Keneth Solomon Kibiki ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kipagamo kata ya Makambako,amekemea vitendo hivyo.

“Tukio hili linatuhuzunisha sana viongozi na tunakemea lisijiludie kwasababu adhabu zinapitiliza mpaka tunapunguza nguvu kazi ya taifa”,alisema Keneth Solomoni.
 
Watu hawaoni hasara kukatisha ndoto za vijana tunaowahitaji kuja kulikomboa taifa lililojaa chuki na roho za ubinafsi na ufisadi kwa viongozi
 
Mmh jaman huyu Aunt ilimuua bint yake kuwa na mshkaji au naye alikua anamtaka jamaa au yawezakuwa kweli alikuwa hata bintiye ajiingize katika mambo hayo. rip
 
Kanuni ya Maisha kati ya mtoto na mzazi au mlezi ipo wazi. Mzazi amepewa wajibu wa kumtunza na kumlea pia kumpa mahitaji yake yote kadri ya uwezo wa mzazi/mlezi.

Hata kwenye Sheria zetu za Tanzania kwenye Sheria ya mtoto inampa mzazi wajibu huohuo. Hata kwenye biblia wajibu huo amepewa mzazi/mlezi. Kwa maantiki hiyo mtoto ana Haki ya kupata hayo kutoka kwa mzazi/mlezi bila upendeleo wala masharti kwa sababu ni maagizo.

Lakini Duniani kote hakuna Haki bila wajibu. Katika hayo yote,kanuni hiyohiyo imempa mtoto wajibu wa KUWAHESHIMU WAZAZI/WALEZI na KUWATII. Kwenye hili Mungu aliweka mkazo zaidi akaweka ktk Amri zake kumi.

Ile Amri ya nne inaagiza watoto KUWAHESHIMU WAZAZI/WALEZI. Na Mungu kwenye Amri ile akawapa na ahadi kuwa wakiwaheshimu wazazi wataishi miaka mingi na Heri Duniani. Hii ndiyo Amri pekee yenye ahadi. Tukirudi kwa marehemu,alistahili hiyo adhabu kutokana na kuvunja kanuni ya Maisha,kuvunja Sheria za Tanzania na Amri ya nne ya Mungu. Huyu hata mbinguni hawezi kwenda labda utokee muujiza!
 
Bado hujakua ukiwa na mtoto wa kike wa miaka 18 afanye hayo ndiyo tutajua utamruhusu au utamzuia!

Kwangu; Kumuadhibu huyo binti haikuwa tatizo sana coz bado alikuwa katika umri unaotoa maamuzi si sahihi sana wanahitaji uangalizi wa karibu na maonyo, kosa hapo ni kutoa adhabu iliyopitiliza mpaka kupelekea kifo cha binti.

Wakati mwingine inawezekana adhabu haikuwa kubwa sana ila katika kurukaruka na kugalagala kajigonga mahali kafa, ukisoma vizuri majirani wanasema walikuta vijiti vya mianzi!

Wangesema magongo ingekuwa balaa!

Lala vyema binti mdogo!
 
Daaah inauma Kwa kweli, hasa huyo jamaa ake.. Naye alipaswa kuunganishwa kwenye kesi
 
Mkuu magode Hakuna imani yoyote inayoruhusu mtoto kuuwawa kwa kutoheshimu wazazi.
Saa nyingine ujuaji ukizidi unakua up.umba.fu....swala la kufika mbinguni muachie Mungu usihukumu huna mamlaka hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kwa shangazi mtu,sipati picha ana maumivu na majuto kiasi gani moyoni mwake japo yeye alikua anatekeleza wajibu wake kumuadhibu mtoto kama kawaida ya wazazi wote wakiona mtoto anaenda njia isiyo sahihi.

Mtoto wa miaka 18 tena msichana kuendekeza mapenzi kwa umri huo ni hatari na sio sahihi hasa kama alikua mwanafunzi, RIP kwake[emoji120]
Natumai vyombo vya sheria vitatenda haki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanuni ya Maisha kati ya mtoto na mzazi au mlezi ipo wazi. Mzazi amepewa wajibu wa kumtunza na kumlea pia kumpa mahitaji yake yote kadri ya uwezo wa mzazi/mlezi.

Hata kwenye Sheria zetu za Tanzania kwenye Sheria ya mtoto inampa mzazi wajibu huohuo. Hata kwenye biblia wajibu huo amepewa mzazi/mlezi. Kwa maantiki hiyo mtoto ana Haki ya kupata hayo kutoka kwa mzazi/mlezi bila upendeleo wala masharti kwa sababu ni maagizo.

Lakini Duniani kote hakuna Haki bila wajibu. Katika hayo yote,kanuni hiyohiyo imempa mtoto wajibu wa KUWAHESHIMU WAZAZI/WALEZI na KUWATII. Kwenye hili Mungu aliweka mkazo zaidi akaweka ktk Amri zake kumi.

Ile Amri ya nne inaagiza watoto KUWAHESHIMU WAZAZI/WALEZI. Na Mungu kwenye Amri ile akawapa na ahadi kuwa wakiwaheshimu wazazi wataishi miaka mingi na Heri Duniani. Hii ndiyo Amri pekee yenye ahadi. Tukirudi kwa marehemu,alistahili hiyo adhabu kutokana na kuvunja kanuni ya Maisha,kuvunja Sheria za Tanzania na Amri ya nne ya Mungu. Huyu hata mbinguni hawezi kwenda labda utokee muujiza!
Umehukumu sana mkuu,sio sawa. Inawezekana alikua na mazuri yake pia huyo mtoto.
Hukumu tumuachie mwenye mamlaka yake...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
napingana na wewe. Kumpiga sio suluhu ya hilo tatizo . miaka 18.ameshakuwa mkubwa unaweza ukamuozesha sio kushindana nae.
Nyege ni kitu kibaya sanaaa. Hauwezi kumzuia mtu asifanye mapenzi ikiwa anakula vizuri.
magode,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Isije ikawa Shangazi mtu nae alikuwa anashea mkuyenge na huyo Binti..
 
Miaka 18 si mtu mzima? Angemwambia tu amlete huyo kijana amtambulishe waondoke nae hapo..
 
Pole kwa shangazi mtu,sipati picha ana maumivu na majuto kiasi gani moyoni mwake japo yeye alikua anatekeleza wajibu wake kumuadhibu mtoto kama kawaida ya wazazi wote wakiona mtoto anaenda njia isiyo sahihi.

Mtoto wa miaka 18 tena msichana kuendekeza mapenzi kwa umri huo ni hatari na sio sahihi hasa kama alikua mwanafunzi, RIP kwake[emoji120]
Natumai vyombo vya sheria vitatenda haki

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani sheria ili utambulike kama mtu mzima ni hadi ufikishe umri wa miaka mingapi?.au siku hizi ni 30 sio 18 tena.
 
Alochofanya huyo shangazi ni mauaji wala hakiusiani kabisa na imani sijui wajibu au nini.Nauko kwa Mungu yeye ndiye atakayechomwa moto.Uyo binti alishafikisha umri wa mtu mzima alichotakiwa kufanya nikukaa naye chini nakuongea naye kwautulivu sio kumpiga.sasa inaonekana shangazi ana matatizo yake yamaisha hasira akaamishia kwa mwingine.Fimbo zakuonya siku zote haziwezi kukatisha uhai wa mtu.
Kanuni ya Maisha kati ya mtoto na mzazi au mlezi ipo wazi. Mzazi amepewa wajibu wa kumtunza na kumlea pia kumpa mahitaji yake yote kadri ya uwezo wa mzazi/mlezi.

Hata kwenye Sheria zetu za Tanzania kwenye Sheria ya mtoto inampa mzazi wajibu huohuo. Hata kwenye biblia wajibu huo amepewa mzazi/mlezi. Kwa maantiki hiyo mtoto ana Haki ya kupata hayo kutoka kwa mzazi/mlezi bila upendeleo wala masharti kwa sababu ni maagizo.

Lakini Duniani kote hakuna Haki bila wajibu. Katika hayo yote,kanuni hiyohiyo imempa mtoto wajibu wa KUWAHESHIMU WAZAZI/WALEZI na KUWATII. Kwenye hili Mungu aliweka mkazo zaidi akaweka ktk Amri zake kumi.

Ile Amri ya nne inaagiza watoto KUWAHESHIMU WAZAZI/WALEZI. Na Mungu kwenye Amri ile akawapa na ahadi kuwa wakiwaheshimu wazazi wataishi miaka mingi na Heri Duniani. Hii ndiyo Amri pekee yenye ahadi. Tukirudi kwa marehemu,alistahili hiyo adhabu kutokana na kuvunja kanuni ya Maisha,kuvunja Sheria za Tanzania na Amri ya nne ya Mungu. Huyu hata mbinguni hawezi kwenda labda utokee muujiza!
 
Umeanza vizuri but umemalizia kama nyumbu

Hakuna mtu mwenye mamlaka juu ya uhai wa mtu mwingine

Back
Top Bottom