Njombe: Miaka 12 sasa ujenzi wa ofisi ya mtaa haujakamilika, Chapangishwa chumba elfu 50 kwa mwezi kama ofisi, wananchi wahofia faragha ofisini

Njombe: Miaka 12 sasa ujenzi wa ofisi ya mtaa haujakamilika, Chapangishwa chumba elfu 50 kwa mwezi kama ofisi, wananchi wahofia faragha ofisini

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Licha ya Mtaa wa Kambarage kuwa na idadi kubwa ya wakazi zaidi ya mitaa mingine yote ya mjini Njombe changamoto kubwa inayoendelea ni kushindwa kumaliza ujenzi wa ofisi yake ulioanza miaka 12 iliyopita.

Mtaa huu unaokaliwa na wakazi 15,195, unahudumiwa katika chumba kimoja kidogo cha kupangisha ambapo wananchi wanailipa kodi ya pango ya shilingi elfu 50 kila mwezi.

Kutokana na mazingira haya, wananchi wanakutana na changamoto kubwa ya kutokuwa na faragha wakati wanapohitaji huduma za kiserikali.

Jambo linalowafanya wengi kushindwa kujieleza vizuri hasa katika masuala nyeti. Hali hii imeleta hasira kwa wazee wa mtaa huu, wakiwemo viongozi wa zamani na wa sasa, ambao wanapanga kumtembelea Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe ili kujua sababu ya kutokamilishwa kwa ofisi hiyo licha ya juhudi mbalimbali.

Mwenyekiti mstaafu Pankras Matinya, aliyekuwa na jukumu la kuanzisha ujenzi wa ofisi hiyo mwaka 2013, anasema kuwa amekuwa akiepuka barabara inayozunguka jengo hilo kwa kuhisi maumivu ya kuona jitihada zake hazijathaminiwa. Mwenyekiti wa sasa, Fransis Msanga, ameongeza kuwa licha ya jitihada za kuandika barua zaidi ya 10 kwa Mkurugenzi wa Mji, msaada wa kumalizia ujenzi wa ofisi hiyo haujapata matokeo.

Diwani wa Kata ya Njombe Mjini, Alatanga Nyagawa, amekiri changamoto hii na amesema atajitahidi kushinikiza halmashauri ikamilishe ujenzi wa ofisi hii ili wananchi wa Kambarage waweze kupata huduma bora na za kistaarabu
1737713644491.png
 
Back
Top Bottom