Kanuni ya Maisha kati ya mtoto na mzazi au mlezi ipo wazi. Mzazi amepewa wajibu wa kumtunza na kumlea pia kumpa mahitaji yake yote kadri ya uwezo wa mzazi/mlezi.
Hata kwenye Sheria zetu za Tanzania kwenye Sheria ya mtoto inampa mzazi wajibu huohuo. Hata kwenye biblia wajibu huo amepewa mzazi/mlezi. Kwa maantiki hiyo mtoto ana Haki ya kupata hayo kutoka kwa mzazi/mlezi bila upendeleo wala masharti kwa sababu ni maagizo.
Lakini Duniani kote hakuna Haki bila wajibu. Katika hayo yote,kanuni hiyohiyo imempa mtoto wajibu wa KUWAHESHIMU WAZAZI/WALEZI na KUWATII. Kwenye hili Mungu aliweka mkazo zaidi akaweka ktk Amri zake kumi.
Ile Amri ya nne inaagiza watoto KUWAHESHIMU WAZAZI/WALEZI. Na Mungu kwenye Amri ile akawapa na ahadi kuwa wakiwaheshimu wazazi wataishi miaka mingi na Heri Duniani. Hii ndiyo Amri pekee yenye ahadi. Tukirudi kwa marehemu,alistahili hiyo adhabu kutokana na kuvunja kanuni ya Maisha,kuvunja Sheria za Tanzania na Amri ya nne ya Mungu. Huyu hata mbinguni hawezi kwenda labda utokee muujiza!