Njombe: Mfungwa apora Bunduki kwa Askari na kumpiga kaka yake kwa kushindwa kumtoa Gerezani na kuuza mashamba ya familia

Naona kama kamanda wa polisi anajifunza kuongea, sijaelewa elewa bado
Huyu bwana kweli hana skills za kuongea. Huongea ongea tu Mambo mambo yake kwa lugha ya kubabaisha Sana. Ni mchapa kazi lakini ajengewe speeching skills.
 
Kijana, Isaack Kawogo(24) aliyempora Askari magereza silaha aina ya SMG Usigani mkoani Iringa ameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi baada ya kumjeruhi kaka yake, Andres Kawogo(61) akimtuhumu kuuza mashamba na kushindwa kumtoa gerezani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amesema tukio hilo limetokea Novemba 20, huko maeneo ya Chaugingi mjini Njombe.

Amesema Kawongo aliiba silaha na kuitumia kufanya uhalifu ambapo alifanya matukio kadhaa Mkoani Iringa ikiwemo kumshambulia Askari kwa panga hali iliyosababisha wafungwa wengine kutoroka.

“Hii ni silaha ambayo askari magereza wanaitumia katika ulinzi wa wafungwa hao sasa huyu kwakuwa ni mhalifu akawa anaitumia katika kufanya uhalifu,” Kamanda Issah.

Amesema silaha hiyo ilikuwa na risasi kumi lakini mpaka inakamatwa na askari ilikuwa imebakiwa na risasi mbili pekee huku risasi nane zikitumika kufanya ualifu maeneo tofauti ikiwemo tukio hilo lilotokea Mkoani Njombe la kumjeruhi kaka yake.

Amesema licha ya juhudi kufanyika za kutaka kuokoa maisha yake ili alieleze Jeshi la Polisi namna alivyoondoka na silaha lakini ilishindikana kwa kuwa umauti ulimfika.

” Ukimnyang’a askari silaha namna pekee ya kuipa hiyo silaha ni kwa kutumia silaha hivyo wanapaswa kuwa makini,” Kamanda Issah
Nimetumia energy nyingi sana kuielewa hii habari ila juhudi zote zimeshindikana. Alieielewa hii taarifa naomba summary yake tafadhali
 
Hii habari labda mm pekee nimeshindwa kuielewa,

Yaan uwe mfungwa umpore Askari silaha umpige nayo mtu(hapa ni Kama tukio lililotekelezwa kwa haraka sana) sasa inakuaje kaenda kufanya nayo matukio mbali mbali na kutumia risasi zote7 wakati ni mfungwa?

Alafu et asingekufa angeeleza aliwezaje kutoka na silaha(hapa hakumpora mtu)
Hili picha la kihindi mie sijalielewa kabisa
 
Isije kuwa pesa zilizitokana na Mashamba yaliyouzwa ndizo zilitumika kumlegeza Afande aporwe silaha kirahisi! Anyway Pole kwa Familia ya Afande Magereza aliyepigwa panga na Pole kwa Familia ya Mfungwa Marehemu.
 
Hii habari labda mm pekee nimeshindwa kuielewa,

Yaan uwe mfungwa umpore Askari silaha umpige nayo mtu(hapa ni Kama tukio lililotekelezwa kwa haraka sana) sasa inakuaje kaenda kufanya nayo matukio mbali mbali na kutumia risasi zote7 wakati ni mfungwa?

Alafu et asingekufa angeeleza aliwezaje kutoka na silaha(hapa hakumpora mtu)
kaiba bunduki, katoroka gerezani akenda mtaani kufanya matukio ya uhalifu.
 
Duuuuh, Askari magereza ndio wenye kozi ndefu kuliko baadhi ya majeshi nchini.
Ilikuwaje huyo Askari Magereza aporwe silaha na mfungwa?
Bila shaka pombe ilihusika.
 
Kumchinja Kobe Yataka Timing
Bado napatwa na wasiwasi maana ukiwa na silaha unaambiwa hata kama ni chooni kunya ingia nazo hata askari mwenzio usimwamini kumwachia au ukiwa na silaha mtu akae mbali na wewe umbali wa mita moja na kuendelea sasa huyu soldier hadi mfungwa anaichukua bado sielewi elewi
Ina maana hata angamua kumpasua nayo huyo askari bado uwezo angekuwa nao sasa
 
Nadhani kuna tatizo kwenye hii habari.
Mfungwa amempora askari magereza silaha... kisha akaitumia kumuua kaka yake.

Kisha inaonekana silaha imetumika kufanyia matukio mengine ya kihalifu... na takribani risasi nane zimetumika...

Tukio lilifanyika wapi, wakati gani.. na ilichukua muda gani kwa tukio kutendeka.. na je mfungwa alitumia silaha hiyo pia kutoroka?
 
Hii habari labda mm pekee nimeshindwa kuielewa,

Yaan uwe mfungwa umpore Askari silaha umpige nayo mtu(hapa ni Kama tukio lililotekelezwa kwa haraka sana) sasa inakuaje kaenda kufanya nayo matukio mbali mbali na kutumia risasi zote7 wakati ni mfungwa?

Alafu et asingekufa angeeleza aliwezaje kutoka na silaha(hapa hakumpora mtu)
Umeona eeeh.
Bado hawajajua aliporaje, si wamuulize aliye porwa.
Siku hiyo hiyo apore silaha
Kawaruhusu wenzake watoroke
Amuadhibu Kaka yake
Halafu dogo Yuko 24 only.
 
Kijana, Isaack Kawogo(24) aliyempora Askari magereza silaha aina ya SMG Usigani mkoani Iringa ameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi baada ya kumjeruhi kaka yake, Andres Kawogo(61) akimtuhumu kuuza mashamba na kushindwa kumtoa gerezani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amesema tukio hilo limetokea Novemba 20, huko maeneo ya Chaugingi mjini Njombe.

Amesema Kawongo aliiba silaha na kuitumia kufanya uhalifu ambapo alifanya matukio kadhaa Mkoani Iringa ikiwemo kumshambulia Askari kwa panga hali iliyosababisha wafungwa wengine kutoroka.

“Hii ni silaha ambayo askari magereza wanaitumia katika ulinzi wa wafungwa hao sasa huyu kwakuwa ni mhalifu akawa anaitumia katika kufanya uhalifu,” Kamanda Issah.

Amesema silaha hiyo ilikuwa na risasi kumi lakini mpaka inakamatwa na askari ilikuwa imebakiwa na risasi mbili pekee huku risasi nane zikitumika kufanya ualifu maeneo tofauti ikiwemo tukio hilo lilotokea Mkoani Njombe la kumjeruhi kaka yake.

Amesema licha ya juhudi kufanyika za kutaka kuokoa maisha yake ili alieleze Jeshi la Polisi namna alivyoondoka na silaha lakini ilishindikana kwa kuwa umauti ulimfika.

” Ukimnyang’a askari silaha namna pekee ya kuipa hiyo silaha ni kwa kutumia silaha hivyo wanapaswa kuwa makini,” Kamanda Issah
Hii story haina principles za uandishi Kama
What
When
Where
How
 
Kaka na mdogo wake wanatofautiana umri kwa miaka 37!!
Umenifanya nipige hesabu tofauti ya mimi na first born wetu. Inawezekana ndio familia zile za wake wengi, Mzee ana miaka 60 anaoa kadogodogo anaendelea kufyatua
 
KWA AMBAO HAWAJAELEWA

Askari magereza aliwapeleka wafungwa kufanya kazi. Walikuwa jumla ya wafungwa wanne.

Kazi ilihusisha utumiaji wa panga. Sasa nyampara katika kundi hilo ambaye ndiye mtajwa hapo juu akam-time askari kashangaa akamshushia panga la haja.

Baada ya askari magereza kwenda chini,wakamnyang'anya hiyo bunduki na kutokomea.

Ndiyo hiyo bunduki akaenda kumjeruhi nduguye. Hata hivyo wote baadae walipatikana.
 
Juzi askar wa Iringa walichachamaa kutafuta wafungwa, inasemekana walikua kazini wakampiga askr magerz na mapanga halafu wakatoroka na bunduki.
Sasa story ya hapo juu inachanganya sijui inazungumzia tukio la Njombe au hili la Iringa.
 
Back
Top Bottom