Njombe: Wananchi wafunga ofisi ya kijiji wakidai mwenyekiti anahujumu uchumi wa kijiji

Njombe: Wananchi wafunga ofisi ya kijiji wakidai mwenyekiti anahujumu uchumi wa kijiji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wananchi wa kijiji cha Ngelenge wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wamelazimika kuifunga ofisi ya mwenyekiti wa kijiji chao Bwana Thomas Mkinga wakimtuhumu kuwa anahujumu uchumi wa kijiji huku wakimtaka ajiuzulu kwenye nafasi yake.
IMG-20230705-WA0002.jpg

Frolence Haule ni mmoja wa wananchi wa kijiji hicho ambapo amesema mwenyekiti amekuwa akikusanya pesa za ushuru na kufanyia matumizi binafsi na wanapohitaji mikutano kwa ajili ya taarifa ya mapato na matumizi amekuwa akikataa kuitisha huku Avelina Mbonde akieleza kuwa hawahitaji kuongozwa tena na mwenyekiti huyo.
IMG-20230705-WA0001(1).jpg

Mkinga alipoulizwa juu ya tuhuma hizohakuweza kuzungumza chochote akidai mpaka atakapopata kibali kutoka ngazi za juu.

Victoria Mwanziva ni mkuu wa wilaya ya Ludewa amesema wanaendelea kufanya uchunguzi juu ya jambo hilo sambamba na kusuruhisha mgogoro huo ili wananchi waendelee kupata huduma kupitia ofisi hizo.
IMG-20230705-WA0000.jpg

"Niwaase viongozi wa ngazi zote kupeuka migogoro na wananchi na zinapotokea kesi mbalimbali watatue kwa wakati ili kutoathiri utendaji kazi na utoaji wa huduma"amesema DC Mwanziva
 
imagine nguvu kama ikawa scaled up to the national level..nchi ingenyooka
 
Wangemcharaza na fimbo, ili kumkanya siku nyingine aheshimu pesa za umma

Ipo siku wananchi Tz nzima wataamka ni kitendo cha muda tu.
 
Eti mwenyekiti anahojiwa kupitia tuhuma hizo, anajibu hawezi zungumza chochote hadi apewe maelekezo na ngazi za juu.

Hizo ngazi za juu ni zipi? Na hizo ngazi za juu ndo zinabariki au zinamtuma afanye ubadhirifu huo? Hii nchi imekuaje kwan?

Inakera na kuboa sasa, aaaah.
 
Back
Top Bottom