Njombe: Prof. Mkenda azindua nyumba pacha ya Walimu wa Shule ya Sekondari ya Lubonde

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkendaleo Oktoba 03, 2024 amezindua nyumba pacha ya Walimu wa Shule ya Sekondari ya Lubonde iliyopo katika Kata ya Lubonde Wayani Ludewa Mkoa wa Njombe.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Waziri Mkenda amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameazimia kuboresha mazingira ya Walimu nchini.

Prof. Mkenda amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia kwa kujenga shule, madarasa na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule ikiwemo kuwekeza katika Shule za Sekondari mkondo wa Amali za kiufundi na zisizo za ufundi.
WhatsApp Image 2024-10-03 at 21.20.40_c6607676.jpg

WhatsApp Image 2024-10-03 at 21.20.40_422de63a.jpg

WhatsApp Image 2024-10-03 at 21.20.41_42a6c468.jpg
Naye, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Joseph Kamoga amesema kata hiyo haikuwa na shule ya Sekondari mpaka Mwaka 2022 ndipo serikali ilipotia fedha kwa ajili wa ujenzi wa shule hiyo.

Mbunge huyo ameongeza kuwa wananchi wa kata hiyo kwa hamu kubwa ya kuwa na sekondari walitoa eneo bure pamoja na kuchangia nguvu zao katika ujenzi wa shule hiyo pamoja na nyumba ya walimu jambo ambalo lilisaidia kuwa na bakaa ya fedha.

Naye, Mkuu wa shule ya Sekondari Lubonde Willy Chaula amesema kuwa serikali kupitia Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ilitoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ambapo shilingi milioni mbili zimebaki.

Chaula amesema kuwa ujenzi wa nyumba hiyo umepumguza changamoto ya Walimu kukaa mbali ya eneo la shule na kuimatisha ulinzi na usalama wa wanafunzi kwa kuwa Walimu wapo karibu na eneo la shule.
 
Tupe mchanganuo wa gharama zilizotumika kufanikisha ziara hiyo ya waziri kwenda kuzindua nyumba hiyo
 
Vitu vya kifala sana... Mkurugenzi yupo,Mkuu wa Wilaya yupo Afisa elimu yupo...mpaka Waziri aende kuzindua nyumba !?? Asee
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkendaleo Oktoba 03, 2024 amezindua nyumba pacha ya Walimu wa Shule ya Sekondari ya Lubonde iliyopo katika Kata ya Lubonde Wayani Ludewa Mkoa wa Njombe.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Waziri Mkenda amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameazimia kuboresha mazingira ya Walimu nchini.

Prof. Mkenda amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia kwa kujenga shule, madarasa na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule ikiwemo kuwekeza katika Shule za Sekondari mkondo wa Amali za kiufundi na zisizo za ufundi.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Joseph Kamoga amesema kata hiyo haikuwa na shule ya Sekondari mpaka Mwaka 2022 ndipo serikali ilipotia fedha kwa ajili wa ujenzi wa shule hiyo.

Mbunge huyo ameongeza kuwa wananchi wa kata hiyo kwa hamu kubwa ya kuwa na sekondari walitoa eneo bure pamoja na kuchangia nguvu zao katika ujenzi wa shule hiyo pamoja na nyumba ya walimu jambo ambalo lilisaidia kuwa na bakaa ya fedha.

Naye, Mkuu wa shule ya Sekondari Lubonde Willy Chaula amesema kuwa serikali kupitia Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ilitoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ambapo shilingi milioni mbili zimebaki.

Chaula amesema kuwa ujenzi wa nyumba hiyo umepumguza changamoto ya Walimu kukaa mbali ya eneo la shule na kuimatisha ulinzi na usalama wa wanafunzi kwa kuwa Walimu wapo karibu na eneo la shule.
Aka kajumba hakana fance, compound ata mpangilio wa aina wote waziri ndo aende kuifungua hiyo ni cheap politics, kangefunguliwa na ofisa elimu kata.
 
Back
Top Bottom