Hao unaosema wanapanga foleni wanafanya kazi na kuongeza pato kubwa sana la taifa kuliko wewe unayeshinda na simu jf. Vijana ukimwi upo na hakuna asiyefahamu hilo ndio maana sasa hivi tunapambana na unyanyapaa ili kupunguza new infections. Watu kama nyie mnaturudisha nyuma sana na unyanyapaa wenu. Sijaona cha maana ulichoandika hapa zaidi ya kuonesha upumbavu ulionao. Mimi kuna watu nawafahamu ni waathirika lakini wanajitambua na kuendesha miradi yao ambayo wameajiri na watu wengine. Hakuna mtu asiyekuwa na taarifa kuhusu maambukizi, athari na kujikinga na huu ugonjwa lakini mambo yanakwenda kama yalivyo. Pigana kuondoa unyanyapaa ili kupunguza maambukizi mapya!!!