Njombe: Mkusanya Mapato wa Serikali afungwa miaka 2 kwa kuiba Tsh. Milioni 12.6

Njombe: Mkusanya Mapato wa Serikali afungwa miaka 2 kwa kuiba Tsh. Milioni 12.6

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Hukumu imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Makete, dhidi ya Isaya Samwel Madoki ambaye ni mtumihsi wa Umma, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la wizi kinyume na kifungu cha 258(1) na 270 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019.

Mahakama imethibitisha kuwa mshtakiwa aliwasilisha Benki kiasi cha Tsh. 75,820,410 badala ya Tsh. 86,455,360 zilizokusanywa katika Kata za Ipelele, Kitulo, Mlondwe, Kinyika, Isapulano, lniho na Lupalilo, hivyo amebainika kuiba Tsh. 12,634,356, fedha za Halmashauri ya Makete.

Mbali na kifungo hicho, Hakimu Irvan Msacky aliyesikiliza kesi amemtaka mshtakiwa kurejesha fedha zote zilizoibiwa mara baada ya kumaliza muda wa kutumikia kifungo.

TAKUKURU NJOMBE
 
2024 anatoka.
Upo sahihi mkuu 2year = 24 months
Wafungwa uwa wanatumikia maximum ⅔ ya kifungo so its
⅔ x 24 months =16 months
Mwaka mmoja na miezi 4

So kutoka 2024 bado inasound legit
 
Hela ndogo sana hiyo kumfunga mtu wezi wa mabilioni mbona hamwafungi kina january mwigulu nk
Ushahidi mtu wangu.Ushahidi.Halafu,wanaziingiza kwenye mzunguko watu wanaendelea kuishi kwa wema.Siyo mimi nikiiba nazitunza/kuficha Ulaya unakuwa mtaji wa wazungu.
 
Mbona TAKUKURU hawa fanyi hivi na kwawale walio tajwa na CAG...🤔
 
Back
Top Bottom