Ajali mbaya imetokea jioni ya leo 24.04.2022 majira ya saa 11.30+ ikihusisha coaster na lori la makaa ya mawe, watu kadhaa wanatajwa kupoteza maisha, taarifa zaidi zitatolewa na mamlaka husika.
====
Zaidi ya Watu watatu wanahofiwa kufariki baada ya gari aina ya coster iliyobeba vijana wa kwaya ya vijana wakatoliki wa Njombe (UVIKANJO) ambao walikwenda kutembelea watoto yatima katika kituo cha Ibumila kugongana uso kwa uso na gari ya makaa ya mawe iliyoacha njia na kuigonga coster hiyo katika eneo la Igima.
Kuna majeruhi ambao idadi yao bado haijajulikana.
====
Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika zinasema hadi leo tarehe 25.04.2022 idadi ya waliofariki kutokana ajali ya jana vimefikia nane (8). Mwenyezi Mungu awarehemu wapumzike kwa amani
View attachment 2199179
View attachment 2199180
View attachment 2199182
View attachment 2199279View attachment 2199503View attachment 2199504