NJOMBE:Mtoto wa Miaka 12 ashikiliwa kwa kumlawiti Mtoto wa Miaka kumi

DALALI MKUU

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2022
Posts
2,011
Reaction score
4,705
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia mtoto wa umri wa miaka (12) kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa darasa la nne (10) katika shule moja iliyopo Makambako mkoani Njombe.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 13, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga zungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.

Amesema tukio hilo lilitokea Aprili 4, 2024 Mtaa wa Jeshini mjini Makambako.

Amesema mwanafunzi huyo alikuwa akilawitiwa kwa ahadi ya kupewa fedha na mtuhumiwa huyo ambaye aliacha shule akiwa darasa la sita.

"Mtuhumiwa huyu anaonekana aliacha shule akiwa darasa la sita lakini amekuwa akimfanyia hivi vitendo kwa muda mrefu kwa ahadi ya kumpatia fedha," amesema Banga.

Amesema kwa muda wote huo mwanafunzi huyo hakusema kwa wazazi lakini tabia yake ilianza kubadilika baada ya kuwa anatokwa na haja kubwa na baada ya mama yake kumuadhibu, ndipo alisema kuwa anafanyiwa vitendo hivyo.
 
Ana miaka 12???
 
Huyo dogo atakua kajifunza sehem au nae alishafanyiwa hivyo vitendo nae akatafuta wa kumfanyia.Jamani sasa hivi si kulinda mtoto wa kike tu hata wa kiume nao wanahitaji uangalizi.Unaweza jua umezaa dume la mbegu kumbe mtoto ni mchicha mwiba kitambo.
 
Back
Top Bottom