Njombe: Edina amekutwa amefariki chumbani baada ya kupaliwa na chakula

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Edina Chaula (23), mkazi wa Mtaa wa Kihesa, Halmashauri ya Mji wa Njombe, amekutwa amefariki dunia ndani ya chumba chake baada ya kudaiwa kukosa hewa kutokana na kupaliwa na chakula.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi Mahamoud Banga, amesema tukio hilo liligundulika Agosti 23, 2026, majira ya mchana, baada ya mwili wa marehemu kukutwa ukiwa ndani ya chumba hicho.

Amesema kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, marehemu huenda alifariki siku nne hadi tano kabla ya mwili wake kugundulika.

Kamanda Banga amesema hakuna dalili zinazoashiria kuwa Edina aliuawa, akieleza kuwa mlango wa chumba ulikuwa umefungwa na ulilazimika kuvunjwa chini ya usimamizi wa viongozi wa Serikali ya Mtaa.

“Amekutwa amefia ndani, ni zaidi ya siku nne au tano. Sio kwamba ameuwawa kwa sababu mlango ulikuwa umefungwa na ulivunjwa chini ya uongozi wa Serikali ya Mtaa,” amesema Banga.

Aidha, amesema ndani ya chumba hicho kulikutwa pombe kali maarufu kama ‘Visungura’.

Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kwa kina mazingira ya kifo hicho.
 
Edina(KE-23)..Kisungura??Siyo kisirani na hasira baada ya kumuudhi akaonanajitoe uhai kwa kuchanganya simu kwenye Kisungura!!!? Mbona mdogo kwa umri???
R.I.P Edina..Hakuwa anaishi na Mama wa Kambo labda???Haya ndiyo mambo ya Msingi kwa Polisi kuyafuatilia...Ajabu wamekuwa ni watabiri wa mambo yanayohitaji utaalamu wa Kitabibu ..Amepaliwa chakula-Edina,Binadamu tunatembea na Maradhi- Mwanafunzi wa Bunda,Ni kifo cha kawaida-Dereva wa Heche!!!!!????
 
Uyo penz limembeba na njia hiyo iringa road ndio inaongoza kujichomoa uhai
 
Hapo Kihesa pombe yetu ni ulanzi baridi pekee. Pombe kali ni huko Moshi na Arusha.
 
unajitunza vizuri usipate magonjwa mabaya, unajitahidi kujiepusha na ajali za barabarani alf unakuja kufa kwa kupaliwa na chakula dadeqq kifo ni usiengeeeee,,,

RIP Edina
 
Alipaliwa kisungura? Mbona hawasemi chakula walichokikuta?
 
Visungura? Sio Ali over drinking? Polee yake na RIP.
 
Choked on her own vomit. Hii ni hatari sana kwa walevi.
 
unajitunza vizuri usipate magonjwa mabaya, unajitahidi kujiepusha na ajali za barabarani alf unakuja kufa kwa kupaliwa na chakula dadeqq kifo ni usiengeeeee,,,

RIP Edina
Daaah☺️☺️
 
Aiseeeee!!!

Hajauawa kwasababu mlango umekutwa ukiwa umefungwa kwa ndani!!!!

Hivi mfano huu mlango wenye kawavu ka kuzuia mbu kwa juu, siwez kuua halafu nikapita hapo kwa juu zen nikaurudishia huo wavu??

Nyumba kama haina sngbod siwez kuua nikarukia chumba chapili?

Tuseme ina sngbod, ila singbod sikuna vdrsha vya kupandia huko darini?

Vp kuhusu dirisha la nyumba? Kuna mtu anaweza kupita mlangoni akaingia na kufunga kwa ndan halafu akatokea dirishani, ukifika kwake utajua yumo kumbe hayumo.

Mwingine anaweza kufunga kufuri nje then akaingia ndan kupitia dirishan ukiona kufuri unajua hakuna mtu, kumbeee!!!

Mimi nyumba yangu ina madilisha tisa ya grill na vioo, kikawaida hua hamna namna ya kufungua hzo nondo bali kioo ndo kinaslide, lakini kuna madirisha mawili ya siri yanafunguka na naweza nikawepo ndani usijue!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…