Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Njombe Rose Mayemba amedai kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jana, Novemba 27.2024 nchini kote haukuwa uchaguzi kama ilivyodhaniwa badala yake ilikuwa ni oparesheni kuwashughulikia wapinzani nchini
Rose ameeleza hayo alipofanya mahojiano na Jambo TV mapema leo, Alhamisi Novemba 28.2024 ambapo amedai kuwa katika mkoa wa Njombe idadi kubwa ya mawakala waliondoshwa kwenye vituo vya kupigia kura wakati zoezi la upigaji kura lingali linaendelea, na wale waliokuwa wabishi kutoka walikuwa wakitolewa kwa nguvu na askari bila kupewa maelezo yoyote
Amesema baadhi ya mawakala walichelewa kuingia vituoni (kwenye vyumba vya kupigia kura) kutokana na kucheleweshwa kupata barua za utambulisho kutoka kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri, huku baadhi ya maeneo yakitaarifiwa kuingizwa kura feki alizodai kuwa zimetumika kuwapa ushindi bandia Chama cha Mapinduzi (CCM)
Ametolea mfano vurugu zilizoibuka jimbo la Njombe mjini, kata ya Mji mwema, mtaa wa Mji mwema kwenye kituo cha Msete ambapo yeye binafsi alipokea taarifa kuwa kuna njama zinaandaliwa kubadilisha matokeo ya kituo hicho kutokana na kile kilichoelezwa kuwa eneo hilo ni 'ngome' ya CHADEMA na ilikuwa vigumu kura feki kuingizwa kituoni hapo
Amedai walipoona njia ya kuingizwa kura feki imeshindikana ndipo wakaamua kubeba masanduku ya kura na kupeleka kwenye eneo wanalolijuwa wenyewe, wakati mpango huo mbaya unaandaliwa ndipo Rose Mayemba alipopata taarifa na kukimbilia eneo hilo, na kukuta kweli masanduku yanahamishwa kabla kura hazijahesabiwa
Anasema alipoona hivyo alihoji sababu inayopelekea kuondoa masanduku kituoni kabla kura hazijahesabiwa ndipo akajibiwa kuwa hayo ni maelekezo kutoka juu kuwa kura zote zikahesabiwe kwenye kituo cha majumuisho jambo ambalo hakukubaliananalo na katika majibizano hayo mwisho waliondosha masanduku hayo kwa nguvu
Ameendelea kudai kuwa katika kituo hicho idadi ya wapiga kura waliojitokeza ni ndogo hivyo masanduku ya kura hayakuwa na karatasi nyingi za kura lakini kwenye gari iliyopakiwa masanduku kulikuwa na masanduku mengine yaliyojaa kura.