NJOMBE MJI WAGOMEA MECHI YA SIMBA SC

Hazard CFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2015
Posts
16,627
Reaction score
38,689
-Uongozi wa klabu ya Njombe Mji hautambui kama mchezo wao na klabu ya Simba Sc utachezwa April 03 katika dimba la Sabasaba mkoani Njombe.

-Uongozi wa klabu hiyo umedai haujapokea barua yoyote kutoka Bodi ya Ligi kama mchezo wao dhidi ya Simba Sc utachezwa April 03 ila wanashangaa kuona kwenye mitandao ya kijamii tu.

-Uongozi huo umedai hautakubali mchezo huo uchezwe siku jumanne ya April 03 kwani wao wanajua wana mechi ya Robo Fainali ya Asfc dhidi ya Stand United March 30 katika dimba la Ccm kambarage Shinyanga.

-Baada ya mchezo huo Njombe Mji wamedai hawatarudi Njombe kucheza mechi dhidi ya Simba Sc bali wataweka kambi huko huko Shinyanga kusubili mchezo wa Ligi kuu ya VPL dhidi ya Stand United tena April 08.

-Njombe mji wako tayari kutocheza mchezo huo dhidi ya Simba April 03 hata washushwe daraja sawa ila hawatakubali kunyanyaswa kwa sababu ya Simba Sc.

-Mchezo wa Njombe dhidi ya Simba ulikuwa uchezwe march 12 huko Njombe ila Bodi ya Ligi iliuairisha kwa sababu ya kuipa Simba muda wakutosha kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Caf Confederation Cup dhidi Al Marsy uliochezwa March 17 nchini Misri.
 
Wanawatafutia simba ubingwa kwa nguvu hao komaeni tff karibu yote simba
 
Hizi ni porojo...mleta uzi ameandika kwa ushabiki.Kwa nini usiweke source?
 
Kweli wanawatafutia mteremko hao jamaa watu wacheze robo fainal then siku moja kusafir mech watacheza je
 
Walishakubali kuyumbishwa na Simba mbona? Unataka msimamo upi tena?
 
Walishakubali kuyumbishwa na Simba mbona? Unataka msimamo upi tena?
Hoja ya Simba na Yanga zipo kikanuni.That's why hata Yanga utakuta wana kiporo pia.Kwa hiyo,chama cha mpira cha nchi husika huwa hakipangiwi na klabu siku ama tarehe ya kucheza.
 
Hao nao wana mikwala sana, hao ni sikio la kufa ni lazima washuke tu daraja hivo kusema eti wako teyari kushuka daraja kisa kugomea match hoja yao haina mashiko
 
Hoja ya Simba na Yanga zipo kikanuni.That's why hata Yanga utakuta wana kiporo pia.Kwa hiyo,chama cha mpira cha nchi husika huwa hakipangiwi na klabu siku ama tarehe ya kucheza.
Yanga wanna kiporo kipi? Ratiba hupangwa mapema kwa kuzingatia mashindano yote.
 
Yanga wanna kiporo kipi? Ratiba hupangwa mapema kwa kuzingatia mashindano yote.
Ulikuwa unamaanisha kwamba yanga hawana kiporo au? Waga wepesi sana kusahau ndugu zetu, msimu uliopita yanga alikuwa na viporo 4 na msimu huu hadi sasa anacho 1
 
Ulikuwa unamaanisha kwamba yanga hawana kiporo au? Waga wepesi sana kusahau ndugu zetu, msimu uliopita yanga alikuwa na viporo 4 na msimu huu hadi sasa anacho 1
Kuwa na viporo ukishiriki michezo ya kimataifa si hoja. Hoja ni namna ya kucheza viporo hivyo ukiifikiria timu pinzani.
 
Kama vipi wabaki kanda ya ziwa na mechi wapewe Simba mezani. Mwaka huu, ubingwa lazima.
 
Mnaambiwa tff n Simba na yanga
Hamtakag kukubali
 
Hao jamaa vp? wao waombe mechi isogezwe mbele sio kutoa maneno ambayo hawawez kuyarudia... mbona Yanga na Simba wakiomba wanasikilizwa? kwa nn wao?
Ishu ya kusema hamuitambui wkt ni ratiba ni upungufu mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…