Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2015 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Njombe. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.
Mkoa wa Njombe una jumla ya majimbo ya uchaguzi 6. Wabunge walioshinda kwenye hayo majimbo ambayo ni
Njombe Kaskazini: Ndugu Joram Hongoli (CCM)
Njombe Kusini: Edward Mwalongo (CCM)
Makambako: Ndugu Deo Kasenytenbda Sanga (CCM)
Wanging'ombe: Nduguy Gerson Hosea Lwenge (CCM)
Ludewa: Uchaguzi Uliahirishwa baada ya Mbunge Deo Filikunjombe Kufariki.
Makete: Norman Adamson Sigalla (CCM)
ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
Kutoka 9jombe jimbo la makambako. Kituo cha Ikando. Hali ni shwarii kabisa watu wamepanga foleni toka saa 11. Wana hamasa kubwa ya kutekeleza haki yao ya kikatiba. Vijana ni wengi na wametulia wakisubiri kuchinja..........
Kutoka Njombe jimbo la makambako. Kituo cha Ikando. Hali ni shwarii kabisa watu wamepanga foleni toka saa 11. Wana hamasa kubwa ya kutekeleza haki yao ya kikatiba. Vijana ni wengi na wametulia wakisubiri kuchinja..........
kutoka jimbo la njombe kusini, kituo cha lunyanywi (hagafilo) hali ni shwari, watu wamejitokeza kupiga kura, wanaume ni wengi kuliko wanawake katika kituo hiki, labda baadaye wanawake watajitokeza. Mungu ibariki Tanzania.