Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 433
Soma pia: Bukoba: Zaidi ya nyumba 300 zazingirwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha
Mvua yabomoa, kuezua mabati kwenye nyumba tano huko Makambako mkoani NjombeNyumba tano zilizopo Mtaa wa Idofi, Kata ya Mlowa mjini Makambako mkoani Njombe zimeharibiwa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha jana, hali iliyosababisha baadhi ya nyumba kuharibika.
Katika tukio hilo, nyumba mbili zimebomolewa kuta huku tatu zikiezuliwa paa, hali iliyowaacha wakazi wake katika mazingira magumu na kukosa hifadhi ya uhakika.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Idofi, Cosmas Sambala amethibitisha kutokea kwa maafa hayo jana Januari 21, 2026, akieleza kuwa baada ya kupokea taarifa walifika eneo la tukio na kujionea uharibifu uliosababishwa na mvua hiyo.
Amesema baada ya kubaini ukubwa wa tatizo, aliwasiliana na Diwani wa Kata ya Mlowa na kwa pamoja wakaweka mikakati ya kuwaita wananchi kupitia kupiga ngoma ili wakusanyike na kuchangia walichonacho kusaidia waathirika.
Sambala amewashukuru wananchi wa Mtaa wa Idofi kwa kujitokeza kwa wingi kuchangia, akibainisha kuwa hadi sasa changamoto imepunguzwa kwa kiasi kikubwa isipokuwa nyumba moja ambayo uharibifu wake ni mkubwa bado inahitaji msaada zaidi.Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi.